Tuesday, May 13, 2008

NANI KASEMA ROHO MTAKATIFU NI DHALIMU?


ANGALIZO: Habari hii nimechanganya lugha kwa makusudi ili kwa wale wasio fahamu kiswahili walao wapate kidogo cha kuambua na kuweza kuchangia.

Kama kuna somo adimu na kitu kigumu ambacho kimewachanganya walio-okoka na hata wasio-okoka ni pale mtu anapotajiwa habari za Roho Mtakatifu: Maswali mengi yameulizwa na yapo yaliyopata majibu ya moja kwa moja na yapo mengine mpaka kesho mtu hawezi kuelewa mpaka naye apitie experience hiyo ya Roho Mt.
Questions like: Holy Spirit
  1. What is it?
  2. What does it do?
  3. What is it's purpose?
  4. How do you all "identify" it?

If I may respond to above queries I would say the Holy Spirit is not an "it" but a He. He is part of the Trinity, God the Father, God the Son and God the Holy Spirit. He is our helper, encourager, comforter, and strengthens us and illuminates our mind with the truth in the Bible.

John 15:26 "But I will send you the Counselor, the Spirit of Truth. He will come to you from the Father and will tell all about Me"

John 16:13 " When the Spirit of Truth comes, He will guide you into all truth. He will not be presenting His own ideas, He will be telling you what He has heard. He will tell you about the future. He will bring Me glory by revealing to you whatever He received from Me".

Sasa maswali mengi yapo hapa:
  1. Nitatambuaje kwamba ninaye huyo Roho Mt?
  2. Nitamtambuaje mtu anayesema ana Roho Mt?
  3. Nitatofautishaje kati ya Roho Mt. na roho Nyehu au Mtakafujo kama wengine wamwitavyo?
  4. Wanaposema Roho alisema nami au na mtu kwa wengi ni mkangayiko, una uthibitisho gani?
Wengi tumewasikia wakisema mwanzoni kwamba Bwana (kwa roho) amewaonesha lakini baadae utaja sikia haohao wakisema kwamba si kweli. Hivi ni kwa nini wengi wamemsingizia huyo Roho na kumfanya kuwa muhuri wa kuhalalishia matakwa yao?

Hebu tusaidiane hapa ndugu zangu na kuelimishana maana hizi ni zama za mwisho na maovu yameongezeka ikiwa ni pamoja na mafisadi wa kiroho!

Mchango wako wa mawazo ni muhimu sana!

7 comments:

Mtade said...

