Monday, June 9, 2008

Mtoto wa Mchungaji awa miss Chang'ombe

Mtoto wa Askofu Mkuu wa kanisa la kipentekoste la Word Alive Mchungaji Deo Lubala, Bi. Angela Deo Lubala, ameshinda taji la Miss Chang’ombe, baada ya kuwashinda wasichana wengine tisa alioshindanishwa nao.
Wakati Angela akivishwa ‘taji’ hilo wiki iliyopita katika ukumbi wa TTC Chang’ombe, Askofu na mama Askofu Clara Lubala walikuwepo ukumbini na walionesha kufurahia ushindi huo.
Walokole wengi wanayaona mashindano hayo kuwa yako kinyume na mpango wa Mungu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo washiriki wa mashindano hayo kuwa katika mavazi yasiyo na heshima kama vile vimini na zile zinazoonesha maumbile ya washiriki.
……katika mahojiano askofu alisema mtoto wake alitaka kushiriki mashindano hayo ili atumie nafasi ya u-miss kufikisha ujumbe wa Mungu kwa watu wengi zaidi. “Alitumia fungu fulani kutoka katika zaburi sikumbuki vizuri lakini katika kiingereza linasema You were created wonderfully by God” Alisema Askofu. Askofu huyo ambaye pia huchunga kanisa la Word Alive lililoko Sinza Mori, jijini Dar-es-salaam, alisema kuwa, katika utafiti wake aligundua kuwa waandaaji wa mashindano lengo lao ni kutafuta wasichana wenye uwezo wa kuwasiliana “Wanatafuta mtu wa ku-communicate, hata serikali inaweka mkono wake hapo, hakuna ngono kule, watu wana mtizamo mbaya bure mimi mwenyewe sikutegemea kama waandaaji wanaangalia na ucha Mungu” Alisema





Source: Strictly Gospel and globalpublisherstz.com

3 comments:

Anonymous said...

Tehthethehehehehe!! Sasa ulokole umeanza kuzama majini! Yaani kwa hili bado haliingii akilini mwangu kwamba nao wameingia kwenye mambo ya ulimbwende! Basi nadhani sio mbali tutawaona Leaders club kwenye mashundano ya kucheza Disco maana kama KILI awards wameshafika.

Shime mlokole hebu na tujitofautishe na mambo ya ulimwengu huu! Hatupaswi kupiga mbio na dunia hii kwani sie tu wapitaji tu! Kama ni injili na tuombe Mungu atupe mafunuo lakini sio kujiingiza kisha kusema ndo mbinu ya kuhubiri hiyo!

Anonymous said...

mimi huwa nasema kila siku huu uhuru usio na mipaka sio uhuru ila ni uhuni.hivi kweli mchungaji na heshima yako unadiriki kuingia mashindano ya umiss tena kumwona binti yako akiwa amevalia kichupi au kisketi kifupi kinaonyesha mapaja yote nje na tumbo na matiti yapo nje huku akikatika kiuno kama yupo kitandani na mume wake afu unakenua meno unamwangalia mwanao wa kumzaa.ukiulizwa unasema ni njia ya kuhubiri...God forbid....Na huyo binti kweli anawezaje kucheza uchi mbele ya baba yake mzazi na kadamnasi afu jumapili anaenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kushida umiss chang'ombe...jamani jamani jamani tunaelekea wapi lakini?afu nasikia na mama mtu alikuwepo kwenye hayo mashidano.sasa huyu mama mchungaji kampeleka mwenyewe mme wake kuona mapaja na kuchochea tamaa huko kwa warembo sasa asubiri aone huyo pastor atakavyoanza kumendea vibinti kanisani maana kasheyachochea matamaa tayari.siku nyingine huyo pastor atakuwa anaenda bar anakaa na mabar medi anasingizia anawahubiria.kuna siku mama mchungaji ataenda gesti atasema anaenda kuhubiri kuna kondoo anamwokoa....hahahahahahahhahaha.....inachekesha lakini inasikitisha sana.....
ngoja niishie hapa maana nimeshaanza kusikia kichefuchefu

Anonymous said...

Nadhani brother Kalenge nilishawahi kukuonya kwamba kuna mambo ambayo yananifanya nione kama hii dini imekaa kisanii fulani or haina mipaka lakini akaniona mimi muongo. Nilianzia pale kibwetere akipoweza kuwashawishi watu kwamba mwisho umefika kisha wakakubali.
Sasa hivi Kanisa limeshabariki ndoa za mashoga uingereza, na karibu itaingizwa kwenye mafundisho kwamba ushoga sio kosa.
Nimesikiza pia mjadala wa kuwafanya wanawake wawe maaskofu hatakama Biblia hairuhusu kama ambavyo Quran hairuhusu pia.

therefore leo anakuja mtu anasema kuwa mlokole ukashinda ni kumuenzi yesu na kuna watu kadhaa wanamfuata mchungaji huyo. Sidhani kama jamaa anafaa kuwatunza kondoo kwani huenda akawala then baadae POPE aende aombe msamaha kwaniaba ya kanisa.

Please Please rudini kwenye maandiko na watu kama hawa lazima wasiendelee kuongoza wanakondoo kwani hawanamfano mwema. baadae mutanikumbuka nimewaonya tena leo.

Mohamed Abdulrahman
UK