Sunday, August 3, 2008

Mtoto wa mchungaji awa balozi wa pombe ya redds

ANGELA LUBALLA AWA BALOZI WA REDD'S


Miss Temeke, Angela Luballa ambaye pia ni mtoto wa mchungaji na askofu wa kanisa la kipentecoste la World Alive Church Askofu Deo Luballa amechaguliwa kuwa Balozi wa bia aina ya redd's na pia amefanikiwa kuingia Top 5 za Vodacom Miss Tanzania zilizofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Agosti 2, 2008.


Source: globalpublisherstz.com

4 comments:

Maranatha said...

Hapa sasa patamu kwelikweli!! Naam ni TEGO la Ibilisi kwa huyo Askofu na kalitafuta mwenyewe!! Sasa na turudi kwenye kauli za babaye ambaye ni Askofu. Atueleze ndio mtoto wake kwa kipawa chake mwenyewe, Je kweli alimtangaza Kristo katika hatua yeyote ile ya hayo mashindano? Na sasa amekuwa Miss Pombe - Tanzania, je hapo kuna ulokole tena? Nambie akishika kopo la hiyo pombe kuwaonesha jinsi anavyokamua hicho kinywaji halafu Jumapili anaingia kanisani na kushiriki Meza ya Bwana je huo ni wokovu tena? Nina mashaka na hiyo dini yake huyo dada! Natamani sana kusikia mahojiano ya huyo Mchungaji juu ya kuchaguliwa kwa mtoto wake kuwa Promota wa pombe Tanzania! tafadhali Mtade kama utapata nafasi jitahidi kuongea na huyo Baba Askofu, au wale wadau walio kuwa wanam-support mpaka kwenye Radio, Je bado wanaendelea na misimamo yao juu yake au ndo wamemtosa dada wa watu?

Anonymous said...

Mlokole awa Mtangazaji wa pombe!!! Balaa tupu! sitashangaa kesho tukisikia na mwingine kawa Miss SIGARA!! Tehehehetehehetehehe

Anonymous said...

Naona majadala sasa umefungwa na kila mtu amepata jibu sahihi na kuridhika. Walisema kupitia Miss Tanzania anamtangaza Kristo yako wapi sasa?

Please tunaomba tusikie maoni ya huyo baba yake anasemaje?

Anonymous said...

acheni ushari,,,
kila mtu analo pito lake na kosa fulani alofanya,,,
Yesu alisema kwa yule mwanamke kahaba asiye na dhambi awe wa kwanza kutupa jiwe,,be prayful