Nimefurahishwa sana na mada hii ya Roho Mtakatifu.Mungu akubariki Mtumishi Maranatha kwa kutuletea changamoto hii.Kwanza nilishtuka sana ulipouliza maswali ya what is it? Lakini nimefurahi kwa kuona kuwa umeelezea vizuri kuwa Roho mtakatifu sio it maana Yeye sio kitu bali ni personality.Ndio maana tunasema yeye ni Mungu.Mungu akubariki kwa hili...
Lakini lazima tukubuke kuwa Biblia inasema kuwa Mungu ni Roho (John 4:24) na tunajua kuwa Mungu mwenyewe amesema kuwa iweni watakatifu kama mimi Mungu nilivyo mtakatifu (1 Peter 1:16 ).Kwa hiyo Roho Mtakatifu ni Mungu mwenyewe.Yaani ni Roho Tatatifu ya Mungu.Na wala sio kitu flani au phenomenon flani hivi.Wakati mwingine watu wengi hudhani kuwa Roho Mtakatifu ni moto au ni nguvu flani au ni upepo flani au ni hali flani.HAPANA ...Roho Mtakatifu ni zaidi ya moto,zaidi ya upepo,zaidi ya maji mengi,zaidi ya hali yoyote unayoidhania.YEYE ni MUNGU...anaouweza wote,yupo mahali pote na anajua yote.Fahamu kwamba Roho Mtakatifu anazo nguvu na wala yeye sio nguvu ila anazo hizo nguvu.Kuna tofauti kubwa ya kuwa na nguvu na kuwa nguvu.YEYE ni zaidi ya nguvu..Biblia inasema katika Acts 1:8 "mtapokea nguvu akishawajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU"..angalia hapa..unapokea nguvu baada ya kujiliwa na Roho Mtakatifu na wala YESU hakusema kuwa Roho Mtakatifu ni nguvu bali anasema kwanza Roho Mtakatifu anawashukia then mnapokea nguvu...halaluya..unaona sasa ..kumbe Roho Mtakatifu anazo nguvu na wala YEYE mwenyewe sio nguvu ila anazo na anamiliki nguvu na ndizo anazotupatia ili kushinda dhambi.Kumbuka kuwa katika chumba cha juu wakati wale 120 wameketi wakisali na kumsifu Mungu Roho Mtakatifu akawashukia na ndimi za moto zikaonekana juu yao.Kumbuka kuwa Roho Mtakatifu hakuwa zile ndimi za moto bali aliwapa ile ishara ya ndimi za moto kudhihirisha uwepo wake.Kumbuka kuwa YEYE ni Roho na binadamu wa macho ya nyama hawezi kuiona roho hivyo Roho Mtakatifu huwa anapenda kujidhihirisha kwetu kwa ishara kama ya kunena kwa lugha au ndimi za moto au upepo au hali flani ili kudhihirisha uwepo wake.Kumbuka kuwa unaponena kwa lugha ile lugha yenyewe sio Roho Mtakatifu ila ni lugha ya Roho Mtakatifu.
Praise the LORD...

Sasa hebu angalia hapa kidogo...

Biblia inasema kuwa "msihuzunisha Roho Mtakatifu"...na mahali pengine inasema kuwa "msimzimishe Roho Mtakatifu" ...angalia kuwa Roho Mtakatifu huwa anahuzunika...kumbe anayonafsi na anao utashi..ana emotions na anazo wills...anaweza kuhudhunika maana ni personality..shemu nyingine Biblia inasema "Yesu akafurahi katika Roho Mtakatifu.."..unaona hapa kuwa Roho Mtakatifu huwa anafurahi na hata kucheka...
Pia Roho Mtakatifu huwa anayo matakwa yake (wills)..Biblia inasema kuwa "kama apendavyo Roho mwenyewe" (1Corinthians 12:11).
Unaona kuwa Roho Mtakatifu huwa anazo wills..hii yote inathibitisha personality ya Roho Mtakatifu.
Kuna wakati flani nilikuwa naangalia Television moja inayomilikiwa na mtume (jina kapuni) mwenye maskani yake katika wilaya ya kindondoni hapa Dar es Salaam..nilishangaa sana na kusikitika sana nilipoona huyu mtumishi wa Mungu akikemea pepo na kutamka maneno kuwa "NAKUAMURU Roho Mtakatifu ingia ndani yake" akimaanisha kuwa anamwamuru MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi aingie ndani ya mtu mwenye pepo ili aende akamtoe...hili jambo lilinisikitisha sana maana kipindi kile kilikuwa kinarushwa kwenye TV na watu wengi walikuwa wanaona.Sijui washirika wake walifunza nini kwa kauli ile.Inawezekana kabisa mtu yule mwenye pepo alifunguliwa lakini hiyo haina maana kuwa mtumishi huyu alifanya sahihi kumwamuru ROHO MTAKATIFU maana huwezi kumwamuru Mungu...unatakiwa kumwomba Mungu na kukikaribia kiti cha rehema kwa ujasili na sio kumcommand ROHO MTATATIFU...Najua kuwa mtumishi yule hakuwa na nia mbaya lakini pengine wakati mwengine hata watumishi wanahitaji kujifunza Biblia vizuri...unaweza kuamuru moto wa Roho Mtakatifu ushuke maana Roho Mtakatifu sio huo moto bali anao huo moto...
Kwa kweli somo la Roho Mtakatifu ni refu sana na lina mapana na marefu na vina virefu sana..
wakati mwingine Mungu akitujalia tutawaletea somo hili kwa upana wake.
mtumishi Maranatha Mungu Roho Mtakatifu akubariki sana kwa kutuletea changamoto hii ili tuijadili na kujifunza kitu..

By Mtade

Anonymous said...

hebu nijaribu kusema princple fupi

Roho Mtakatifu+Yesu+Baba=1!!

Roho mtakatifu atasema kile kitu tu amabcho kinapatikana katika neno la Mungu kinyume na hapo ni uongo, maana kamwe hawezi kwenda kinyume na Yesu au Baba maana wao ni wamoja.

Rafiki tuliyenaye kwa karibu sana kila mahali ni Roho,Roho ndio anatawala sasa naye anafundisha, anafunua, anaelekeza,yote ambayo Yesu alisema.tena anafariji, anatupa nguvu,anatukumbusha, anajali anaokoa, anaponya, mtendaji wa Yote, mwombezi n.k

Kalenge

Anonymous said...

Haleluya..Aisee Mwalimu Mtade uliyefundisha somo hapo juu,natamani uendelee kufundisha, nilikuwa nimenogewa na somo lako,maana umeelezea vizuri na Neno limeingia ndani yangu na kunifungua vizuri sana..Ubarikiwe sana.

Danny.

Anonymous said...

Ni kweli kwa mliyofafanua hapo juu haswa Mtade. Ila inakuwaje kusikia watu wakisema Roho kaniambia halafu baadae anageuka kama Maranatha alivyosema kwenye blog?Ni roho kweli au anamsingizia?

Kuna hata watumishi wanasema kanisani kwamba Bwana kawaonesha kwamba fulani ni mchumba wa fulani halafu baadae mambo yanakuja kuwa magumu, maana yake nini? Upo ushahidi mwingi tu wa matumizi mabaya ya huyo Roho mnasemaje katika hili au naye ni roho?
Tutawatambuaje hawa watu kama ni waongo? Ninaogopa sana maana ako wengi kanisani na wengine hata wamefungua makanisa yao!

Mtade said...

Somo la Roho Mtakatifu ni moja kati ya masomo yanayowasumbua watu wengi siku zetu za leo.Miaka ile ya zamani kidogo ilikuwa mtu akioka anakaa chini anafundishwa neno ipasavyo.Nakumbuka kipindi kile ilikuwa unafundishwa nini maana ya kuokoka,mkristo anapaswa awe vipi au aishi vipi,mambo ya mabatizo,na Roho Mtakatifu na karama zake 9.
Lakini siku hizi hali imekuwa ni tofauti kabisa kwani mtu anapookoka utaona tu watu wanaanza kunena kwa lugha (sina hakika kama huwa wanaigiza kile wanachosikia kwa viongozi wao au ni kweli ni lugha ya Roho Mtakatifu).Sina tatizo na mtu kuokoka na kuanza kunena kwa lugha muda huo huo but nadhani kuna ulazima wa kuwafundisha watu kwa undani kabisa kuhusu Roho Mtakatifu.Huwa najiuliza mara nyingi inakuwaje mtu ukwazane na ndugu yako kiasi au mke wako afu uende kuomba na kuanza kunena kwa lugha kana kwamba hakuna kilichotokea.Ndio maana YESU alisema kuwa ukiwa na daawa na ndugu yako kabla hujaenda kuomba au kutoa sadaka yako iache madhabahuni kwanza na uende ukapatane nae then urudi uitoe.Na atakaye kukumbusha hayo ni Roho Mtataktifu maana Neno linasema kuwa atatwaa kutoka katika yaliyo ya YESU na kuwapasha habari zake....haleluyaaa....umeona sasa hapo....
Mimi nasema kuwa matatizo mengi tuliyonayo siku hizi ni kwa kutokumfahamu vizuri Roho Mtakatifu.Ndio maana utaona mtu anasema kuwa nimeambiwa na Roho kuhusu jambo hili na mara baada ya Muda utaona huyo huyo tena anageuka na kusema kuwa yule hakuwa Roho...sasa watu wa namna hii huwa wanatuchanganya sana kwani inatupa shida kuwaamini tena kuwa tutawaaminije kuwa aliyewaambia kuwa wa kwanza hakuwa Roho ni Roho Mtakatifu....

Kama wakristo wangefundishwa vyema kuhusu Roho Mtakatifu hata maaskofu wetu wasingekuwa wanatumia muda mwingi kuwahubiria watu kuhusu mawigi au kupaka rangi kucha au kuseti nywele na kadhalika...kazi hii ingefanywa na Roho Mtakatifu..na sio kama viongozi wetu wanatumia muda mwingi kuwahubiria ibada nzima wanawake wasipake rangi kucha au kuvaa wigi na kadhalika wakati kumbe watu hawa hawajajaa Roho.
Biblia inasema vita vyenu vyatoka wapi? mapigano yatoka wapi? si katika hizi tamaa zenu mbaya...? ..unaona sasa kumbe hivi vita vya makanisa na huduma kupigana madongo ..mara leo huyu anasema Mungu anaangalia moyo kesho huyu anasema Mungu anaangalia mavazi ....yote haya yanatoka katika tamaa zetu tu....
Jamani jamani lazima tukubali kuwa Roho Mtakatifu hajapewa nafasi ya kutosha katika makanisa yetu ndio maana tunasigana namna hii..
Watu hawajafundishwa vyama...imefika kipindi watu wanadhani mtu akinena tu hata kama anaigiza hiyo lugha basi amejazwa na Roho Mtakatifu...kuna tofauti ya kujazwa na Roho Mtakatifu na kujaa Roho Mtakatifu...(Somo hili nitafundisha nikipata nafasi siku nyingine)....praise the LORD...
Lazima tujue kuwa karama 9 anatoa Roho Mtakatifu, Huduma 5 anatoa Yesu mwenyewe na huduma zile nyinginezo mbalimbali kama maongozi,kuonya nk anatoa Mungu Baba...(Soma Warumi 7,Waefesio 4 na Wakorintho 12)..

Mungu awabariki sana...

nitarudi tena baadaye...

Mtade

Anonymous said...

Hello!
HIVI NIKWELI MUNAAMINI KWAMBA ROHOMTAKATIFU+YESU+BABA=1???

BEFORE YESU HAJAJA!
ROHOMTAKATIFU+BABA=1-YESU=NGAPI?

CHANGANUA ROHOMTAKATIFU=?, BABA=? NA YESU=?

MOHAMED

Anonymous said...

Mohamed!
Ndio sie twaamini kwamba Roho Mt.+Yesu+Baba ni kitu kimoja. Ni sawa na mwanadamu alivyo katika hali tatu: Nafsi, Roho na mwili. Kama wewe huna roho una nafsi na mwili tu, nakupa pole! Ndo maana mtu akifa maiti yake hatusemi Hashim kalala hapa, bali mwili wa Hashim. Yuko wapi Hashim mwenyewe? Ni ile roho na nafsi ambavyo vimetoka na kuacha mwili. Kwani mwili asili yake ni hapa duniani na lazima ubaki hapahapa duniani.

Katika Mungu, yeye hana mwanzo wala mwisho na katika yeye utatu wake wote watenda kazi. Yaani Baba, Mwana na Roho mt.

Ila nikutahadharishe tu haya mambo ukiyaingilia kichwakichwa utapotea ndugu yangu. Lazima ukubali kufundishwa na pia kuelekezwa vinginevo ukileta ubishi kama ulivyokuwa mkijadili mada fulani hapo nyuma hutaambulia kitu kamwe!

Karibu tena!
Mdau - Muscat