Saturday, August 23, 2008

Hakuna madhara kujiunga na OIC

Serikali imesema hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (IOC).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, aliyasema hayo jana bungeni wakati akifunga mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake jana.

Akiwasilisha hotuba hiyo juzi, wizara hiyo iliomba iidhinishiwe Sh. 69,405,738,700 ambapo kati ya hizo Sh. 52,355,164,900 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, Sh. 10,500,000,000 kwa ajili ya maendeleo na zilizobaki kwa ajili ya mishahara pamoja na maduhuli ya serikali.

Waziri Membe, alisema serikali mwaka huu, imefanya kikao na Baraza la Wawakilishi kuhusu suala hilo na kugundua kuwa nchi 21 zimejiunga na Umoja huo.

Alisema kati ya nchi hizo, zimo pia nchi za Wakristo ambazo zimejiunga na hazijapata madhara yoyote.

``Tumeshakusanya takwimu za nje na kuona hakuna madhara yoyote ya kujiunga na IOC, bora tu kufuata taratibu,`` alisisitiza.

Alisema suala hilo lilileta utata awali kwa sababu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, Bw. Ahmed Hassan Diria, alipeleka ombi la Zanzibar kujiunga kwenye Umoja huo bila kuishirikisha Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo, alisema suala hilo limefanyiwa kazi na serikali na kuona kuwa hakuna madhara kujiunga na IOC.

Akichangia mjadala wa wizara hiyo juzi jioni, Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Bw. Manju Msambya, alisema Tanzania kujiunga na IOC kuna faida nyingi kuliko watu wanavyodhani.

``Kujiunga na IOC kutatupunguzia adha ya kupata bei kubwa ya mafuta,`` alisisiza na kutoa mfano wa nchi za Kiafrika za Guinea, Gabon, Cote de Viore na Msumbiji kuwa zimejiunga na Umoja huo na kupata manufaa makubwa ya kiuchumi.


Haya wapendwa habari ndio hiyo

1 comment:

Anonymous said...

katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti hakuna kitu iki kitokee ktk nchi ya Tz
tunafunga hii roho kbs