Sunday, August 24, 2008

Kweli sasa tuombe tena kwa bidii..

Bwana Yesu asifiwe wapendwa wote!
Ninachukua nafasi hii kuwakumbusha wapendwa wenzetu popote pale duniani, tujipange wote kushika sana zamu zetu ili kuiombea nchi yetu na wakristo wenzetu popote pale duniani.
Hapo chini kuna makala inayozungumzia habari za familia moja iliyompokea Bwana wetu Yesu Kristo, na kisha wakakamatwa na kuteswa sana na dola ya huko Iran. Nawasihi tuchukue muda wetu kumwomba Bwana Yesu aingilie kati na kufanya kazi yake ifanikiwe, kama aliweza kwa Sauli akawa Paulo, anaweza na huko pia, kama aliweza kumtoa Petro gerezani,anaweza hata sasa, jamani tuombe.

Kuna post pia inamwonyesha mbunge mmoja akitushawishi kuwa hakuna hasara zozote za kujiunga na OIC, ile jamii ya nchi za Kiislamu, sisi wote tunaelewa kauli ya Bwana juu ya hili. Vita vyetu si vya damu na nyama, tushike zamu zetu Kuomba.

Wote mnalikumbuka suala la mahakama ya Kadhi, namna lilivyoshika kasi kule bungeni.Asante Mungu kwa wabunge aliowatumia kuzungumza kusudi la Bwana, wapendwa, tafadhali tuchukue muda kwa pamoja kumwomba Mungu, tusisubiri mpaka mambo yaharibike.

Bwana atutie nguvu, tuungane, hata ikibidi kuanzisha vikundi vya maombi, kwa ajili ya kuombea kusudi la Mungu ktk nchi yetu.

Mbarikiwe wote, Karibuni Sayuni.


No comments: