Wednesday, November 12, 2008

MAOMBI KATIKA MLIMA SAYUNI:BWANA MUNGU WETU AMEJIBU MAOMBI YETU

BWANA YESU ASIFIWE SANA SANA WAPENDWA WA MLIMA SAYUNI.
BINAFSI NAMSHUKURU MUNGU KWA MAOMBI HAYA YA SIKU 21.TULIANZA MAOMBI HAYA TAR 22/10/2008 NA TUMEMALIZA LEO TAR 12/11/2008.
MUNGU WETU AMEKUWA MWAMINIFU SANA KWA KUTUJIBU YALE TULIYOKUWA TUNAMWOMBA.UKISOMA KATIKA BIBLIA KATIKA KITABU CHA WAEBRANIA 11:6 INASEMA KUWA HAIWEZEKANI KUMPENDEZA MUNGU PASIPO IMANI.NA KILA AMWENDEA MUNGU LAZIMA AAMINI KUWA YEYE MUNGU YUPO NA HUWAPA THAWABU WALE WAMWENDEAO KWA IMANI KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU.
TULIKUWA NA MAMBO MATATU YA MSINGI YA KUOMBEA KATIKA MAOMBI HAYA.
1.KUHUSU TANZANIA NCHI YETU KUJIUNGA NA JUMUIYA YA NCHI ZA KIISLAMU (OIC).(TULIOMBA MAPENZI YA MUNGU KATIKA HILI KWANI ANASEMA KUWA MAPENZI YAKE NI MAKAMILIFU SIKU ZOTE.WARUMI 12:2)
2.KUHUSU NCHI YETU KUANZISHA MAHAKAMA YA KADHI NA KUUNGIZA MFUMO HUO RASMI KATIKA KATIBA YA NCHI NA KIUTENDAJI KATIKA SERIKALI YETU KWA KODI ZA WANANCHI.(HAPA PIA TULIMWAMBIA MUNGU AINGILIE KATI)
3.KUHUSU AMANI YA NCHI YETU.(WENGI MMEONA NA KUSIKIA MIGOMO,MAANDAMANO,VURUGU,MAUAJI YA MAALBINO, NA VITENDO VINGINE VINGI VINAVYOHATARISHA AMANI YA NCHI YETU).
MUNGU WETU NI MWAMINIFU KATIKA YOTE HAYO NA HAKIKA AMEJIBU MAOMBI YETU NA DUA ZETU.ANASEMA KATIKA NENO LAKE KUWA YEYE ANAJIBU KULIKO YALE TUYAWAZAYO NA KUYAOMBA PIA.
WATU WENGI WALIJITOKEZA KATIKA MAOMBI HAYA YA MNYORORO SEHEMU MBALI MBALI DUNIANI.SI TANZANIA TU ILA WATANZAIA WALIOTAWANYIKA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI WALISHIRIKI KATIKA MAOMBI HAYA.WAPO WALIOAMUA KUFUNGA NA WENGINE KUOMBA TU KWA NJIA YA KAWAIDA.WALE TULIOO DHAIFU HATUKUWEZA KUFUNGA SIKU ZOTE 21.LAKINI KADRI BWANA ALIVYOTUFANIKISHA TULIMWOMBA NA KUPELEKA DUA ZETU KWA MOYO WOTE NA KWA BIDII.WAPO AMBAO WALIPENDA KUSHIRIKI ILA WALIBANWA NA SHUGHULI ZA KAZI.NAJUA HATA WEWE MSOMAJI NA MPENZI WA MLIMA SAYUNI ULIPENDA KUSHIRIKI ILA ULIBANWA.NATAKA KUKUHAKIKISHIA KWA KUWAZA KWAKO TU BASI NA NIA YAKO NJEMA KWA NCHI YETU PIA ULISHIRIKIANA NA SISI KUOMBA JAPO HUKUNITUMIA EMAIL YAKO KUOMBA KUJIUNGA NA CHAIN PRAYER HII.WENGI WALIJIUNGA NA KUTUMA EMAIL ZAO NA NIMEZIHIFADHI KWA KUMBUKUMBU NA KAMA NILIVYOWAJIBU KWENYE EMAIL ZENU KUWA SITAWATANGAZA HAPA BILA IDHINI YENU.WAPO PIA AMBAO WALIOMBA KUJINGA NA MAOMBI HAYA LAKINI KWA BAHATI MBAYA NILISAHAU KUWAUNGANISHA NA KUWAPA PRAYER POINTS ZA KILA SIKU ZA KUOMBA PIA NAOMBA MNIWIE RADHI KWA KUTOWAJUMULISHA KWA WAKATI ILA NAJUA MLIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KUOMBA.HII ILISABABISHWA NA MIMI KUWA SEHEMU AMBAZO HAKUNA MAWASALIANO MAZURI HUKU INDIA.
WAPO PIA WALIOTUKEBEHI,KUTUPINGA KUONA MWISHO WETU WAKIDHANI TUTAISHIA NJIANI.LAKINI WOTE HAO WALIFANYIKA CHACHU KWETU NA KUTUFANYA TUENDELEE KWA BIDII KUBWA.NA HATIMAYE TUMEMALIZA MAOMBI YETU SALAMA.
SISI KAMA WATU TULIOOKOKA KAZI YETU KUBWA SI KUILAUMU SERIKALI AU MAMLAKA ILIYOPO MAANA BIBLIA INATUAMBIA KUZITII MAMLAKA NA KUZIOMBEA.KAZI YETU SISI NI KUOMBA.NATAKA NIKUHAKIKISHIE MPENDWA KUWA MAOMBI NDIO MASTER KEY.HAKUNA JAMBO LINALOSHINDIKANA KATIKA MAOMBI.MUNGU WETU NI MWAMINIFU MNO MNO NA TUNAMWAMINI KUWA AMESHAJIBU MAOMBI YETU SAWA SAWA NA NENO LAKE KATIKA KITABU CHA 2MAMBO YA NYAKATI 7:14 "IKIWA WATU WANGU WALIOITWA KWA JINA LANGU.WATAJINYENYEKEZA NA KUOMBA,NA KUNITAFUTA USO WANGU,NA KUACHA NJIA ZAO MBAYA,NITAISIKIA KUTOKA JUU MBINGUNI NA KUIPONYA NCHI YAO NA KUWASAMEHE MAOVU YAO...".
MUNGU WETU HACHELEWI WALA HAWAHI MAANA KWAKE HAKUNA MAJIRA WALA SAA.KUMBUKA KUWA HAYA MAJIRA TUNAYOYAONA HAYAKUWEPO KABLA YA MWANZO 1:1. BIBLIA INASEMA KUWA HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI.NAYO NCHI ILIKUWA UKIWA TENA UTUPU, NA ROHO WA MUNGU AKATULIA JUU YA USO WA VILINDI VYA MAJI.
MAJIRA NA SIKU NA NYAKATI ZILIANZIA HAPO MUNGU ALIPOUMBA JUA NA MWEZI NA NYOTA .MAANA TUNAPATA MASAA 24 KWA DUNIA KUZUNGUKA JUA.KABLA YA HAPO HAKUKUWA NA SAA WALA NYAKATI.KWA HIYO MUNGU WETU HAFUNGWI NA MUDA HATA KIDOGO MPENDWA.MUNGU WETU YEYE NI WA MILELE NA WALA HATAKAWIA.AMESHAJIBU TAYARI NA WALE WALIO WA ROHONI WANAELEWA KUHUSU HAYA.
MUNGU AWABARIKI SANA SANA SANA WAPENDWA KWA KUYAFANIKISHA MAOMBI HAYA.

1 Wathesalonike 5
23Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase kabisa. Roho zenu, nafsi zenu na miili yenu na ihifadhiwe bila kuwa na lawama kwa wakati atakapokuja Bwana wetu Yesu Kristo. 24Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya haya

NI MIMI MTUMWA WENU ,MIMI NILIYE MDOGO MIONGONI MWENU,MTENDA KAZI ASIYE NA FAIDA.
MTADE

No comments: