Sunday, February 17, 2013

Haki ya kuchinja wanyama: Desturi iliyokuwepo iendelee – Waziri Mkuu

IMG_0077
Sheikh Hasani Kabeke wa Mwanza  akichangia katika kikao cha klutatafuta muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji wanyama kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Banki  Kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)


IMG_0084
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0094
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0102
Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro wa uchinjaji  wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu  jijini Mwanza Februari 16,2013.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
IMG_0122
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.
IMG_0143
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Ahmed  Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa Buswelu, Athumani Ali  katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………….
Na  Frederick Katulanda
SAKATA la nani achinje nyama kati ya Waislamu na Wakristo bado linaumiza vichwa, ambapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu Waislamu kuchinja nyama yaendelee, hadi hapo maamuzi mengine yatapofikiwa na Serikali.
 Kufuatia hali hiyo, Pinda ameagiza kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kwamba kazi hiyo ifanyike haraka iwezekanavyo, na kisha ripoti yake iwasilishwe Serikalini kwa hatua zaidi za kimaamuzi.
Waziri Pinda ameyasema hayo muda mfupi uliopita leo, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, kuhusiana na kikao chake cha pamoja na viongozi wa Kikristo na Kiislamu, kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la Mwanza, kwa lengo la kutatua mgogoro wa kidini unaoonekana kuota mizizi.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda, imekuja siku chache baada ya kutokea mapigano makali baina ya wafuasi wa dini ya Kiislamu na Wakiristo kuzuka huko Buseresere-Katoro katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, ambapo mchingaji mmoja aliuawa kwa kuchinjwa huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya.
Aidha, Pinda alikemea vikali vurugu za kidini zilizotokea mkoani Geita, na kuwataka viongozi wa madhehebu yote ya dini kuheshimiana, kujenga mshikamano na kutohasimiana, kwani wao ni watu muhimu sana katika maendeleo na utulivu wa nchi.

Source:http://mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/1224-pinda-alipokuwa-geita-juu-ya-kuchinja-wanyama.html#.USDWlJHcg1Q

No comments: