{Ni Jane naishi mwenge Dar es salaam
naomba utalifuta jina la baba yangu maana sitaki liwe kwenye blog watu
watanijua na kuniangamiza maana nimeshawaangamiza wengi sana kwa ukimwi
ila mengine yote usifute hata moja ili dunia ijue tu japokua mimi
nitakufa kwa huu ukimwi nilionao}.
Nilizaliwa mkoa wa dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na
hata sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya
kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa
mwenge. nilipata marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja alinitongoza kwa
muda mrefu sana na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu kutongoza
ili mschana unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu ngono
na wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana basi
huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.Nilimkubalia tukawa wapenzi ila
nilikataa kuhusu kufanya mapenzi maana anayekupenda kiukweli sio uongo
lazima asitake ngono kabla ya ndoa. kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia
kuhusu kufanya mapenzi nilikataa alitumia mbinu nyingi sana kwa
kunibembeleza na hata kulia mbele yangu ili tufanye tu mara moja ila
nilikataa, alisema atavumilia hadi siku ya ndoa yetu ambapo tulipanga
kuoana mwaka sept 2009. Siku moja aliniambia twende kwenye kumbi za
starehe na mimi kwa sababu ya upagani na kumwamini pia kwa sababu
nampenda nilikubali tulienda huko na kulikua na bendi fulani maarufu ya
mziki wa dansi ilikua inatumbuiza. Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi
wangu akaagiza pombe alianza kunywa huku akinionjesha, nilikataa kwa
sababu nilikua sijawahi kunywa pombe katika maisha yangu yote, hata
sijui alinishawishi vipi nilijikuta nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa
tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa 5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4
japokua nilikua nakunywa kidogo kidogo tu tena kwa kunywesha na mpenzi
wangu maana nikama nikua nanyweshwa kila baada kama ya dakika 25 ndipo
nakunywa mara moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila niliihisi tu
naonja ili kumlizisha mpenzi wangu.ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi
usingizi na pia nilijiona wa tofauti najua nililewa hata kama sikujua
kama nimelewa maana nakumbuka tulitoka pale huku amenishika mkono huyo
mpenzi wang. Tulikodo tax na kuondoka na siku hiyo aliniambia twende
kwake alikokua amepanga chumba maana tulikua na usingizi sana nilikubali
huku nikidhani hatuwezi kufanya mapenzi, tulifika salama na kuingia
ndani ukweli pombe ni kichocheo cha ngono na ningekua mimi ndio Raisi wa
Tanzania ningefunga bar zote, nilijikuta natamani kufanya mapenzi na
huyu mpenzi wangu hata alikua hana nia maana alijua atanichukiza sana na
uhusiano ungekufa siku hiyo lakini kwa sababu ya pombe nilimwambia siku
hiyo tufanye kidogo maana mwili wangu unataka ni kweli siku hiyo kwa
sababu ya pombe nilifanya mapenzi na huyo mpenzi wangu na baadae
akanipeleka nyumbani baada ya wiki mbili maana tulikaa wiki mbili bila
kuonana alikuja na kunieleza habari ambayo sikuihitaji katika maisha
yangu maana nilikua nasikia tu kwa watu wengine lakini sio kwangu
alisema ''JANE ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA SASA'' nilidhani utani lakini
aliniambia kuwa yeye ana ukimwi tangu mika mitano iliyopita na anapenda
tu ngono maana hawezi kuacha.nililia sana na baada ya wiki moja baadae
nikaenda kupima na kukutwa nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na
chanzo cha yote ni pombe, kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua
wanadamu wengi.Nilikua na ukimwi na kwa hasira maana mpenzi wangu
alihamia arusha huku akisema neno moja la mwisho kwamba ''shetani
amemtuma kuwaambukiza wanadamu ukimwi''.Sikujua sikujua sikujua
sikujuaaaaaaaaa basi tu ooh YESU nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa mzigo
ambao haukunistahili mimi, hata leo hua najiuliza kwamba nilijitunza kwa
miaka 23 yote lakini pombe na huyu wakala wa shetani wamenifanyia
hivi.Baada ya kujua nina ukimwi na hali hiyo nikaikubali na kulikua na
kundi kubwa sana la wanaume ambao walikua wamewahi kunitongoja na
niliwakataa sana kwa sababu hii nilikubali ili nami nife na wengi,
nilianza kumkubali kila mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3
niliwahi kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini
wakati huu nilmkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga na
akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua
kuwa namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao
wana ukimwi uliotoka kwangu. kiukweli tangu may 2009 hadi 2012
nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana ilifika kipindi nala na
wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa
na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa ukimwi wanadamu zaidi ya
10,000 na hili tangazo la ''TUKO WANGAPI'' huwa linaniliza kila siku
maana hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa
idadi kubwa sana ya watu.Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku naombewa
nilikutwa na mapepo mengi sana na hata waombeaji wakashangaa. ningejua
ningeokoka tangu nikiwa na miaka 5 ili lakini ndio hivyo sina jinsi wala
uwezo wa kubadirisha hali hiyo.Na naomba kila atakayesoma ujumbe huu
ajue kuanzia leo kuwa pombe ni dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza
pombe ni dhambi na kila kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi.hadi
sasa mtu yeyote hawezi kujua kama nina ukimwi na sikui MUNGU ana mpango
gani na mimi maana kwake yote yanawezekana nauamini uponyaji wake na
sijawahi kutumia ARV hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi
hata wewe kujua kama uovu huu nimefanya mimi.Ndugu zangu kama una ukimwi
nenda kanisani ukaombewe na kama una akili mpe YESU maisha yako maana
pia baada ya kifo ni hukumu yasalimishe maisha yako kwa YESU na
usiambukize wengine tena. Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi
tena na sitafanya hivyo wala sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa
uovu niliofanya na hadi sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki
na nilihudhulia misibani huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.Mwisho
nawashauli wababa kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni na waume
zenu, vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa au
kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye ukimwi
ni wengi kuliko unavyozani.fuata unachofundishwa kanisani na pia soma
BIBLIA na uwe mtakatifu.MUNGU akubariki
Source:http://maishaushindi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment