Wednesday, August 6, 2008

BREAKING NEWS

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Dr. Barnabas Mtokambali amepita bila kupingwa kwenye uchaguzi wa kumchangua askofu mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG).Katika idadi ya kura 1493 zilizopigwa katika hatua ya awali ya kupendekeza majina ,Dr. Mtokambali amepata kura 1040 na kuwashinda wapinzani wake wengine aliokuwa nao katika kinyangányiro hicho.Askofu Mtokambali ambaye pia ni mchangaji kiongozi wa Kanisa la TAG Morogoro mjini la Bethel Revival Temple amekuwa akiungwa mkono na idadi kubwa ya wachugaji vijana na wazee wa miaka mingi katika kanisa hilo ni msomi aliyebobea wa kiwango cha PhD katika maswala ya theolojia na Huduma.
Tutaendelea kuwaletea habari zaidi za matokeo ya uchaguzi huo kadri tutakavyopata.

Stay tuned

2 comments:

Anonymous said...

Nawapongeza Sayuni kwa kutuweka hewani live.
Mungu awabariki sana.

LM - Canada

Anonymous said...

Narudia tena na tena, TAG mmeyaacha mbali sana makanisa mengine, hamna itikadi za kichama, wala wenyeviti au maaskofu wa mpaka kufa