Wednesday, June 4, 2008

Mtanzania aendelea kutesa riadha ujerumani

Katika hali ya kufurahisha sana,mtanzania anayeishi nchini Ujerumani mtumishi wa Mungu Faustin Baha kwa mara nyingine amefanikiwa kuipatia sifa njema Tanzania kwa kushika namba moja katika mashidano ya riadha yaliyofanyika nchini ujerumani mapema mwezi may mwaka huu.Faustin amekuwa ni balozi wetu mwema sio tu kwa nchi yake ya Tanzania bali zaidi sana katika mwili wa Kristo.Faustin ambaye ameokoka na anampenda na kumwishia Bwana wetu YESU katika maisha yake akiwa nchini ujerumani amewahi kushinda mara kadhaa mashindano mbalimbali nchini humo kwa kushika nafasi ya tatu,ameiambia blogu ya sayuni kuwa anamshukuru sana YESU na kumrudishia utukufu wote kwani mara hii amefanikiwa kushika namba moja kati ya watu 8000 walioshiriki mbio hizo.

Wadau wa mlima sayuni tunampa hongera mtumishi Faustin na kumtakia mafanikio mema katika mashindano ayaendeyao siku zijazo.Biblia imeahidi kuwa sisi ni vichwa na wala sio mkia.

Deuteronomy 28:13 "And the LORD will make you the head and not the tail; you shall be above only, and not be beneath, if you heed the commandments of the LORD your God, which I command you today, and are careful to observe them. "

Utukufu kwa Mungu.

No comments: