Thursday, February 28, 2013

Bishop Kakobe with Don Moen


WORSHIP WITH DON MOEN AT THE BISHOP ZACHARY KAKOBE MIRACLE HEALING CRUSADE IN TORONTO, CANADA.
Venue/Date: Rexall Centre Tennis Stadium, June 20-23, 2013.

Worship with the world-acclaimed worship leader DON MOEN from USA, a man who many consider "the father of contemporary worship", and the House Worship Team KRYSTAAL based in Toronto, Canada; an award winning, multi-talented group of three brothers who excel in various genres of music. It will be a music extravaganza accompanied by Biblical signs, wonders and miracles! COME ONE, COME ALL!

Wednesday, February 27, 2013

TCRA yafungia vituo viwili vya redio nchini


Makamu Mwenyekiti wa  Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano(TRCA)Walter Bugoya akitoa tamko la kuzifungia Redio Imani  na Redio Kwa Neema kwa kipindi cha miezi 6 kutokana kutangaza matangazo yanayodaiwa kuwa ya kichochezi jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mkurungenzi wa Idara ya Habrio Maelezo Arthur Mwambene na Kaimu Mkurugenzi wav Utangazaji wa (TRCA)Andrew Kisaka.Picha na Fidellis Felix 

Vilevile kamati hiyo imetoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni kwa Kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kubainika pia kukiuka taratibu za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi
re

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu ya kuvifungia muda wa miezi sita vituo viwili vya redio za dini, Imani na Kwa Neema kwa kile kilichoelezwa ni kuendesha vipindi vya uchochezi.
Vilevile kamati hiyo imetoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni kwa Kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kubainika pia kukiuka taratibu za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi kilichotafsiriwa kuwa ni cha uchochezi.

Kamati hiyo ya maudhui ilitangaza adhabu hizo jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ikisisitiza kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinazingatia maadili.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA,Walter Bugoya alisema TCRA imefikia hatua hiyo baada ya kuyafanyia uchunguzi wa kina malalamiko yaliyotolewa na wasikilizaji wa vituo hivyo vya redio.

Bugoya alisema redio hiyo ilitangazia wasikilizaji wake wasishiriki kwenye mkakati huo wa Sensa ya Taifa kwa kile walichodai kulingana na imani ya Kiislamu, wasingejua hatima ya mkakati huo.

Kuhusu Redio Kwa Neema inayorusha matangazo yake kutokea Geita, Bugoya alisema ilieneza uchochezi dhidi ya mtafaruku wa kidini uliozuka mkoani humo juu ya upande gani una haki ya kuchinja wanyama kwa ajili ya kitoweo.

Akizungumzia Kituo cha redio cha Clouds, Buyoga alisema kamati imeitaka kulipa fidia ya Sh5 milioni baada ya kubainika kuwa nacho kilienda kinyume cha maadili ya utangazaji kupitia kipindi chake cha Power Break Fast, cha Jicho la Ng’ombe walitoa kauli za uchochezi.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1705746/-/127h4m2/-/index.html

Thursday, February 21, 2013

KAHABA ALIYEOKOKA

Hili ni simulizi la  kweli linalomhusu mwanamke  mmoja ambaye alikuwa ni kahaba  wa makahaba......

Mwanamke  huyu  alijitambua  vyema  na  kukiri  ndani ya  nafsi yake kuwa hawezi  kuolewa  na maname  yoyote  yule  maana  jamii yote ilikuwa inamtambua  kwa uchangudoa  wake......

Kwa hiyo , ili kurahisisha mambo na  kuifanya  biashara  yake  iimarike, mwanadada  huyu aliamua  kwenda hospitali kukitoa  kizazi chake.Hakutaka  tena  usumbufu wa kutoa  mimba  au kufikiria kutumia kondomu......

Tangu wakati  ule biashara  yake  iliimarika na wateja  walizidi kumiminika.Baada  ya miaka  kadhaa, Upako  wa  Mungu  ulimfikia kupitia kwa mtumishi  mmoja  wa  Mungu ambaye  alifanikiwa  kumfanya  aokoke  na  kuwa mtumishi mzuri  kanisani.....
 
Siku moja, mchungaji  mmoja alimwita na  kumwambia  kuwa:
"Dada yangu, Mwenyezi Mungu  amenena  na  mimi na  kunifunulia  kuwa  wewe  ndo mke  wangu wa ndoa, hivyo naomba tuoane.."

Mwanamke huyu alitabasamu na kusema:
 "Kaka  yangu, Mungu hajakwambia lolote, lasivyo, utakuwa  hujamsikia vizuri.Naomba  uniache tu maana  sina  mpango wowote wa  kuolewa"

Yule  mchungaji  aliendelea kushikilia  msimamo wake  na  kudai kuwa :

"Mungu  amenifunulia,wewe  ndo  mke wangu" 

Mwanamke  huyu  aliendelea  kuyapuuza  maneno hayo na ndipo sakata  hilo  lilipomfikia  Askofu  wa  kanisa  hilo.....

Wakiwa mbele  ya mchungaji,Mwanamke huyu  alifunguka  kwa  uwazi mbele  ya askofu  na  kudai kuwa kabla ya kuokoka yeye  alikuwa  ni kahaba  wa  makahaba....

Askofu naye alifunguka  na  kudai kuwa :"Sioni sababu ya kuumiza kichwa  kwa  mambo yaliyopita.Mungu  humsamehe  mwanadamu  kwa  kuzifuta  dhambi zake  zote za  nyuma  na  kumfanya  awe  mpya..!!!"

Mwanamke huyu  alifunguka  tena na kudai kuwa:
"Baba  askofu, mimi  nilishatoa kizazi changu  wakati nikiwa  kahaba, kwa hiyo  sitaweza    kuzaa  tena"
Askofu  aliishiwa  pumzi baada  ya kusikia hivyo.Hakuweza tena  kusema  kuhusu  kusahau ya  nyuma.Ilibidi amgeukie yule mchungaji  na  kumwamba: 

"Vipi, bado  kuna maono yoyote  toka  kwa mwenyezi Mungu?" 

Mchungaji alijibu  ,"Ndio, huyu ndo mke wangu.."


 Askofu  ilibidi  awaombee kwa  sala  maalumu.Hatimaye ndoa  ikafungwa......Baada  ya  miezi  michachtu, huyu mwanamke  alibeba  mimba.Yeye  pamoja  na mumewe waliongozana pamoja kwenda  hospitalini, tena  kwa  yule  yule doctor  aliyekitoa  kile  kizazi......

Daktari  alipomuona  alifurahi  akidhani kuwa pengine  mteja  wake  kamletea  mteja mwingine.....Doctor  hakuamini  masikio  yake baada  ya kuambiwa kuwa  huyu  mwanamke ni mjamzito na  amekuja  kujiandikisha  clinic....
Hakika Mungu ni  Muweza wa  yote....

PICHA ZA MAZISHI YA PADRI EVARISTUS MUSHI VISIWANI ZANZIBAR

Picha za mazishi ya padri Evarist Mushi aliyeuwawa kwa kupigwa kwa risasi asubuhi ya tarehe 17 mwezi huu huko visiwani Zanzibar akijiandaa kwenye ibada kanisa katoliki parokia ya Minara miwili visiwani humo ambapo watu wasiofahamika wakiwa kwenye pikipiki walimpiga risasi padri huyo akiwa ndani ya gari lake na kufariki dunia.

















             






 

  



           


Source:http://gospelkitaa.blogspot.com/2013/02/picha-za-mazishi-ya-padri-evaristus.html

Wednesday, February 20, 2013

Breaking news...Kanisa lachomwa moto Zanzibar

images     

 WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la kipentekoste la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku.
Amesema moto huo ulizuka mara baada ya kikundi cha watu watatu kuonekana wakipita njia karibu na kanisa hilo na baada ya muda mlinzi wa kanisa hilo alisikia kanisa likishambuliwa kwa mawe juu ya maapaa.

 Picha na maktaba

Amesema baada ya mlinzi huyo kubaini kuwepo kwa hatari, alilazimika kukimbia kwenda kujificha lakini huku akiangalia kwa mbali kinachoendelea.
Kamanda Olomi amesema kuwa wakati mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni huku akiangalia kinachotokea, mara aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa na ndipo alipopiga simu kwa kiongozi wa kanisa hilo naye kuwajulisha Polisi.
Amesema Polisi walipofika hapo walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo lakini wakati huo tayari ulishateketeza thamani za kanisa hilo na vitu vingine vilivyokuwa kanisani hapo.
Kamanda Olomi amesema moto huo ungeweza kusababisha athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema.
Hata hivyo amesema uimara wa dali lililotengenezwa kwa Gibsam kumesaidia kuunusuru moto huo kuunguza mapaa na kuliteketeza kabisa kanisa hilo.
Amesema wakati uongozi wa kanisa hilo ukifanya tathimini ya harasa iliyopatikana kutokana na moto huo, Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka washukiwa kwa kutafuta taarifa kwa raia wema na bado hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusika na tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Olomi amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia matishio mengine kama hayo.

Source:http://www.fullshangweblog.com/2013/02/19/kanisa-lachomwa-moto-zanzibar/

Sunday, February 17, 2013

Haki ya kuchinja wanyama: Desturi iliyokuwepo iendelee – Waziri Mkuu

IMG_0077
Sheikh Hasani Kabeke wa Mwanza  akichangia katika kikao cha klutatafuta muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji wanyama kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Banki  Kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)


IMG_0084
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0094
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0102
Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro wa uchinjaji  wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu  jijini Mwanza Februari 16,2013.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
IMG_0122
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.
IMG_0143
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Ahmed  Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa Buswelu, Athumani Ali  katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………….
Na  Frederick Katulanda
SAKATA la nani achinje nyama kati ya Waislamu na Wakristo bado linaumiza vichwa, ambapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja nyama yaendelee, hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.
 Kufuatia hali hiyo, Pinda ameagiza kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kwamba kazi hiyo ifanyike haraka iwezekanavyo, na kisha ripoti yake iwasilishwe Serikalini kwa hatua zaidi za kimaamuzi.
Waziri Pinda ameyasema hayo muda mfupi uliopita leo, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, kuhusiana na kikao chake cha pamoja na viongozi wa Kikristo na Kiislamu, kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la Mwanza, kwa lengo la kutatua mgogoro wa kidini unaoonekana kuota mizizi.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda, imekuja siku chache baada ya kutokea mapigano makali baina ya wafuasi wa dini ya Kiislamu na Wakiristo kuzuka huko Buseresere-Katoro katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, ambapo mchingaji mmoja aliuawa kwa kuchinjwa huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya.
Aidha, Pinda alikemea vikali vurugu za kidini zilizotokea mkoani Geita, na kuwataka viongozi wa madhehebu yote ya dini kuheshimiana, kujenga mshikamano na kutohasimiana, kwani wao ni watu muhimu sana katika maendeleo na utulivu wa nchi.

Source:http://mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/1224-pinda-alipokuwa-geita-juu-ya-kuchinja-wanyama.html#.USDWlJHcg1Q

Amani Amani Amani Tanzania

Mungu tunaomba amani Tanzania,Mungu tunaomba upendo utawale miongoni mwa watanzania.Mungu iepushe nchi yetu na uvunjivu wa amani,chokochoko za kidini,kisiasa,kikabila na kiitikadi.
Tunaomba haya kwa jina la YESU ....amen

Watatu wanahojiwa Zanzibar: Padre/Father Mushi auawa kwa risasi

UPDATE/TARIFA MPYA (saa nane u nusu mchana) Taarifa ya Polisi:

Watu watatu wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padre Mushi. Tafadhali bofya vipande vya picha zilizopachikwa hapo ili kuvikuza na kusoma taarifa ya Polisi inayoonekana hapo (shukurani kwa Francis Dande).
UPDATE/TAARIFA MPYA (saa saba mchana) Taarifa ya habari Radio One Stereo:
Taarifa ya habari ya Radio One Stereo iliyosomwa saa 7 mchana imeripoti kuwa Padre Mushi aliuawa na watu walipolisimamisha gari la Padre huyo alipokuwa akielekea katika kanisa la Mtakatifu Theresia lililoko eneo la Mtoni, na alipopunguza mwendo ili awasikilize, ndipo alipopigwa risasi kichwani na kusababisha gari alilokuwamo kukosa uelekeo na kuigonga nyumba iliyokuwa jirani. Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua Padre Mushi ili kumwahisha hospitalini katika jitihada za kuokoa uhai wake, lakini alifariki dunia. Waliomwua Padre Mushi bado hawajakamatwa.
                                                                                                      -----------------------

Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Miwili huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.

Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.

Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.

Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.

Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.

Tukio kama hili liliwahi kutokea mwishoni mwa mwaka jana kwa Padre Ambrose kupigwa risasi.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/02/zanzibar-padrefather-mushi-emepigwa-risasi-na-kuuawa.html#ixzz2L9yw5E9H

Breaking News Zanzibar: Padre/Father Mushi emepigwa risasi na kuuawa

Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Mirefu huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.

Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.

Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.

Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.

Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.


Breaking news...Padri pigwa risasi zanzibar na kuuwawa

Padri Mushi, ambaye ni paroko wa parokia ya Minara Miwili - Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana leo mida ya saa moja asubuhi akielekea kanisani kuongoza ibada.

Source: Radio Wapo kipindi cha patapata...

Thursday, February 14, 2013

Tuesday, February 12, 2013

POMBE ILISABABISHA NIKAAMBUKIZWA UKIMWI NAMI NIMEWAAMBUKIZA MAELFU

{Ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la baba yangu maana sitaki liwe kwenye blog watu watanijua na kuniangamiza maana nimeshawaangamiza wengi sana kwa ukimwi ila mengine yote usifute hata moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi nilionao}.        
Drunk Girls                                                                                                                                                 Nilizaliwa mkoa wa dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa mwenge. nilipata marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja alinitongoza kwa muda mrefu sana na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu kutongoza ili mschana unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu ngono na wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana basi huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.Nilimkubalia tukawa wapenzi ila nilikataa kuhusu kufanya mapenzi maana anayekupenda kiukweli sio uongo lazima asitake ngono kabla ya ndoa. kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia kuhusu kufanya mapenzi nilikataa alitumia mbinu nyingi sana kwa kunibembeleza na hata kulia mbele yangu ili tufanye tu mara moja ila nilikataa, alisema atavumilia hadi siku ya ndoa yetu ambapo tulipanga kuoana mwaka sept 2009. Siku moja aliniambia twende kwenye kumbi za starehe na mimi kwa sababu ya upagani na kumwamini pia kwa sababu nampenda nilikubali tulienda huko na kulikua na bendi fulani maarufu ya mziki wa dansi ilikua inatumbuiza. Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi wangu akaagiza pombe alianza kunywa huku akinionjesha, nilikataa kwa sababu nilikua sijawahi kunywa pombe katika maisha yangu yote, hata sijui alinishawishi vipi nilijikuta nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa 5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4 japokua nilikua nakunywa kidogo kidogo tu tena kwa kunywesha na mpenzi wangu maana nikama nikua nanyweshwa kila baada kama ya dakika 25 ndipo nakunywa mara moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila niliihisi tu naonja ili kumlizisha mpenzi wangu.ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi usingizi na pia nilijiona wa tofauti najua nililewa hata kama sikujua kama nimelewa maana nakumbuka tulitoka pale huku amenishika mkono huyo mpenzi wang. Tulikodo tax na kuondoka na siku hiyo aliniambia twende kwake alikokua amepanga chumba maana tulikua na usingizi sana nilikubali huku nikidhani hatuwezi kufanya mapenzi, tulifika salama na kuingia ndani ukweli pombe ni kichocheo cha ngono na ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania ningefunga bar zote, nilijikuta natamani kufanya mapenzi na huyu mpenzi wangu hata alikua hana nia maana alijua atanichukiza sana na uhusiano ungekufa siku hiyo lakini kwa sababu ya pombe nilimwambia siku hiyo tufanye kidogo maana mwili wangu unataka ni kweli siku hiyo kwa sababu ya pombe nilifanya mapenzi na huyo mpenzi wangu na baadae akanipeleka nyumbani baada ya wiki mbili maana tulikaa wiki mbili bila kuonana alikuja na kunieleza habari ambayo sikuihitaji katika maisha yangu maana nilikua nasikia tu kwa watu wengine lakini sio kwangu alisema ''JANE ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA SASA'' nilidhani utani lakini aliniambia kuwa yeye ana ukimwi tangu mika mitano iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi kuacha.nililia sana na baada ya wiki moja baadae nikaenda kupima na kukutwa nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na chanzo cha yote ni pombe, kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua wanadamu wengi.Nilikua na ukimwi na kwa hasira maana mpenzi wangu alihamia arusha huku akisema neno moja la mwisho kwamba ''shetani amemtuma kuwaambukiza wanadamu ukimwi''.Sikujua sikujua sikujua sikujuaaaaaaaaa basi tu ooh YESU nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa mzigo ambao haukunistahili mimi, hata leo hua najiuliza kwamba nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini pombe na huyu wakala wa shetani wamenifanyia hivi.Baada ya kujua nina ukimwi na hali hiyo nikaikubali na kulikua na kundi kubwa sana la wanaume ambao walikua wamewahi kunitongoja na niliwakataa sana kwa sababu hii nilikubali ili nami nife na wengi, nilianza kumkubali kila mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini wakati huu nilmkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga na akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua kuwa namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao wana ukimwi uliotoka kwangu. kiukweli tangu may 2009 hadi 2012 nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana ilifika kipindi nala na wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa ukimwi wanadamu zaidi ya 10,000 na hili tangazo la ''TUKO WANGAPI'' huwa linaniliza kila siku maana hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi kubwa sana ya watu.Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku naombewa nilikutwa na mapepo mengi sana na hata waombeaji wakashangaa. ningejua ningeokoka tangu nikiwa na miaka 5 ili lakini ndio hivyo sina jinsi wala uwezo wa kubadirisha hali hiyo.Na naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi.hadi sasa mtu yeyote hawezi kujua kama nina ukimwi na sikui MUNGU ana mpango gani na mimi maana kwake yote yanawezekana nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia ARV hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe kujua kama uovu huu nimefanya mimi.Ndugu zangu kama una ukimwi nenda kanisani ukaombewe na kama una akili mpe YESU maisha yako maana pia baada ya kifo ni hukumu yasalimishe maisha yako kwa YESU na usiambukize wengine tena. Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi tena na sitafanya hivyo wala sitaolewa  na mtu yeyote maana yatosha kwa uovu niliofanya na hadi sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki na nilihudhulia misibani huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.Mwisho nawashauli wababa kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni na waume zenu,  vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa au kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye ukimwi ni wengi kuliko unavyozani.fuata unachofundishwa kanisani na pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.MUNGU akubariki 

Source:http://maishaushindi.blogspot.com

Are there dinosaurs in the Bible?

What does the Bible say about dinosaurs? " Diplodocus Family
The topic of dinosaurs in the Bible is part of a larger ongoing debate within the Christian community over the age of the earth, the proper interpretation of Genesis, and how to interpret the physical evidences we find all around us. Those who believe in an older age for the earth tend to agree that the Bible does not mention dinosaurs, because, according to their paradigm, dinosaurs died out millions of years before the first man ever walked the earth. The men who wrote the Bible could not have seen living dinosaurs.

Those who believe in a younger age for the earth tend to agree that the Bible does mention dinosaurs, though it never actually uses the word “dinosaur.” Instead, it uses the Hebrew word tanniyn, which is translated a few different ways in our English Bibles. Sometimes it’s “sea monster,” and sometimes it’s “serpent.” It is most commonly translated “dragon.” The tanniyn appear to have been some sort of giant reptile. These creatures are mentioned nearly thirty times in the Old Testament and were found both on land and in the water.

In addition to mentioning these giant reptiles, the Bible describes a couple of creatures in such a way that some scholars believe the writers may have been describing dinosaurs. The behemoth is said to be the mightiest of all God’s creatures, a giant whose tail is likened to a cedar tree (Job 40:15). Some scholars have tried to identify the behemoth as either an elephant or a hippopotamus. Others point out that elephants and hippopotamuses have very thin tails, nothing comparable to a cedar tree. Dinosaurs like the brachiosaurus and the diplodocus, on the other hand, had huge tails which could easily be compared to a cedar tree.

Nearly every ancient civilization has some sort of art depicting giant reptilian creatures. Petroglyphs, artifacts, and even little clay figurines found in North America resemble modern depictions of dinosaurs. Rock carvings in South America depict men riding diplodocus-like creatures and, amazingly, bear the familiar images of triceratops-like, pterodactyl-like, and tyrannosaurus rex-like creatures. Roman mosaics, Mayan pottery, and Babylonian city walls all testify to man’s trans-cultural, geographically unbounded fascination with these creatures. Sober accounts like those of Marco Polo’s Il Milione mingle with fantastic tales of treasure-hoarding beasts. In addition to the substantial amount of anthropic and historical evidences for the coexistence of dinosaurs and man, there are physical evidences, like the fossilized footprints of humans and dinosaurs found together at places in North America and West-Central Asia.

So, are there dinosaurs in the Bible? The matter is far from settled. It depends on how you interpret the available evidences and how you view the world around you. If the Bible is interpreted literally, a young earth interpretation will result, and the idea that dinosaurs and man coexisted can be accepted. If dinosaurs and human beings coexisted, what happened to the dinosaurs? While the Bible does not discuss the issue, dinosaurs likely died out sometime after the flood due to a combination of dramatic environmental shifts and the fact that they were relentlessly hunted to extinction by man.

UGOMVI WA NANI ANA HAKI YA KUCHIJNA KITOWEO HUKO GEITA


VITA YA WAISLAM NA WAKRISTO GEITA YAFIKIA PABAYA, MCHUNGAJI ACHINJWA HADI KUUAWA

TAHADHARI PICHA ZIFUATAZO ZINATISHA.

Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Yasin Rajabu na hapa akiwa amelazwa katika wod namba 8 Hospitali ya wilaya ya Geita kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Mwili  wa marehemu mchungaji Mathayo Kachila ukiwa jokofu la mochwari kwenye hospitali ya wilaya ya geita.


Hivi ndivyo anavyoonekana Majeruhi Said Ntahompagaze aliyejeruiwa mguu wakati wa vurugu za waislam na wakristo zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.

Hivi ndivyo unavyoonekana mguu wa Said Ntahompagaze aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristo  zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.


Majeruhi Vicent Damon akiwa amelazwa wod na 8 hospitali ya wilaya ya Geita aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristo zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama.


Majeruh Sadick Yahaya.


Majeruhi Ramadan aliyejeruiwa wakati wa vurugu za waislam na wakristu zilizotokea leo katika kijiji cha Buseresere wilayani Chato mkoani Geita na kusababisha fukuto kubwa la vurugu zilizosababisha shughuli mbalimbali kusimama.

Machafuko makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristo na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini  wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.

Habari za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.

Imeelezwa kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu.

Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristo kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga.

Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE, YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.

Kutokana na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya wakristo na waislam ambapo mbali na wakristo kutumia mawe waislamu wao walitumia mapanga na majambia.

Hata hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.

Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45), Sadick Yahaya(40), Yasin Rajab(56), Vicent Damon(22), wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya wilaya ya Geita.

Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.

Jeshi la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya kidini.

Source:http://gsengo.blogspot.com/  

Monday, February 11, 2013

UKWELI KUHUSU UZUSHI WA “DA VINCI CODE”

Baada ya kukisoma kwa makini kitabu hiki kilichoandikwa na mwandishi na mtaalmu wa elimu ya dini Dan Brown,aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa kueneza uzushi mkubwa duniani kuhusu imani ya kikristo na YESU KRISTO mwenyewe,nimeonelea ni vyema nikauanika uongo huu hadharani ili kila mmoja wetu apate kuutambua uzushi huu.
Uwongo huu unaojizolea umaarufu siku hadi siku sio kitu cha kupuuzwa hata kidogo na ni lazima sisi kama kanisa tusimame na kuupinga kwa kweli zilizopo (facts) bila kuuonea aibu wala kuugopa maadam ukweli upo wazi.Kitabu cha mwandishi Dan Brown kimeuza zaidi ya nakala milioni 40 duniani kote tangu kitoke kwa mara ya kwanza mwaka 2003.Pia f
ilamu iliyotengenezwa huko Hollywood Marekani kutokana na kitabu hicho imeshaonyeshwa karibu duniani kote ikiwemo hapa kwetu Tanzania ambapo hata nakala zake zimeshaanza kusambaa.Unaweza kushangaa kwa nini uwongo huu umepata umaarufu mkubwa kiasi hicho,hii inawezekana kwa sababu wapinzani wa ukristo wapo wengi na ile roho ya mpinga kristo ipo na inafanya kazi,2Wathesolanike 2:1-10;
Nafahamu zipo njia nyingi za kupingana na uwongo huu,ikiwemo njia ya maombi,kuwafundisha wakristo Neno la Mungu kwa usahii na hata kupuuzia huu uwongo ili upotee wenyewe.Lakini hatuwezi kukataa ukweli kuwa lipo kundi la watu ambalo hata mtume Paulo analiita “wenye masikio ya utafiti” ambalo litaendea kuzitafuta filamu hizi na vitabu hivi ili kutaka kujua kilichomo ndani. Nchi nyingi za magharibi watu wengi wamachukuliwa na uwongo huu na hata wengine wametokea kuuamini bila kujua ukweli halisi wa uzushi huu.Mfano msomaji mmoja wa kitabu hiki alikaliliwa akisema kuwa “kuanzia sasa sitaenda tena kanisani ..Sikujua kama ukristo ni hadithi za kutunga….”.
Sasa matokeo kama haya si mambo ya kupu
uzia hata kidogo,kwani history ya kanisa inaonyesha kuwa imani potofu mbalimbali zilizowahi kuibuka duniani zilianza na mawazo ya vikundi vidogo au mtu mmoja na zilipata nguvu kadri siku zilivyoendelea.Na ndio matokeo ya imani nyingi za uwongo tunazoziona leo hapa duniani na waumini wa imani hizo wapo tayari kuzitetea kwa hali na mali kwa kuwa hawakufahamu msingi halisi wa imani zao.Hii imesababisha hata kupishana kwa mafundisho baina ya madhehebu mbalimbali ya kikristo.Yapo madhehebu ya kikristo yasiyoamini kuhusu ROHO mtakatifu,Uungu wa YESU na mambo kadhaa.Kwa hiyo kanisa haliwezi kupuuzia hata kidogo uwongo huu.
Labda kwanza tungeanza kujiuliza hoja alizoanzisha mwandishi Dan Brown kama zinaukweli wowote,

  • Je, YESU alikuwa na ndoa ya siri na Mariam Magdalena?
  • Ni kweli Uungu wa YESU ulianzishwa na kutungwa na mtawala wa kirumi Constantino na Kanisa?
  • Ni kweli Constantino alitumia umaarufu na ushawishi wa YESU kutunga Uungu wa YESU?
  • Je vitabu vya agano la kale tunavyotumia siku za leo vilichaguliwa na Constantino?
  • Je kumbukumbu za kwanza kuhusu maisha ya YESU ziliteketezwa ili kuuficha ukweli?
  • Je, maandiko ya kale yaliyogunduliwa hivi karibu pamoja na injili za wagnostika (Gnostic gospel) yanatueleza ukweli kuhusu YESU?
Hayo ni madai makuu ya msingi yaliyomo kwenye kitabu cha Da Vinci Code.
Labda tungeanza na kuelewa kwanza nini maana ya neon “Da Vinci Code”.Hili ni jina la mwanahistoria,mwanasayansi,mwanafilosofia na mchoraji mashuhuri aliyekuwa akiitwa Leornando Da Vinci(1452 – 1519 A.D).Dan Brwon anadai kuwa huyu jamaa alikuwa ni mwanachama wa kikundi cha siri kilichokuwa kikidai kujua mambo ya siri ya wakati huo kilichojulikana kwa jina la “Priory of Sion”.Leornado Da Vinci ndio msingi mkubwa wa mwandis
  • hi Dan Brown kuhusu madai yake kuwa YESU KRISTO alikuwa na ndoa ya siri na Mariam Magdalena.Hii inatokana na mchoro aliochora Leornado Da Vinci ukielezea kalamu ya mwisho ya YESU na wanafunzi wake.Katika mchoro huu unaoitwa Da Vinci Code,inadaiwa kuwa Leornado amemchora Mariam Magdalena akiwa pembeni mwa YESU.Japo baadaye wakristo wengi waliamini huyo ni Yohana mwanafunzi wa YESU yule ambaye YESU alimpenda sana.Da Vinci hakuwa na lengo la kumchora Yohana kama kanisa lilivyokuwa likiamini bali alimchoro Mariam Magdalena, na ndiyo maana inaitwa “Da Vinci Code” yaani siri ya Da Vinci. Da Vinci anadai kwamba kwa kuwa YESU alikuwa na ndoa ya siri na Mariam Magdalena ndio sababu Mariam Magdalena ilibidi awepo kwenye kalamu hiyo ya mwisho.Angalia mchoro hapo chini.












Kutoka kulia kwenda kushoto ni Bartholomeo, Yakobo mdogo, Andrea, Yuda, Petro, Yohana(au Mariam Magdalena kulingana na Da Vinci Code), YESU KRISTO, Thomaso, Filipo, Mathayo, Thadeo na Simon.



Kwa hiyo Brown anaelezea uwongo wake kwenyer kitabu chake hicho kwa kumtumia profesa wa uingereza wa mambo ya kale yanayohusu elimu ya dini anayeitwa Sir Leigh Teabing.
Teabing anadai kwamba katika baraza la maaskofu zaidi ya 300 lililokutana Nikea mwaka 325 A.D, ”mambo mengi yanayohusu ukristo yalipigiwa kura na kutolewa maamuzi baada ya kujadiliana na kubishana kwa kirefu” likiwemo la Uungu wa YESU.
Teabing anasema kuwa kabla ya baraza la Nikea mwaka 325 A.D,YESU alikuwa anatambulika na wanafuasi wake kama mmojawapo wa manabii waliowahi kuwepo,na kwamba ni mwanadamu aliyekuwa na uwezo wa ajabu tu ila siyo Mungu kama inavyodaiwa.Kwa hiyo Teabing anadai kwamba YESU alifanywa kuwa mwana wa Mungu na pia alifanywa kuwa Mungu rasmi na baraza hilo la Nikea kwa kupigia kura uamuzi huo chini ya Mtawala wa Rumi wa wakati huo aliyejulikana kama Constantino.Tena anadai kuwa baada ya makubaliano hayo ya Maaskofu hao wapatao 300 ndipo nyaraka zote za muhimu zilizomuhusu YESU ziliteketezwa na kupotezwa kabisa.Kwa maneno yake Teabing anadai kuwa msingi mzima wa ukristo umejengwa juu ya uwongo.
Da Vinci Code haiwezi kujisimamia yenyewe bila kutumia matukio jalisi ya kilichofanywa katika baraza la Nikea, watu waliowahi kuishi kama Constantino na Arius na nyaraka zilizowahi kuandikwa kama injili za wagnostika.
Kwa hiyo kama tunataka kutengenisha kweli na uzushi huu, kazi yetu kubwa itakuwa ni kubainisha ukweli halisi wa hayo mambo ambayo bwana Dan Brown anayategemea kusambaza uongo wake.
UKRISTO NA CONSTANTINO
Kabla ya Constantino kuanza kutawala Rumi,wakristo walikuwa wakiteswa sana.Lakini baada ya Constantino kuwa mkristo(kuokoka) kwenye miaka ya 300 AD,akaigeuza Rumi na kuwa utawala wa kwanza wa kikristo na hivyo kanisa na serikali vikaunganishwa na kuwa kitu kimoja.Kutokana na hilo mateso kwa wakristo katika utawala wa Rumi hayakuwepo tena wakati wote wa utawala wa Constantino.
Kwa hiyo Constantino akaazimia kuunganisha utawala wake wa mashariki na magharibi ambao ulikuwa umegawanyika vibaya kutokana na kuibuka kwa imani mbalimbali za uongo,madhehebu mbalimbali,migawanyiko iliyotokana na tofauti za kiimani na mengineyo mengi ambayo yalitokana na mabishano kuhusu uhalisia wa YESU.
JE, KWELI CONSTANTINO NDIYE ALIYEANZISHA UUNGU WA YESU?
Kuweza kujibu madai ya Dan Brown ni lazima kwanza tujue ni kipi wakristo walikuwa wanaamini kabla ya Constantino na baraza la Nikea hawajakaa mwaka 325 A.D.
Wakristo walikuwa wakimwabudu YESU kama MUNGU tangu karne ya kwanza.Lakini katika karne ya nne,Kiongozi wa kanisa lililopo upande wa mashariki wa utawala wa Constantino aliyekuwa akiitwa Arius alianzisha kampeni akidai kuwa YESU aliumbwa kipekee zaidi ya malaika lakini hakuwa Mungu.Athanasius na viongozi wengine wengi wa kanisa kwa upande wao waliamini kuwa YESU alikuwa ni MUNGU katika mwili.
Kwa hiyo Constantino akataka kuumaliza mgongano huo ili alete amani katika utawala wake wa mashariki na magharibi.Kwa hiyo mwaka 325 A.D akawaalika zaidi ya maaskofu 300 kutoka kila sehemu ya ulimwengu wa kikristo wa wakati huo kwenda Nikea (ambayo kwa hivi sasa ni sehemu za Uturuki)
Swala kubwa hapa ni, Je kanisa la kwanza lilimchukulia YESU kama muumbaji au ni kiumbe tu – mwana wa Mungu au mwana wa fundi seremala? Je mitume walifundisha nini kuhusu YESU?Kutoka katika maelezo yao ya awali kabisa kwenye nyaraka zao walimwona YESU kama Mungu.Baada ya miaka 30 tangu kufa na kufufuka kwa YESU,Paulo mtume anawaandikia wafilipi kuwa YESU ni MUNGU katika mwili (Wafilipi 2:6-7).
Pia Yohana,mwanafunzi aliyekuwa karibu zaidi na YESU na kuishi naye kwa zaidi ya miaka 3 anathibitisha Uungu wa YESU katika maneno haya (Yohana 1:1-4,14) ”Hapo mwanzo alikuwepo Neno,naye Neno alikuwepo kwa Mungu,naye Neno alikuwa Mungu,………………………………………….naye Neno akafanyika mwili na kukaa kwetu.Nasi tukauona utukufu wake……………….”
Aya hii kutoka injili ya Yohana iligundulika kwa kutumia kipimo cha carbon-14 kuwa iliandikwa kwenye mwaka 175 A.D.
Kwa hiyo YESU alikuwa akitajwa kama Mungu zaidi ya miaka 100 kabla ya Constantino hajaitisha baraza la Nikea.Kwa hiyo tunaona kuwa madai ya uzushi ya Da Vinci Code kuwa Uungu wa YESU ni matokea ya mkutano wa Nikea karne ya 4 ni uongo mtupu.
Kwenye kitabu chake Dan Brown anadai kupitia Teabing kwamba maaskofu wengi kule Nikea walikubaliana na mafundisho ya Arius kuwa YESU ni nabii wa kawaida tu na kuwa eti mafundisho ya sasa kuhusu Uungu wa YESU yalikubaliwa kwa kura chache sana.
Ukweli ni kwamba ,kati ya kura 318 za maaskofu wote waliopiga kura ni wawili tu ndio waliokubaliana na mafundiho ya Arius ,lakini wengine wote waliamua kubaki na mafundisho ya mitume wa kwanza walioishi na YESU KRISTO kuwa YESU ni Mungu na ni zaidi ya nabii wa kawaida.
Baraza likaamua na kukubali kuwa YESU na Mungu Baba ni wamoja,Pia Mungu Baba,Mwana na Roho Mtakatifu ni utatu mtakatifu,(coexistent,coeternal Persons but one God).Mafundisho haya ya utatu mtakatifu ndiyo msingi mkuu wa imani ya kikristo.Japokuwa Arius alikuwa ni mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa,lakini baada ya majadiliano marefu na kutafuta ukweli na ushahidi wa kutosha baraza la Nikea likamtangaza rasmi Arius kuwa ni mzushi dhidi ya imani ya kikristo (heretic) kwa sababu mafundisho yake yanapingana na yale waliofundisha mitume kuhusu Uungu wa YESU
Historia inaonyesha bila mashaka yoyote kuwa YESU akikubali waziwazi kabisa kuabudiwa na wanafunzi wake.Paulo na wanafunzi wengine wanafundisha kwa uwazi kabisa kuwa YESU ni Mungu na anastahili kuabudiwa.Na hawa mitume walifundisha hivi na hata kumwabudu YESU tangu karne ya kwanza.Sasa iweje tena Teabing adai kuwa Constantino ndiyo aliyeanzisha Uungu wa YESU wakati kanisa lilikuwa likimwabudu YESU kama Mungu miaka zaidi ya 200 kabla ya Constantino.Huu ni uwongo wa wazi kabisa na wala hauhitaji mtu kuwa na PhD kuugundua.
JE, NI KWELI HISTORIA YA KWANZA YA YESU ILIHARIBIWA NA CONSTANTINO?
Da Vinci Code inadai kwamba Constantino aliharibu ushahidi wa historia ya kwanza kabisa ya YESU na kuamuru iandikwe upya kwa kutumia injili tulizonazo hivi sasa kwenye agano jipya na kuziharibu injili nyingine zaidi ya 80.
Hapa kuna mambo mawili ya kumjibu Dan Brown.Kwanza ni kujua iwapo kuna ukweli wowote katika madai kwamba Constantino alibadilisha na kulazimisha uchaguzi wa vitabu vya Agano Jipya.Pili ni kujua iwapo aliteketeza nyaraka za awali ambazo zingetumika kuandika Biblia.
Tukianza kujibu hoja ya kwanza, maandiko na nyaraka mbalimbali zilizoandikwa na viongozi wa kanisa karne ya pili na wazushi na wapinzani mbalimbali zinathibitisha matumizi makubwa ya vitabu tunavyotumia leo hii vya agano jipya.
Karibu miaka 200 kabla ya Constantino hajaitisha baraza la Nikea, mpinzani na mzushi Marcion alivikubali vitabu 11 kati ya 27 vya Agano Jipya kama maandiko ya mitume wa kwanza.
Na kwa wakati huohuo mzushi mwingine na mpinzani Valentinus alitumia sehemu kubwa ya maandiko yaliyopo katina Agano Jipya.Kwa hiyo tunaona kuwa hawa wazushi wakubwa wawili waliokuwa ni wapinzani wakubwa wa viongozi wa kanisa la kwanza walitumia maandiko hayahaya tunayotumia leo hii kwenye Agano Jipya, haingekuwa rahisi kwao kuandika yale ambayo maaskofu wa Nikea waliyataka, Hii inaonyesha wazi kuwa kanisa la kwanza walitumia sana vitabu vya agano jipya tunavyotumia leo kabla ya Constantino.
Hivyo basi hakuna ukweli wowote kuwa Constantino alishinikiza na kuanzisha matumizi ya vitabu hivi vya Agano Jipya wakati ambapo vilishakuwa vinatumiwa na mamilioni ya waamini kama maneno ya Mungu karibu miaka 200 kabla yake.
Na kujibu hoja ya pili kuwa nyaraka hizi za kale za injili ya wagnostika ziliteketezwa na kutoweshwa zisiwemo kwenye agano jipya ili kupotosha ushahidi.Teabing anadai kwamba injili za wagnostika ziliondolewa kutoka kwenye Biblia 50 za mwanzo ambazo Constantino aliagiza ziandikwe.
Injili hizi za wagnostika zinatokana na kikundi cha watu wanaojulikana kama wagnostika, Jina hili linatokana na neon la kiyunani (kigiriki) gnosis, likiwa na maana ya “maarifa”.Watu hawa walikuwa wakifikiri kuwa wao wanafahamu mambo fulani fulani ya siri ambayo watu wengine hawakuwa wakiyajua.
Kadri ukristo ulivyokuwa ukienea sehemu mbalimbali, wagnostika waliyachanganya mafundisho yao na baadhi ya mafundisho ya ukristo na wakaanzisha imani iliyokuwa na mchanganyijko wa kignostika na ukristo.
Katika historia ya ukristo iliyoandikwa na Oxford, John Manners anaandika jinsi wagnostika walivyochanganya ukristo na hadithi zao za kale, dini za miungu yao ya asili na mizimu na mambo yao ya kiuaguzi.
Tofauti na Brown anavyodai,si kweli Constantino ndiye aliyesababisha kuichukulia imani ya wagnostika kama imani potofu bali ni mitume wenyewe wa kanisa la kwanza ndio waliosema kwa uwazi kabisa kuwa imani ya wagnostika ni potofu.
Mfano Mtume Yohana alivyoandika kati ya mwaka 95-99A.D. Katika 1Yohana 2:22Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Masiha. Mtu wa namna hiyo ni adui wa Kristo--anamkana Baba na Mwana.”
Kwa kufuata mafundisho ya mitume,viongozi wa kanisa la kwanza walitangaza waziwazi kuwa ugnostika ni imani potofu.Mmoja kati ya mababa wa kanisa, Irenaeus,aliandika miaka 140 kabla ya baraza la Nikea kuwa ugnostika ulichukuliwa na kanisa kama imani potofu.Pia alizikataa “injili” zao na akiunga mkono injili nne zilizopo kwenye agano jipya alisema “haiwezekani vitabu vya injili vilivyopo vipunguzwe au viongezwe
Mwanatheolojia mmoja aliyejulikana kama Origen aliandika hivi katika karne ya 3 ,zaidi ya miaka 100 kabla ya Nikea.
Najua kuna injili fulani inayoitwa ,”Injili ya Thomaso”,and “Injili ya Mathias”, na nyinginezo nyingi—Hebu na mtu asituone sisi ni wajinga kwa sababu ya hao wanaojifikiria wao wenyewe kuwa wanaoufahamu fulani[gnostics].Hata hivyo zaidi ya yote haya,sisi tumeshathibitisha bila mashaka yoyote ni injili zipi kanisa linazitambua,ni zile injili nne tu ndizo zinazokubalika
Kwa hiyo hapa tunaona kauli na mapendekezo ya viongozi wa mwanzo wa kanisa waliokuwa wakiheshimika sana kwa wakati huo.Wagnostika hawakutambuliwa kama wakristo na walijulikana kama imani potofu kabla ya hata baraza la Nikea
KUHUSU WAANDISHI WA INJILI ZA WAGNOSTIKA.
Swali la kujiuliza hapa ni,Je, kwa nini basi injili zote hizi za wagnostika zinadaiwa kuandikwa na wahusika waliopo kwenye agano jipya la Biblia tunayoitumia leo hii? Mfano,Injili ya Filipo,Injili ya Petro,Injili ya Mariam(Magdalena),Injili ya Yuda, na kadhalika.Je ni kweli ziliandikwa na wahusika wenyewe kama inavyodaiwa na wagnostika?
