Saturday, August 2, 2008

Uvaaji wa kitambaa kichwani kwa wanawake...!

Nimepokea swali hili kutoka kwa mdau wa sayuni anaomba ushauri wa swala hili..

karibuni wapendwa tujengane kiroho.

Bwana Yesu asifiwe.

Mimi binafsi kuna swali ambalo ningependa kuuliza, Ni kuhusu uvaaji wa kitambaa kichwani wakati wa kusali (kwa wanawake kufunika kichwa)

Je hilo jambo tunalichukuliaje maana tukisoma biblia 1Wakorinto 11:13 inatuambia tufunike vichwa, lakini wanaume wasifunike vichwa vyao wakati wa kusali.

Kwa wanaume wanafanya hivyo, lakini wanawake tunalitafsiri vipi hilo neno, maana linaniacha njia panda.

Mungu azidi kuwabariki, asante.

No comments: