Tuesday, January 15, 2013

Apostle Peter Nyaga vs Polisi

Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa

JESHI la Polisi  Ilala, jijini Dar es Salaam  walilazimika  kuwapiga mabomu  waumini na mchungaji wao waliokuwa wamekusanyika katika mkutano wa Injili uliokuwa ukifanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Liwiti, Tabata Januari 6, mwaka huu .
Mchungaji Peter Nyaga akihubiri Neno la Mungu Tabata Liwiti.
Imeelezwa na baadhi ya mashuhuda kwamba, askari polisi walilazimika kutumia mabomu kuwatawanya watu waliohudhuria mkutano huo kwa madai kwamba muda wao wa kufanya mkutano…
Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
JESHI la Polisi  Ilala, jijini Dar es Salaam  walilazimika  kuwapiga mabomu  waumini na mchungaji wao waliokuwa wamekusanyika katika mkutano wa Injili uliokuwa ukifanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Liwiti, Tabata Januari 6, mwaka huu .
Mchungaji Peter Nyaga akihubiri Neno la Mungu Tabata Liwiti.
Imeelezwa na baadhi ya mashuhuda kwamba, askari polisi walilazimika kutumia mabomu kuwatawanya watu waliohudhuria mkutano huo kwa madai kwamba muda wao wa kufanya mkutano ulikuwa umeisha, hivyo walitakiwa kutawanyika.
Mkutano huo ambao ulianza Desemba 29, mwaka jana na hitimisho lake lilikuwa siku hiyo waliyopigwa mabomu, ulikuwa ukiongozwa na Mchungaji Peter Nyaga wa Kanisa la GRS.
 Kati ya waumini waliopata madhara ya mabomu hayo ni baadhi ya wasanii akiwemo Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ambaye alijitahidi kuwasihi polisi kuacha kuwapiga mabomu waumini bila mafanikio.
Katika mkutano huo kulikuwepo pia wana kwaya kutoka nje ya nchi na wasanii wengine wa Tanzania waliotumbuiza kama vile Christina Shusho na Upendo Nkone.
Vyanzo vyetu vya habari vilieleza kwamba mara baada ya polisi kufika katika viwanja hivyo saa 11;55, walimwamuru Mchungaji Nyaga ambaye wakati huo alikuwa akiombea taifa na viongozi wake kushuka kutoka jukwaani na kuondoka, jambo ambalo alilitekeleza lakini liliwachukiza waumini.
 ‘’Sijui ni kitu gani kiliwafanya polisi kutoa amri ya kutawanyika hata kabla ya saa 12;00, wakati siku zote walikuwa wakitulinda hadi mkutano unapoisha kati ya saa 12;15 hadi saa 12;30,” alisema Thomas John mmoja wa wahudhuriaji.
Mchungaji Nyaga alipohojiwa alisema: “Ingawa nilikuwa na kibali kutoka serikalini na uongozi wa shule juu ya mkutano huo lakini sikupenda kupingana na polisi, nilitii amri yao japokuwa ilikuwa  saa 11;55.”
Akaongeza: “Mikutano ya kiroho ni tofauti na ya kisiasa kwani wakati fulani watu unaowaombea wanaweza kupandwa na mapepo sasa huwezi kukatisha maombi eti kwa kuwa muda umekwisha wakati mapepo hayajaondoka, nawashauri (polisi) wawe wanaangalia mambo kama hayo hasa inapofanyika mikutano ya kidini.”
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Liwiti, Veronica Mbalamwezi ambaye viwanja hivyo vipo katika eneo lake, alikiri kutoa kibali cha mkutano huo wa Injili  wa siku tisa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Marietha Minangi alipoulizwa sababu ya polisi kutumia mabomu  katika mkutano huo alisema kwamba mkutano huo haukuwa na kibali cha polisi bali walitumia kibali cha serikali ya mtaa kitu ambacho ni kuvunja sheria, hivyo taratibu hazikukamilishwa.
Kamanda huyo amewataka watu wote wanapotaka kufanya mikutano iwe ya kidini au siasa wajue kuwa wenye mamlaka ya kutoa kibali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa eneo husika ni polisi  na siyo serikali ya mtaa.

Source: GlobalPublishers

No comments: