Saturday, January 10, 2009

KWAHERI KAKA YETU SEDEKIA


BWANA YESU ASIWE WAPENZI WOTE WA SAYUNI NA PIA WOTE WALIOMPENDA NDUGU FANUEL SEDEKIA.

Hatimaye leo tarehe 10,January 2008, ile safari ya mwisho kwa hapa duniani ya kaka yetu mpendwa, muimbaji Fanuel Sedekia imefanyika leo hapa jijini Arusha.

Mwili wa kaka Sedekia (36) uliletwa kwa ndege maalumu jana na kufika hapa Arusha hospitali ya mkoa majira ya saa 12 kamili jioni ulipohifadhiwa hadi leo asubuhi.

Leo asubuhi mwili wake uliletwa katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid hapa Arusha ulipowekwa kutoa nafasi kwa watu walioweza kufika kutoa heshima zao za mwisho kwa kaka yetu.
Baadaye mwili wake ulipelekwa kuzikwa katika makaburi yaliyopo Njiro hapa Arusha.

Zoezi hilo limefanyika leo na hii ni taarifa fupi tuu kwenu kuwajulisha kilichotokea. Kesho nitawaletea picha kadhaa na maelezo zaidi kuhusu tukio hili la aina yake.

"Yes, brother Sedekia, We will meet on that beatiful shore when the time of the Lord comes"

MUNGU UNABAKIA KUWA MUNGU HATA KAMA HUKUJIBU KAMA TULIVYOTAKA SISI.

2 comments:

Anonymous said...

Kaka Sedekia Tulikupenda lakini Mungu kakupenda zaidi. Jina la Bwana na libarikiwe. Nimepokea hizi taarifa kwa huzuni, Natoa pole kwa familia yake, tupo wote katika majonzi. Ameni

Anonymous said...

Kaka Sedekia Tulikupenda lakini Mungu kakupenda zaidi. Jina la Bwana na libarikiwe. Nimepokea hizi taarifa kwa huzuni, Natoa pole kwa familia yake, tupo wote katika majonzi. Ameni