Hili ndilo kanisa la Calnel Centre mbeya lipo katibu na kiwanja cha ndege mwanjelwa Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel Centre
Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai kuwa ni
mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea juzi katika kanisa hilo lililopo Airport Jijijini
Mbeya baada ya Mchungaji huyo kupokea ujumbe mfupi katika simu yake ya mkononi
kutoka kwa Mwanamke anayedai alikutwa mke wake ambaye waliachana miaka mine
iliyopita.
Mchungaji
huyo akiwa mbele ya wazee wa kanisa, Familia yake, waumini pamoja na wanahabari
alisema sababu ya kuwakusanya watu hao kumetokana na mwanamke huyo
aliyejulikana kwa jina la Sabina Lameck akitaka kutubu kwa mabaya aliyomtendea
mumewe.
Hata
hivyo baada ya mwanamke huyo kupewa nafasi ya kuanza kujieleza alianza
kumtuhumu muumini wa kanisa hilo kuwa anauhusiano na mchungaji ambaye ni mumewe
wa ndoa ambapo pia alidai kuwa mwanamke huyo alichukua nguo za mchngaji na
mkewe kwa madai ya kupeleka kwa mganga ili kusudi awasaidie warudiane.
“
Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa sababu alizichukua ili
apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane na mchungaji lakini
badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi anataka kuolewa yeye,”
alisema Mwanamke huyo.
Kwa
upande wake mchungaji Jongo alimtuhumu mwanamke huyo kuwa ni mshirikina na
kwamba sababu ya kutengana naye ni kutokana na mwanamke huyo kuzaa na mwanaume
mwingine nje ya ndoa hali aliyosema alidhalilishwa kama mchungaji.
“
Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane alianza kunivurugia huduma
ambapo waumini walianza kupungua kanisani nayeye kwenda kwa waganga wa kienyeji
kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema mchungaji huyo na kuongeza.
“
amekuja leo hapa baada ya kusikia mimi nataka kuoa muumini wangu ambapo yeye
ameanza kumzushia kuwa ni mshirikiana kitu ambacho si cha kweli lakini kama
kuna ukweli wowote utajulikana kwa sababu Mungu yupo,” alisisitiza Mchungaji
huyo.
Hata
hivyo usuluhishi huo haukufika mwafaka baada ya kuibuka kwa malumbano hali
iliyomlazimu msimamizi wa usuluhisho huo Askofu wa kanisha hilo laiyejulikana
kwa jina moja la Pasta Lugito kuahilsha mazungumzo hayo huku wakimpiga marufuku
mwanamke huyo kukanyaga katika makazi ya mchungaji.
Source:http://eddymoblaze.blogspot.com/2013/01/mchungaji-aachana-na-mkewe-kwa.html?zx=f963f3ff79b788d9
|
No comments:
Post a Comment