Bwana YESU asifiwe,namtukuza mungu kwa matendo yake makuu ninayoyaona.Ninafanya kazi ya udereva na ufundi wa magari kwa ndugu yangu mwarabu,chaajabu ni kuwa mda wa miezi miwili hatujapata sijapata mshahara,ninaye mke na watoto,lakini wenye haki wataishi kwa imani,hatujapungukiwa na chochote zaidi ya hayo tumezidishiwa,hii ni kuwa MUNGU hata wakati mwingine amemugusa boss huyo na kunipa kazi za ziada na kuzilipia inje ya mshahara mungu amegusa watu naona wakija nyumbani na nafaka.Kweli wapendwa MUNGU yupo,alivyowalisha wana waisrael jangwani,kamlisha eliya,waaminio msisumbuke na kupanda kwa maisha duniani kwa YESU kuko sawa,ila tuutafute kwanza ufalme na haki yake mengine yote mtazidishiwa,na tufanye kazi kwa bidii tutamuona MUNGU akiwa upande wetu.Mbarikiwe
SAYUNI: Bwana Yesu atukuzwe kwa hayo yote.Tena ni maombi yetu kuwa Bwana Yesu aendelee kujifunua kwa huyu ndugu, afanye zaidi na zaidi, amfanya kuwa kichwa na sio mkia kila eneo, Ambariki atokapo na aingiapo, aibariki kila kazi ya mikono yake, uzao wake ubarikiwe popote waendapo, na mshahara wake pia apewa vizuri sana bila usumbufu wowote. Amen
No comments:
Post a Comment