Monday, May 19, 2008

Kazi ya Mungu Zanzibar

Shalom wanasayuni,

Nilikuwa Zanzibar kwa siku 2,3 hivi na jumapili nilipata Neema ya kuabudu katika kanisa la TAG Kariakoo hapo Zanzibar.Kwa kweli nilivyokuwa naifikira Zanzibar ilivyo ni tofauti kabisa.Kwanza nilidhani nitakuta kakanisa kadogo kabisa kwa namna tulivyozoea kuona makanisa ya vijijini.Lakini nilishangaa sana kukuta kanisa kubwa kabisa la TAG lililopo hapo Zanzibar katika kati ya mji likiwa nawashirika kwa haraka haraka kama 600 au 800 hivi.Kwa kweli wakrsito wa Zanzibar wamenibariki sana kwani watu wako serious na Mungu,uimbaji wa kumtukuza Mungu na sio wa maonyesho na usanii.Mahubiri ya kumjenga mkristo na kumfanya awe mwanafunzi na sio mahubiri ya maonyesho na mbwembwe.Kwa kweli kila kitu kilinibariki.Mungu ambariki sana Mch. wa kanisa hilo Pastor Kadanga.

Nilitamani nifanye nae mahojiano nae lakini muda wangu ulikuwa mdogo sana.

Mungu awabariki wakrsito wa Zanzibar kwa kusimama na Bwana na kuinena injili ya wokovu bila uwoga.Kazi ya Mungu inaenda mbele Zanzibar..


Halaluyaa..!

2 comments:

Anonymous said...

Musijesema sikuwaambia hapo mwanzo!

kuna mashaida wa uwongo!!!!!

Mohamed Abdulrahman
UK

Anonymous said...

Mtade Asante mtumishi, nina furaha sana kuliona kanisa ambalo nimewahi kuabudu wakati nafanya kazi na kampuni ya Noremco kuikarabati bandari, hilo kanisa limenifanya siku moja nitamani tena kwenda kuabudu pale!! kipindi chao cha sifa kizuri sana, mchungaji wao mzuri sana na injili yake ni ya ajabu, jambo nililoligundua ni kuwa kuna nguvu sana ya Roho mtakatifu.

Pembeni hap pana shule moja nzuri mabayo kila jumapili watu na madhehebu yao wanakusanyika na kuabudu, tusisahau Zanzibar katika maombi.

Kalenge
Canada