Monday, May 19, 2008

Kakobe na Injili ya mawigi

Kwa takribani week 2 sasa zimepita tangu Askofu Kakobe aanze kurusha series ya vipindi vya mahubiri yake yanayoelezea mapambo ya wanawake kama mawigi,rangi za kucha,kucha bandia,kujichubua, kujiremba kwa kuchonga kope na nyusi bandia na mambo yanayoendana na hayo.Alianza kwa kuwashambulia wale wanaopiga power na kuwaangusha watu, wale wanawakumbatia watu madhabahuni n.k.Mafundisho haya yameleta mgongano mkubwa wa kimawazo miongoni mwa wapentecoste nchini na ikumbukwe kuwa jambo hili si geni hapa nchini kwani miaka ya 70,80 na hata mwanzo mwa miaka ya 90 lilipigiwa kelele sana kiasi cha kuleta mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wapendwa hapa nchini.
Kwa sasa jambo hili ni kama askofu Kakobe ameliibua upya na kuleta changamoto kubwa miongoni mwa jamii ya waaminio.
Jambo la kujiuliza hapa ni je...jambo hili linajenga mwili wa Kristo au linabomoa..?

1 comment:

Anonymous said...

swali gumu sana, lakini nadhani Kakobe ana wahubiria watu ambao wameokoka na kukomaa!!! ni vizuri injili ikahuburiwa na watu wakafundishwa na hatimaye kazi ya Yesu ndani ya mtu iamue,nachela kusema kuwa isije ikawa sheria,

ni vizuri mtu akabadilishwa kabisa akaacha uovu,WIGI TUNALIONA KWA NJE, LAKINI DHAMBI ZINGINE HATUZIONI, na mtu akiokoka anakuwa mtoto mdogo, anahitajiwa kulelewa na kufikia kuliona hili kakobe analosema,

inahitaji mtu wa Rohoni sana kuelewa na mtu wa rohoni kukubali, ndio maana nasema Roho afanye kazi, hili mtu huyu asiishie kuacha dhambi tu ya kuvaa wigi bali zote hata tusizoziona


Kalenge