Thursday, May 1, 2008

Uchaguzi wa Fellowship ya ICF -Uhasibu Arusha wafana

Mungu apewe sifa zote! Wiki iliyopita hapa katika chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) katika fellowship isiyofungamana na dhehebu lolote ya ICF, tulishuhudia uwepo mkuu wa Mungu katika uchaguzi muhimu sana wa viongozi wa Fellowship kwa mwaka mzima wa 2008-2009.
Uchaguzi ulianza muda wa kawaida kuanzia saa moja kamili na ulikwisha kwenye majira ya saa tatu hivi usiku.
Tabia moja ya uchaguzi huu ni kwamba ulitanguliwa na maombi makubwa kutoka kwa watu wa Mungu ili kuomba hekima za Mungu katika uchaguzi huo.
Na kwa kweli tumemwona Mungu na tunamtukuza yeye.

Viongozi wapya waliochaguliwa ni:
Elihaika Bryson--Mwenyekiti
Rehema Stephen,---Makamu wake
Anganile Mbale---Katibu
Flora Kasian—Makamu katibu
Jameson—Mweka hazina
Zawadiel Gideon--Mwakilishi
Hellen Andrew---Mwakilishi
Tabitha---M.Kiti maombi
**Uchaguzi wa maombi bado unaendelea

Tunamshukuru Mungu kwa kutupatia wakinadada wengi safari hii, Je mwajua kuwa ki-Biblia wanawake wana nguvu kuliko wanaume? Sisi wana SAyuni tunawatia moyo katika Bwana,wasiogope KABISA kwani Mungu yu upande wao na hatawaacha wala kuwapungikia.
Tunawaomba wanasayuni wote tuungane kuwaombea hawa wapendwa kwa Bwana.

Mbarikiwe nyote daima, Amen.

No comments: