Wednesday, February 27, 2013

TCRA yafungia vituo viwili vya redio nchini


Makamu Mwenyekiti wa  Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano(TRCA)Walter Bugoya akitoa tamko la kuzifungia Redio Imani  na Redio Kwa Neema kwa kipindi cha miezi 6 kutokana kutangaza matangazo yanayodaiwa kuwa ya kichochezi jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mkurungenzi wa Idara ya Habrio Maelezo Arthur Mwambene na Kaimu Mkurugenzi wav Utangazaji wa (TRCA)Andrew Kisaka.Picha na Fidellis Felix 

Vilevile kamati hiyo imetoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni kwa Kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kubainika pia kukiuka taratibu za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi
re

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu ya kuvifungia muda wa miezi sita vituo viwili vya redio za dini, Imani na Kwa Neema kwa kile kilichoelezwa ni kuendesha vipindi vya uchochezi.
Vilevile kamati hiyo imetoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni kwa Kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kubainika pia kukiuka taratibu za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi kilichotafsiriwa kuwa ni cha uchochezi.

Kamati hiyo ya maudhui ilitangaza adhabu hizo jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ikisisitiza kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinazingatia maadili.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA,Walter Bugoya alisema TCRA imefikia hatua hiyo baada ya kuyafanyia uchunguzi wa kina malalamiko yaliyotolewa na wasikilizaji wa vituo hivyo vya redio.

Bugoya alisema redio hiyo ilitangazia wasikilizaji wake wasishiriki kwenye mkakati huo wa Sensa ya Taifa kwa kile walichodai kulingana na imani ya Kiislamu, wasingejua hatima ya mkakati huo.

Kuhusu Redio Kwa Neema inayorusha matangazo yake kutokea Geita, Bugoya alisema ilieneza uchochezi dhidi ya mtafaruku wa kidini uliozuka mkoani humo juu ya upande gani una haki ya kuchinja wanyama kwa ajili ya kitoweo.

Akizungumzia Kituo cha redio cha Clouds, Buyoga alisema kamati imeitaka kulipa fidia ya Sh5 milioni baada ya kubainika kuwa nacho kilienda kinyume cha maadili ya utangazaji kupitia kipindi chake cha Power Break Fast, cha Jicho la Ng’ombe walitoa kauli za uchochezi.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1705746/-/127h4m2/-/index.html

No comments: