Thursday, July 8, 2010

Upentekoste Tanzania na Mafanikio ya Kiuchumi

Zamani kulikuwa na msemo watu wanataniana "utakuwa maskini kama panya wa kanisani"... Msemo huo kwa sasa hauna maana tena hasa miongoni mwa wapentekoste hapa Tanzania ambapo ilionekana kuwa ukiwa umeokoka basi wewe ni maskini wa kutupwa.
mafundisho na injili ya mafanikio (najua kuna watu hawapendi hili neno la injili ya mafanikio but kwa leo naomba mvumilie maana hata Yesu alitumia muda mwingi kuhubiri injili ya mafanikio...) zimewasaidia wapentekoste wengi hasa kuanzia miaka ya mwanzo ya 90 na kuendelea , kwani wengi wameamka kiuchuni na kufanikiwa kwa kuwa wamekuwa wakiyatendea kazi mafundisho ya Yesu Kristo , mwokozi wa ulimwengu.
Tukiachilia mbali tofauti zetu za kimafundisho na kitheolojia baina ya makanisa ya kipentekoste , hakuna ubishi kuwa kuna watumishi ambao ni mfano wa kuigwa kwa kazi zao njema hasa katika jamii yetu.Wachache kati ya hao ni hawa hapa:-


Mtume & Nabii Josephat Mwingira-Efatha Ministry (Efetha Bank-first pentecostal bank in tanzania,Trenet TV station,large agricultural plantaions)
Mchunga Dr. Getrude Rwakatare-Mikocheni B Assemblies (St. Marry's International Schools and Colleges-first pentecostal highly reputable for middle & high class education systems in Tanzania, Praise Power FM-Radio Station,first pentecostal pastor to be elected as Member of Parliament)


Askofu Sylvester Gamanywa-WAPO Mission (First Pentecostal News Paper in Tanzania,First Pentecostal wide spread FM Radio in Tanzania,Most reputable pentecostal pastor by the government)

Mtume Fernandes-World Agape Ministries (First Pentecostal TV Station in Tanzania-has many viewers accross Africa)

No comments: