"Hizi ni siku za mwisho." Ndivyo unavyoweza kuyaeleza matukio mawili ya kishirikina ambayo yamejitokeza katika Jiji la Dar es Salaam ndani ya muda wa wiki moja.
Awali, simulizi hizi zilionekana kama hadithi za kutunga au sinema, lakini sasa zimedhihirika wazi kuwa za kweli baada ya mtoto mwingine wa kike mwenye umri wa miaka 18 kushikiliwa na polisi kwa madai ya kujihusisha na ushirikina.
Binti huyo, Rehema Kefa (18) amekamatwa juzi kwa madai ya kuwa katika harakati za kutafuta damu na miili ya binadamu. Inadaiwa kitendo hicho alikuwa anakifanya katika zahanati iliyoko Tabata, Dar es Salaam.
Binti huyo amekamatwa siku nne baada ya mtoto mwingine wa kiume, Ramadhan Mussa (18)kunaswa katika eneo la Hospitali ya Taifa Muhimbi kwa tuhuma za kukutwa na kichwa cha mtoto amabcho alidai kuwa ni anampelekea shangazi yake kama zawadi.
Ilidaiwa kuwa alipokamatwa na kuhojiwa juu ya kichwa hicho, Ramadhan aliyedaiwa kuwa na umri wa miaka 12, alikitoa na kuanza kukitafuna.
Ramadhani alikutwa na kichwa cha mtoto Salome Yohana (3) aliyeuawa Ijumaa usiku kwa imani za kishirikina na kuzikwa juzi kwenye makaburi ya Tabata Segerea, Kwa Bibi juzi.
Lakini Rehema alipokuwa anajieleza baada ya kufikishwa katika kituo cha Polisi Buguruni, jijini Dar es Salaam jana alidai yeye ni mkazi wa Tabata Msimbazi na kukiri kuwa alifika katika Kituo cha Afya Tabata kwa agizo la bibi yake .
Alidai bibi yake alimwagiza akamchukue mtoto aliyezaliwa na damu ya mama mzazi kwa ajili ya masuala yao ya binafsi.
Binti huyo, mrefu wa wastani na mwenye umbo la kuvutia alisimulia bila woga wala hofu kuwa yeye pamoja na mabinti wenzake watatu wamekuwa wakitumiwa na bibi yake aliyemtaja kwa jina moja la Asha.
Aliongeza kuwa wamekuwa wakitumiwa kwa shughuli za kichawi na wamekuwa wakishiriki pia kula nyama na hata kunywa damu za binadamu.
Kama vile haitoshi, alitoboa siri kuwa kuwa siku hiyo, juzi alianza kujisikia vibaya baada ya kufika katika Hospitali ya Tabata, saa 10.30 jioni alipokuwa ameagizwa kumchukua mtoto na damu ya mama kichanga hicho aliyezaliwa siku hiyo.
Alieleza kuwa alipofika hapo alijikuta akinasa kwenye mtego na hivyo kulazimika kumweleza ukweli Afisa Muuguzi, Magreth Mapunda (45) aliyekuwa akimsaidia mama mmoja aliyekuwa akijifungua.
?Mimi nilivalishwa ujuzi (uchawi) na bibi yangu ambaye aliniagiza nichukue na kumpelekea mtoto aliyekuwa akizaliwa hospitalini hapo. Huo, kwangu ulikuwa mtihani wangu wa kwanza ambao kama ningefaulu, basi ningepewa cheo cha kitaalamu cha mama yangu kama zawadi,? alisimulia.
Alieleza kuwa alipofika katika zahanati hiyo alijikuta ghafla akikutana na nguvu isiyo ya kawaida kwake ambayo ilimzuia kufanya alichotumwa na pia alishindwa kuondoka mahali hapo hadi alipokutana na muuguzi huyo, ambaye alijikuta akilazimika kumweleza ukweli.
Aliongeza: " Nimekuwa nikifanya shughuli hizo kwa kushirikiana na mama na bibi yangu , lakini bila baba yangu kujua kuwa mama nani tunashiriki katika masuala hayo.
Binti huyo aliendelea kusimulia kuwa, katika tukio hilo ambalo wananchi wengi wa maeneo ya Tabata na wapita njia walishindwa kulivumilia na kukusanyika nje ya zahanati hiyo baada ya kupata taarifa zake jana saa tano asubuhi kwalengo la kumshambulia na kumdhuru.
Alieleza kuwa, alisaidiwa kwanza na mama yule (muuguzi) kwa kumpeleka kwenye maombi katika kanisa moja lililopo Ubungo na kuombewa kwa usiku mzima, kabla ya kurejeshwa Tabata.
Rehema ambaye alisema kuwa amekuwa akiishi na baba yake (ambaye hakutaka kumtaja jina) ambaye alidai kua amekuwa akitofautiana naye mara kwa mara amekuwa akiogopa kurejea nyumbani kwa kuwa anaweza kudhuriwa baada ya kubainika kuwa anashiriki katika uchawi.
"Ninakumbuka tulipoondoka juzi, tulitumwa tukiwa wasichana wanne, wote tukaagizwa kwenda kwenye maeneo tofauti. Mimi nilitumwa Zahanati ya Tabata, mwenzangu alikwenda Hospitali ya Amana, mwenzetu mwingine akaenda Muhimbili ( Hospitali ya Taifa) na wa mwisho kule Hospitali ya Temeke. Lakini, sijui wenzangu wako wapi na katika hali gani, nimepoteza mawasilano nao," alisema.
Aliwataja wenzake kuwa ni wakazi wa Kipalang?anda, Kisarawe na Jaribu huko Kimanzichana, mkoani Pwani.
Akielezea alivyokutana na binti huyo, Ofisa Muuguzi wa Zahanati ya Tabata, Magreth Mapunda ambaye alikiri kuwa ameokoka, alisema alikuwa katika shughuli zake za kawaida akimsaidia mama aliyekwenda kujifungua hospitalini hapo na mara alipotoka alikutana na wauguzi wenzake ambao walimtaka amsikilize binti huyo aliyekuwa akihangaika muda wote tangu alipofika hapo.
Alisema kuwa alipomhoji, msichana huyo alishindwa hata kumwelewa ndipo alipoamua kumfanyia maombi, ndipo binti huyo alijipotambua na kumwelezea kilichompeleka kwenye zahanati hiyo.
"Alinieleza wazi kuwa yeye ni mchawi na kwamba alikuwa ametumwa na bibi yake kuchukua damu ya mtoto kwa madai kuwa huwa wanafanya hivyo na kwamba wakifanikiwa huwa wanakunywa damu hizo na kula nyama za binadamu," alisimulia muuguzi huyo.
Aliongeza kuwa baada ya kumsikiliza kwa umakini, niliamua kumpeleka katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo, Dar es Salaam ambako aliombewa.
Maombezi hayo yaliongozwa na wachungaji Mwaijumba na Daniel na baada ya purukushani za muda mrefu binti huyo aliziduka na kurejea katika hali ya kawaida na alikuwa akirudia maelezo yake bila kupoteza kumbu kumbu.
Hata hivyo, binti huyo alisema anaogopa kurudi kwao kwa hofu kwamba huenda wenzake wakamdhuru kutokana na mtandao walio nao, ambao huwasiliana kwa kutumia vioo kila wanapotaka kukutana.
Alifichua kuwa bibi yao hutumia aina moja ya simu ambayo hunasa mawasiliano ya maeneo yote walipo watu wake.
Binti huyo anashikiliwa katika kituo cha Polisi Buguruni kwa usalama wake na uchunguzi.
Hata hivyo, pamoja na kuandikisha maelezo yake, Mkuu wa Kituo hicho, OCD Akili Mpwawa, aliagiza apelekwe hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina kabla ya kuchukuliwa kwa hatua nyingine
No comments:
Post a Comment