Thursday, February 21, 2013

KAHABA ALIYEOKOKA

Hili ni simulizi la  kweli linalomhusu mwanamke  mmoja ambaye alikuwa ni kahaba  wa makahaba......

Mwanamke  huyu  alijitambua  vyema  na  kukiri  ndani ya  nafsi yake kuwa hawezi  kuolewa  na maname  yoyote  yule  maana  jamii yote ilikuwa inamtambua  kwa uchangudoa  wake......

Kwa hiyo , ili kurahisisha mambo na  kuifanya  biashara  yake  iimarike, mwanadada  huyu aliamua  kwenda hospitali kukitoa  kizazi chake.Hakutaka  tena  usumbufu wa kutoa  mimba  au kufikiria kutumia kondomu......

Tangu wakati  ule biashara  yake  iliimarika na wateja  walizidi kumiminika.Baada  ya miaka  kadhaa, Upako  wa  Mungu  ulimfikia kupitia kwa mtumishi  mmoja  wa  Mungu ambaye  alifanikiwa  kumfanya  aokoke  na  kuwa mtumishi mzuri  kanisani.....
 
Siku moja, mchungaji  mmoja alimwita na  kumwambia  kuwa:
"Dada yangu, Mwenyezi Mungu  amenena  na  mimi na  kunifunulia  kuwa  wewe  ndo mke  wangu wa ndoa, hivyo naomba tuoane.."

Mwanamke huyu alitabasamu na kusema:
 "Kaka  yangu, Mungu hajakwambia lolote, lasivyo, utakuwa  hujamsikia vizuri.Naomba  uniache tu maana  sina  mpango wowote wa  kuolewa"

Yule  mchungaji  aliendelea kushikilia  msimamo wake  na  kudai kuwa :

"Mungu  amenifunulia,wewe  ndo  mke wangu" 

Mwanamke  huyu  aliendelea  kuyapuuza  maneno hayo na ndipo sakata  hilo  lilipomfikia  Askofu  wa  kanisa  hilo.....

Wakiwa mbele  ya mchungaji,Mwanamke huyu  alifunguka  kwa  uwazi mbele  ya askofu  na  kudai kuwa kabla ya kuokoka yeye  alikuwa  ni kahaba  wa  makahaba....

Askofu naye alifunguka  na  kudai kuwa :"Sioni sababu ya kuumiza kichwa  kwa  mambo yaliyopita.Mungu  humsamehe  mwanadamu  kwa  kuzifuta  dhambi zake  zote za  nyuma  na  kumfanya  awe  mpya..!!!"

Mwanamke huyu  alifunguka  tena na kudai kuwa:
"Baba  askofu, mimi  nilishatoa kizazi changu  wakati nikiwa  kahaba, kwa hiyo  sitaweza    kuzaa  tena"
Askofu  aliishiwa  pumzi baada  ya kusikia hivyo.Hakuweza tena  kusema  kuhusu  kusahau ya  nyuma.Ilibidi amgeukie yule mchungaji  na  kumwamba: 

"Vipi, bado  kuna maono yoyote  toka  kwa mwenyezi Mungu?" 

Mchungaji alijibu  ,"Ndio, huyu ndo mke wangu.."


 Askofu  ilibidi  awaombee kwa  sala  maalumu.Hatimaye ndoa  ikafungwa......Baada  ya  miezi  michachtu, huyu mwanamke  alibeba  mimba.Yeye  pamoja  na mumewe waliongozana pamoja kwenda  hospitalini, tena  kwa  yule  yule doctor  aliyekitoa  kile  kizazi......

Daktari  alipomuona  alifurahi  akidhani kuwa pengine  mteja  wake  kamletea  mteja mwingine.....Doctor  hakuamini  masikio  yake baada  ya kuambiwa kuwa  huyu  mwanamke ni mjamzito na  amekuja  kujiandikisha  clinic....
Hakika Mungu ni  Muweza wa  yote....

No comments: