WAKATI Watanzania wakiendelea
kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi,
wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa
mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la kipentekoste la Shaloom lililoko
eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa
Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, alisema jana kuwa tukio
hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku.
Amesema moto huo ulizuka
mara baada ya kikundi cha watu watatu kuonekana wakipita njia karibu na
kanisa hilo na baada ya muda mlinzi wa kanisa hilo alisikia kanisa
likishambuliwa kwa mawe juu ya maapaa.
Picha na maktaba
Amesema baada ya mlinzi huyo
kubaini kuwepo kwa hatari, alilazimika kukimbia kwenda kujificha lakini
huku akiangalia kwa mbali kinachoendelea.
Kamanda Olomi amesema kuwa wakati
mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni huku akiangalia kinachotokea,
mara aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa na ndipo alipopiga simu kwa
kiongozi wa kanisa hilo naye kuwajulisha Polisi.
Amesema Polisi walipofika hapo
walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo lakini wakati huo tayari
ulishateketeza thamani za kanisa hilo na vitu vingine vilivyokuwa
kanisani hapo.
Kamanda Olomi amesema moto huo ungeweza kusababisha athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema.
Hata hivyo amesema uimara wa dali
lililotengenezwa kwa Gibsam kumesaidia kuunusuru moto huo kuunguza mapaa
na kuliteketeza kabisa kanisa hilo.
Amesema wakati uongozi wa kanisa
hilo ukifanya tathimini ya harasa iliyopatikana kutokana na moto huo,
Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka washukiwa kwa kutafuta taarifa kwa
raia wema na bado hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusika na tukio
hilo.
Hata hivyo Kamanda Olomi amesema
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na
Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia
matishio mengine kama hayo.
Source:http://www.fullshangweblog.com/2013/02/19/kanisa-lachomwa-moto-zanzibar/
No comments:
Post a Comment