Injili hizi zote za wagnostika zimeandikwa kati ya mwaka 110 hadi 300 A.D.Na hakuna hata mwanazuoni yeyote anayeamini kuwa zimeandikwa na wahusika wenye majina ya hizo injili kwa kuwa hazina ushahidi wa kutosha.
Moja kati ya maelezo yanayopatikana katika maktaba ya Nag Hammadi huko Misri(sehemu ambayo injili ya wagnostika ya filipo iligundulika mwaka 1945) yanaeleza kwamba “injili za wagnostika ziliandikwa na waandishi wasiojulikana na wahusika wanaodaiwa kuandika injili hizo siyo wale waliopo kwenye agano jipya [tunalotumia leo]
Mmoja kati ya wanazuoni wa agano jipya Norman Geisler akizielezea injili mbili za wagnostika,injili ya Petro na matendo ya Yohana(hizi siyo vitabu vya agano jipya tunavyovifahamu) anasema,”maandiko ya wagnostika hayakuandikwa na mitume ila na watu wengine katika karne ya 2 na kuendelea,wakijifanya kupewa ruhusa na mitume ili wafikishe mafundisho yao kwa wakristo.Katika siku za leo tunauita huu ni udanganyifu na utapeli
JE, KWELI YESU ALIKUWA NA NDOA YA SIRI NA MARIAM MAGDALENA?
Hoja hii ndiyo ambayo imeonekana kuleta utata zaidi ulimwenguni na hata kusababisha kitabu hicho cha uzushi cha Dan Brown kuuzwa na kununuliwa sana.
Da Vinci Code inadai kuwa YESU na Mariam Magdalena walikuwa na ndoa ya siri iliyosabisha kuwa na uzao.Dan Brown anadai kwamba kikundi cha siri cha kikatoliki kinachojulikana kama “Priory of Sion” ndicho kinachotunza siri kuwa tumbo la Mariam Magdalena lilobeba uzao wa YESU ndio linaloitwa kikombe kitakatifu “Holy Grail”. Brown anadai kuwa baadhi ya wanachama wa kikundi hiki cha Priory of Sion ni pamoja na Sir Isaac Newton, Botticelli, Victor Hugo na mzushi maarufu Leornado Da Vinci.
Je madai haya ni ya kweli? Hebu tuangalie wanazuoni wengine wanasemaje kuhusu uzushi huu.
Katika makala moja iliyotochapishwa na gazeti la Newsweek inamnukuu mwanazuoni mmoja akisema kuwa “Madai kwamba YESU na Mariam Magdalena walioana kwa siri hayana ushahidi wowote wa kihistoria,Hoja zinazotolewa na Da Vinci Code zinasimamia kwenye mstari mmoja wa injili ya wagnostika ya Filipo inayoonyesha kuwa Mariam Magdalena alikuwa na ukaribu na YESU”
Pia kuna mstari mmoja tu katika Injili hiyo ya wagnostika ya Filipo kuwa YESU alimbusu Mariam Magdalena.Lakini kumsamia mtu kwa kumbusu kilikuwa ni kitu cha kawaida katika karne ya kwanza katika eneo hilo la mashariki ya kati,na hilo siyo jambo la ajabu”.
Siyo hivyo tu ila tunaona kwamba injili ya Filipo ya Wagnostika ni ulaghai ulioandikwa kati ya mwaka 150-220 A.D na mwandishi asiyejulikana.Kwa hiyo madai yote yaliyomo humo hatuwezi kuyaamini hata kidogo.
Pia kuhusu kikombe kitakatifu (Holy Grail) na pamoja na Priory of Sion,Brown hana ushahidi wowote kuhusu hilo kwa sababu kikombe kitakatifu ni kile kikombe alichotumia YESU wakati wa kalamu ya mwisho na wala hakina uhusiano wowote na Mariam Magdalena.
Kuhusu Priory of Sion ni uongo wa wazi kabisa ambao Dan Brown anauzusha bila kuona aibu hata chembe.Leornado Da Vinci hajawahi kuwa mwanachama wa kundi hilo kwa sababu kundi hilo liliundwa rasmi mwaka 1956, miaka 437 baada ya kifo chake. Leornado Da Vinci aliishi kati ya mwaka 1452 hadi mwaka 1519.
JE NI KWELI KUNA NYARAKA ZA SIRI ZILIZOFICHWA?
Teabing anadai kwamba kuna maelfu ya nyaraka za siri zinazothibitisha kwamba ukristo ni hadithi za uongo za kutunga na kufikirika.Je, madai haya ni kweli?
Kama kungekuwa na nyaraka hizo kama anavyodai Teabing,basi wanazuoni wapinzani wa ukristo wangekuwa tayari wameshazisambaza tangu kipindi hicho.Nyaraka za uzushi zilizokataliwa na kanisa la kwanza wala siyo siri tena na zimekuwa wazi kwa karne nyingi sasa.Wala hakuna la ajabu hapo,kwani hazikuhusishwa kama sehemu ya maandiko yaliyokubaliwa na mitume.
JE, LERONADO DA VINCI ALIKUWA SHOGA?
Baadhi ya wanazuoni wanaamini kwamba Leornado Da Vinci alikuwa shoga au alipenda kujihusisha na mambo ya kishoga.Wanatoa madai haya kutokana na ukweli kwamba Leornado Da Vinci hakuwahi kuwa na mke.Lakini hili sio jambo hasa la kumfanya mtu kudhaniwa kuwa ni shoga ila tatizo hapa ni ile tabia yake ya kupenda kuchora picha za vijana wa kiume wazuri wakiwa uchi wa mnyama. Mara nyingine alichora vijana hao wazuri wakiume wakionekana kuingiliana kimwili wao kwa wao.Pia mwaka 1476,Leornado Da Vinci alifikishwa mahakani kwa mashtaka ya vitendo vya kishoga.Japokuwa alifungwa kwa miezi miwili lakini mashtaka hayo yalifutwa kwa kukosekana ushahidi wa kutosha.
UKWELI UPO WAZI KABISA.
Tumeona kwa uwazi kabisa ukweli usiopingika kuhusu maisha matakatifu ya YESU KRISTO mwana wa MUNGU na ni MUNGU halisi kama Biblia takatifu inavyosema katika Injili ya Yohana 1:1-4; 14
Tofauti kabisa na injili za wagnostika, ambazo waandishi wake hawajulikani (hazijulikani ziliandikwa na nani), Agano Jipya tunalotumia leo hii limepitia majaribio mengi likithibitishwa kwa karne nyingi sasa.
Mwanazuoni mmoja aliwahi kusema kwamba, kama unataka kusoma uzushi na hadithi za uongo kuhusu YESY KRISTO wa Nazareth, basi kitabu cha Da Vinci Code chaweza kuwa chaguo lako zuri, lakini kama unataka kuujua ukweli wa maisha ya YESU kutoka kwa watu waliomwona kwa macho na kuishi naye basi Injili kama ilivyoandikwa na Mtakatifu Mathayo, Mtakatifu Marko, Mtakatifu Luka na Mtakatifu Yohana ndiyo chaguo lako bora kabisa la wakati wote la kujua njia sahihi kabisa ya kuweza kumwona Mungu.