Thursday, June 12, 2008

Bajeti 2008/2009.Wenye magari wapata ahueni kidogo

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI
MHESHIMIWA MUSTAFA HAIDI MKULO (MB.),
AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2008/2009

Sheria zinazosimamia Kodi za Magari
Mheshimiwa Spika, inapendekezwa kufanya marekebisho yafuatayo katika kodi za magari:-

(i) Kupunguza viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari kama ifuatavyo:-
(a) Kwa magari yenye ujazo wa ingini usiozidi cc500 kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 30,000;

(b) Kwa magari yenye ujazo wa injini unaozidi cc500 lakini hauzidi cc1500 kutoka shilingi 80,000 hadi shilingi 50,000;

(c) Kwa magari yenye ujazo wa injini unaozidi cc1500 lakini hauzidi cc2500 kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 120,000;

(d) Kwa magari yenye ujazo wa injini unaozidi cc2500 lakini hauzidi cc5000 kutoka shilingi 330,000 hadi shilingi 140,000; na

(e) Kwa magari yenye ujazo wa ingini unaozidi cc5000 kutoka shilingi 175,000 hadi shilingi 150,000.

(ii) Kusamehe ada ya mwaka ya leseni za magari kwa matrekta ya kilimo

(iii) Kuongeza viwango vya ada ya usajili wa magari kutoka shilingi 27,000 kwa pikipiki na shilingi 90,000 kwa gari, hadi shilingi 35,000 kwa pikipiki na shilingi 120,000 kwa gari. Ada hii inalipwa mara moja tu na mwenye gari.

Hatua hizi kwa pamoja zitapunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi 2,380 milioni.

No comments: