Juzi na jana kumekuwepo na mijadala mikali inayoendelea radio wapo fm kuhusu walokole kushiriki kwa namna yeyeote ile mashindano ya umiss.Mwinjilisti Alfonce Temba ambaye ni moja kati ya watumishi wanaochipua kwa kasi sana hapa jijini Dar amekuwa akifundisha na kuhojiwa na wananchi kuhusu kuunga mkono kwake kwa wakristo kushiriki mashidano ya umiss na jinsi anavyounga mkono kwa mtoto wa askofu Deo Lubala anayeitwa Angela Deo Lubala kushiriki mashindano ya umiss Chang'ombe na kushinda huku akiungwa mkono na baba yake na mama yake mzazi ambao ni watumishi wa Mungu wanaoliongoza kanisa la Word Alive lilipo Sinza jijini Dar.
Mlima sayuni tunafanya mkakati wa kufanya mahojiano na Mwinjilisti Alfonce Temba ili kuweza kujua msimamo wake.
1 comment:
Ili kuikubali hii philosophy yake ya waliokoka kuanza kutembea uchi majukwaani aje na vifungu vya kwenye Biblia vinavyoonesha uhalali wa kufanya hivyo. Nachelea siku moja tutakuwa na mpendwa ndani ya Big Brother na huko tutaanza kushabikia kwa nguvu zote pamoja na upuuzi unaondelea humo kwenye hilo jumba! Watu wa Mungu sidhani kama twapaswa shiriki hii kitu after all kwa ajili ya utukufu wa nani?
Post a Comment