Sunday, May 4, 2008

Je hii ni sahihi?

Kuna mambo mengi yamekuwa yakinitatiza kwa muda mrefu katika makanisa yetu haya tunayoyaita ya kiroho..
Moja ya mambo hayo ni suala la watumishi wa Mungu kuwapa washirika wao vitisho kiasi cha kuwafanya washirika hao kuwaogopa kwa kuwaona wao ni miungu watu.Mara nyingine unaona mlokole anamsifia mchungaji au mtume au nabii au mwinjilisti au mwalimu anayeongoza huduma alipo huyo mlokole kana kwamba huyo mtumishi wa Mungu ni substitute ya YESU..Nimewahi kuona mara nyingi mtu anasema kuwa yaani mtumishi flani ni kama YESU jamani.Huyu mtu anatisha jamani….hivi watumishi wa Mungu tunalipeleka wapi kanisa la Mungu?Hivi ndivyo tunavyowafundisha washirika wetu au ni nani kawafundisha hawa washirika wako wakuone wewe ni kama upo sawa na YESU kiasi cha kukutukuza wewe tu muda wao wote nakuona bila wewe maisha yao ya wokovu ni kama bure?
Nafahamu wapo watumishi wengi wa Mungu walitangulia mbele za Bwana na walikuwa wamewafundisha washirika wao vizuri kiasi kwamba hata walipoondoka wao bado kondoo wao waliendelea vizuri na kuchanua na kuzaa matunda bora.Ila nina wasiwasi na kondoo hawa wa watumishi hawa kama

2 comments:

Anonymous said...

Mtumishi asante nadhani wiki hii tulikuwa tunawaza jambo moja!! ili ni tatizo na inabidi kweli kuwa wakali kuiondoa hali hii.

''Akawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye Mamlaka juu Yao huitwa Wenye fadhili; lakini kwenu ninyi sivyo; Bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye.Luka 22:25-27''

Htuna watumishi wa mfano wa Yesu, huo ndio ukweli!! watumishi wanatumia jina la Yesu kimakosa hawafanyi ya Yesu!!!

Anonymous said...

hapa sio sawa wanafanana kwa sababu lwasipofanana na yesu kitabia hatuna haja nao madhabahuni.wanaowasifia ndio wenye shida watumishi hawajawatuma wawasifu.yesu ni mkuu.