Friday, October 8, 2010

Strictly Gospel yazidi kuchanua

Kundi La Strictly Gospel Lajipanga!


Pichani Mchungaji Abel Orgenes Akiombea Viongozi Wa Kundi

Kundi La Strictly Gospel limejipanga kuanza kufanya kazi ya Mungu kwa vitendo. Akiongea kwenye mkutano wa wana SG uliofanyika tarehe 18/9/2010, kiongozi wa kikundi Bi. Mary Damian alisema: “Tunahitaji tuwafikie wengine, tunahitaji kutatua matatizo yaliyopo kwenye jamii yetu, Tuwaambie watu Waache Kufanya Maovu Wamgeukie Mungu. Tuwafikie wafungwa, wagonjwa wa hospitalini, yatima na kuwahubiri masikini habari njema za Bwana Yesu pia kuwategemeza wachungaji wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu”

Bi Mary Aliendelea Kusema “Tunahitaji watu wenye huduma na wito wa kumtumikia Mungu, japokuwa watu wako busy na majukumu mbalimbali inawezekana kuutoa muda wao hata kwa siku moja na kufanya kazi ya Mungu hali ambayo tasaidia kusimama imara na kuwa karibu na Mungu”

Dada Rose Lusinde Kwenye Maombezi

Mkutano Huo Ulifanyika Jijini Dar es salaam Na Kuhudhuriwa na wajumbe wa kikundi cha Strictly Gospel na kupanga mikakati ya kuanza kazi mara moja Oktoba mwaka huu. Akiongea kwenye mkutano huo, mgeni mualikwa Mchungaji Abel Orgenes Alisema “Huu ni wakati mzuri wa kumtumikia Mungu, watu wanapata fursa kupitia kundi hili pasipo kujali madhehebu yao”

Kundi la Strictly Gospel Group linataraji kuanza huduma hizo kuanzia October mwaka huu na kuanzia January 2011 Watakuwa wakifanya semina na matamasha mbalimbali ya Injili. kwa maelezo jinsi ya kujiunga na kundi hili wasiliana nasi kwa simu. +255 715 730 813, +255 752 730 813.


Strictly Gosple ni moja ya blogu za kikristo zinazofanya vizuri sana sana sana hapa nchini na hata nje ya mipaka ya Tanzania ikiwa chini ya mbeba maono na mwanzilishi wa kundi hili mpakwa mafuta dada Mary Damiani.

Ukitaka kujua mengi kuhusu SG tembelea blogu yao hii hapa http://strictlygospel.wordpress.com/


Source: http://strictlygospel.wordpress.com/

No comments: