Thursday, November 27, 2008

KUKAMATWA KWA VIONGOZI WA SERIKALI TANZANIA WAKRISTO TUFANYE NINI?

Shalom watu wa MUNGU!


Nimekuwa nikifuatilia hali ya mambo ya kisiasa na matukio ya kupelekwa mahakamani kwa watu ambao hakika tusingeweza dhania kwa siku za huko awali. Hivi punde tumesikia juu ya watuhumiwa wa EPA na pia juzijuzi Mh. ndugu Mramba na Daniel Yona na tetesi zinasema bado wengine wengi wako mbioni kuelekea mkono wa sheria.

Sasa basi kama kanisa na watu wa MUNGU, Je! Tuhesabu kwamba huu ni ushindi wa maombi mengi ya watu ambayo wamekuwa wakifanya mfano yakiwa yale yaliyofanyika Jangwani na mengineyo? Na kama kanisa je kipindi hiki tufanye nini? Tumshukuru au ndo tukaze kamba kuhakikisha kwamba hawa watu wanafungwa wote? Mh.Daniel Yona (l) na Mh. Basil Mramba wakiwa Mahakama ya Kisutu, DSM.
Nachelea sana kwa hali hii kwani isije leta namna ya mtafaruku wa amani nchini mwetu haswa pale watakapoanza kukaangana wenyewe kwa wenyewe walio kwenye mamlaka maana ndio wahusika wakuu. Ni maombi yangu kitu chochote cha kutishia uvunjaji amani kisitokee kamwe! Japo najua adui hafurahii hili kabisa!

Kama watu wa Mungu hebu tushauriane hapa Mlimani Sayuni ili tujue tunaipekaje nchi yetu TANZANIA mbele za Baba yetu aliye mbinguni.

No comments: