Wednesday, August 6, 2008

TAG kufanya uchaguzi wa askofu mkuu leo

Kanisa la Tanzania Assemblies of God linafanya uchaguzi wake mkuu wa viongozi wake wakuu wa kanisa hilo leo hapa jijini Dar es Salaam katika mkutano wa siku 3 unaotazamiwa kufanyika katika majengo ya chuo cha usafirishaji Mabibo.

Tetesi zinasema kuwa wanaotazamiwa kuingia katika kinyangányiro hicho ni pamoja na askofu mkuu wa sasa , Ranuel Mwenisongole (Dar),Askofu Mtokambali(Morogoro) anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo ,Askofu wa zamani wa kanisa hilo Mzee Emmanuel Lazaro(Kilimanjaro) na Askofu mkuu msaidizi wa zamani wa kanisa hilo Mchungaji Swai (Kinondoni jijini Dar).

Mlima sayuni imetuma timu ya waandishi wake mkutanoni hapo kuwapatia yale yanayojiri hapo na matokeo yote ya uchaguzi huo.

Stay tuned...

No comments: