Unakumbuka hizi picha?
Siku Mzee Moses Kulola (Askofu mkuu wa EAGT) alipokumbatiana na Mzee Emmanuel Lazaro wa TAG pale kanisani Full Gospel kwa Askofu Kakobe.
Siku hii ilikuwa ni siku maalum ya kupatana kwa maaskofu wetu hawa wawili baada ya utengano wa muda mrefu wa kanisa la TAG na EAGT.Japokuwa siku hii watumishi hawa wa Mungu walisema hawakuwa kuwa na ugomvi wowote kati yao ila watu ndio walikuwa wakiwazushia.Walikumbatiana kwa furaha sana na hao wawili ni wake zao wakikumbatiana pia kwa furaha.
Picha hii hapa chini ni Mwimbaji wa injili wa siku nyingi Mtanzania anayeishi Kenya Faustin Munishi akiwa na Mchungaji Mwasota wakipiga picha na Askofu Moses Kulola enzi hizi injili ilikuwa si ya mzaha kama ilivyo sasa kuna wasanii wengi wamejiingiza makanisani.Picha hii ilipigwa miaka ya mwishoni mwa sabini au mwanzoni mwa themani.Mchungaji mwosota pia alikuwa ni mwimbaji maarufu hasa kwenye mikutano ya mzee kulola.Hata leo hii wote wawili Munishi na Mwasota bado wanaimba na niwachungaji.
No comments:
Post a Comment