Saturday, June 21, 2008

Shuhuda..! Shuhuda...! Shuhuda..!

Haleluyaa watumishi wa Mungu.

Kwa muda mrefu nimekuwa kimya kidogo kwa kutoonekana mlimani sayuni kwa kuwa nimekuwa nikibanwa na majukumu mbalimbali ikiwemo kuwaombea wapendwa wengi wenu mliokuwa mmetutumia mahitaji yenu. Na sisi kwa kuwa tumeitiwa kuwaombea watu wenye mahitaji BURE kabisa kwa jina la YESU,wengi wamekuwa wakipokea mahitaji yao kupitia blogu yenu hii ya kikristo.Mambo mengine ni ya siri na si vyema sana kuyaanika hapa hadharani bila ruhusa ya wahusika.

Kwa kuliona hili sisi wanasayuni tumeonelea ni vyema sasa tukawa tunapokea shuhuda mbalimbali kutoka kwenu kwa yale mambo ambayo Mungu amekuwa akifanya katika maisha yenu kupitia makanisani kwenu/kwenye huduma zenu au kupitia mlima huu wa sayuni.Tutumie shuhuda motomoto ili wengine wanapozisoma waweze kujengwa kwani shuhuda zinainua imani.

Tutumie shuhuda zako kwa email zetu hizi hapa nasi tutaziweka hapa ili wapendwa wazisome na kutiwa moyo na kumtukuza Mungu pamoja na wewe:

1.Mtade (Dar,Tanzania),Email: miwlc@yahoo.com

2.Maranatha(Oslo,Norway), Email: chalujohn@yahoo.com

3.SavedLema(Arusha,Tanzania), Email: savedlema2@yahoo.com

4.Kalenga(Ottawa,Canada,),Email:hkalenga@mirarco.org

5.Sauti ya Nyika (Dar,Tanzania),Email:jsiulapwa@yahoo.com

Tuma ushuhuda wako wa jambo lolote ambalo Mungu amekufanyia kwenye email yoyote hapo juu nasi tutamtukuza Mungu kwa kuweka hapa juu ya mlima ili watu wote waone na walitukuze juna la Bwana Mungu wetu wa majeshi.

1 comment:

Maranatha said...

Point of correction kwa sasa naripoti toka Australia mpaka wakati ambao Bwana ataona vema!