Monday, July 19, 2010

Mkutano wa Injili na Gospel Concert Belgium
Kipindi hiki ni cha sikukuu hapa ulaya...so wapendwa walipata nafasi kulihubiri Neno la Mungu kwa njia ya muziki wa injili siku ya jumamosi hapa St. Peters Station, Gent.Ilikuwa ni siku ya ajabu kwani watu walisikia Neno hapa kwa njia ya uimbaji na watu walimpa Yesu maisha yao.
Sheria za Gent, haziruhusu kabisa kuhubiri hadharani na watu hawapendi kusikia habari za YESU japo Belgium ni taifa la Kikristo kimakatarasi but kivitendo ni kinyemu kabisa.
Tukio hili ni mara moja tu kutokea kila mwaka wakati wa festival za yuropu.
Makanisa yote ya Gent yalikutanika hapa kuunganisha nguvu katika kuhubiri injili.Ilikuwa ni siku ya ajabu na tukio la kipekee kabisa.
Wakristo huwa wanatumia mwanye huu wa festival hizi kuhubiri injili kwa kutumia upenyo wa muziki wa injili ambao unaonyesha kuwa na nguvu sana kuwavuta watu kwa YESU kwa maeneo haya.

No comments: