Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas
wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa
Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara
Mirefu huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu
wasiofahamika- na kufariki dunia.
Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.
Padre
Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani
kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la
Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na
kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo
kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.
Mwanahabari
anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao
wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema
ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike
Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.
Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.
No comments:
Post a Comment