Monday, March 31, 2008

Mama Rwakatare na Misukule

Week mbili zilizopita tuliambiwa na watu walioudhuria ibada kanisani kwa mchungaji Rwakatare na hata vyombo vilireport kuwa kuna watoto wawili (Ramadhani na Yusufu) waliodai kuwa ni misukule na kuwa walianguka wakati maombi na ibada ya nguvu ikiendelea kanisani hapo.Mwandishi wetu wa sayuni alikuwepo ibadani hapo na alituletea habari hiyo mchana huo huo wa jumapili.Ila mlima sayuni tulisita kidogo kuzitangaza hapa habari hizo hasa kwa kuzingatia nature ya tukio lenyewe.
Siku chache tangu Mch. Rwakatare atangaze kisa cha watoto hao kudondoshwa na nguvu ya maombi kanisani hapo, jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa kinondoni na mganga (Daktari) mmoja wa kitengo cha magonjwa wa akili muhimbili walisema kuwa watoto hao hawakuwa misukule na ni matapeli wanaojulikana.Polisi walidai kuwa watoto hao wenye umri kati ya miaka 7 na 10 walishawahi kukamatwa kwa utapeli huo na kanisa moja la kipentekoste manzese na walipobainika kuwa walikuwa na njama za kujipatia kipato kwa udanganyifu walipelekwa kituo cha polisi.Kamanda wa polisi mkoa wa kipolis kinondoni ndg Jamal Rwambow, alisema kabla ya kujifanya wameanguka katika kanisa hilo la Mchungaji Rwakatare, hivi karibuni, watoto hao walifanya jambo kama hilo Januari 6, mwaka huu katika eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam.
Watoto hao walidaiwa kuanguka kanisani hapo mikocheni B assemblies of God wakati wakisafiri kwa ungo kutokea mwanza kuelekea mtwara.Na kwamba wao makazi yao ni makaburi ya kindondoni jijini Dar wanapofukua makaburi na kula nyama za watu.
Kisa hiki kimezua mjadala mpya kuhusu maombi ya kuombea misukule hapa nchini.
Sisi kama wanasayuni tunasema kuwa
1.Iwe kwa njia yoyote ile injili lazima itahubiriwa kila mahali ili iwe ushuhuda kwa watu wote na hapo huo mwisho ndipo utakapo kuja.Biblia inasema iwe kwa hila au kwa ukweli injili inahubiriwa.
2.Ni ushauri wetu kuwa ni vyema tuwe makini na roho zidanganyazo makanisani ili kuepuka kuutia aibu mwili wa Kristo.
3.Tunamuheshimu Mch. Rwakatare kama mtumishi wa Mungu na tunatambua mchango wake kwenye jamii yetu.Tunaomba wakristo wawe wanajifunza Biblia kwa umakini zaidi ili wasitumbukie kwenye mitego ya shetani.
4.Ni vyema wakristo tujue kuwa sisi sote ni mwili wa Kristo na shetani amefurahi sana kusikia habari hii na hata kusema kuwa "kiko wapi sasa...tulisema ninyi ni wasanii"...sasa naomba ndugu zangu wapendwa katika Bwana tuwe tunapima mambo maana wakati mwingine shetani anaweza kuleta jambo hili kwa mtindo huu kumbe akawa na lengo la kutuchafua wakrsito wa kweli.
5.Ni vyema tusisahau kuwa shetani ni baba wa uongo tena kweli haipo ndani yake.Kama watoto wale walienda kanisani na kudai kuwa wameanguka kwa nguvu ya maombi..kanisa likawaamini...then wakaenda hospitali na kukiri kuwa walidanganya habari ya kuanguka kwao na pia jamii ikawaamini....je tunaweza vipi kuthibitisha habari wanayoidai sasa kuwa walidanganya nayo ni ya ukweli...?
NB: Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa ya akili hospitali ya muhimbili akihojiwa na ITV alidai kuwa watoto hao wanaugua ugonjwa unaitwa saikosis ambao humfanya mtu kutunga habari na kuifanya kuwa ya kweli hata kama ni uongo...Sasa cha kujiuliza hapa ni kuwa bado tuendelee kuamini habari hii ya wagonjwa hawa wa saikosisi?
Mwandishi wetu wa mlima sayuni alituambia kuwa watoto hao waliletwa kanisani hapo wakiwa na mavumbi mwilini na michubuko sehemu sehemu inayodaiwa ilitokana na kuanguka kwao na kujeruhiwa na kuwafanya watu wengi waamini habari hiyo..

Mungu atusaidie katika kutafakari jambo hili.

Friday, March 28, 2008

From The Voice of the Martyrs

Prayers for March 25, 2008
Baptist Pastor Released from Prison " VOM SourcesOn March 19,
Baptist Pastor Zaur Balaev was released from prison in Azerbaijan, under a presidential amnesty on Novruz Bairam, a holiday marking the beginning of spring. The Voice of the Martyrs contacts reported Pastor Balaev was met by his son and Ilya Zenchenko, head of the Baptist Union. "When Balaev was released, journalists asked whether he was feeling grateful to Azerbaijan's president for his release. Zaur answered that he always in everything feels grateful to Jesus only and no one else. Journalists immediately quit shooting (footage) of him," VOM contacts said. The Voice of the Martyrs rejoices with Pastor Balaev and his family on his release. We encourage you to continue praying for their protection and wisdom as he returns home to his family and congregation. Ask God to give him discernment and favor. Isaiah 54:17

WITO wa kuombea mapenzi ya Mungu katika siasa na uongozi Tanzania

“Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.” (1Timotheo 2:1-6) “Nami Nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana Mungu” (Ezekiel
22:30,31).

Bwana Yesu asifiwe wapendwa!
Tunamshukuru sana Mungu kwa neema na rehema zake katika nchi yetu na pia tunamshukuru kwa ajili ya blog hii,tunaamini yapo makusudi yake hapa.
Ndugu zangu, Mungu ameweka ndani ya moyo wangu haja/mzigo wa kuomba kwa ajili ya nchi hii,hasa kwenye maeneo yanayohusu siasa na uongozi wa serikali yetu. Lakini pia nimegundua na kumshukuru Mungu kuwa ameweka mzigo kama huu kwa watu wengine wengi pia,namshukuru Mungu kwa hilo.
Tumekusudia kuanziasha mtandao wa watanzania walio ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya kushika zamu zetu kumwomba Mungu kwa ajili ya nchi hii.Tumekusudia kuuita Tanzania Prayer Network (TNP) (*Bado tunakaribisha maoni kuhusu hili jina).Mtandao huu utakuwa na majukumu yafuatayo;
a) Kuomba toba kila siku kwa ajili ya maovu yafanyikayo nchini kwetu hasa na viongozi na wanasiasa.
b) Kuwaombea viongozi wa serikali na wa vyama vya siasa kila siku ili Mungu awasaidie.
c) Kuchukua hatua ya kuwashauri viongozi wa serikali na siasa juu ya mambo muhimu katika nchi yetu.
d) Kuchukua jukumu la kuingia katika uongozi wan nchi hii kwa wale wenye upako huo.
e) Kuchukua jukumu la kuonyesha mfano bora kwa viongozi pale tulipo.

Majukumu mengine tutaendelea kufahamishana.
Tunawakaribisha na kuwasihi “wapendwa” watanzania popote walipo tuungane kwa ajili ya hili.
Kama upo tayari kwa ajili ya hili, basi tutumie email yenye maelezo yako kama Jina,Mahali unapoishi,Kanisa unalosali,mtazamo wako juu ya hili n.k ,Tuma email hiyo kwa;

savedlema@yahoo.com -Tanzania,
chalujohn@yahoo.com -Brother Chalukulu,Norway,
hkalenga@mirarco.org -Brother Kalenge,Canada

Tuache kulalamika,tushike zamu zetu kuomba.Karibuni.
Mungu awajaze nguvu zake.


I'M TIRED! :Man

A man was sick and tired of going to work every day while his wife stayed home.He wanted her to see what he went through so he prayed:
"Dear Lord: I go to work every day and put in 8 hours while my wife merely stays at home. I want her to know what I go through, so please allow her body to switch with mine for a day. Amen." God, in his infinite wisdom, granted the man's wish..

The next morning, sure enough, the man awoke as a woman. - He arose, cooked breakfast for his mate, Awakened the kids, Set out their school clothes, Fed them breakfast, Packed their lunches, Drove them to school, Came home and Picked up the dry cleaning, Took it to the cleaners and Stopped at the bank to make a deposit, Went grocery shopping, then drove home to put away the groceries, Paid the bills and balanced the check book. He cleaned the cat's litter box and bathed the dog. Then it was already 1P.M. And he hurried to make the beds, Do the laundry, vacuum, dust, and sweep and Mop the kitchen floor. Ran to the school to pick up the kids and Got into an argument with them on the way home. Set out milk and cookies and Got the kids organized to do their homework, Then set up the ironing board and Watched TV while he did the ironing. At 4:30 he began peeling potatoes and Washing vegetables for salad, Breaded the pork chops and Snapped fresh beans for supper. After supper, he cleaned the kitchen, Ran the dishwasher, Folded laundry, Bathed the kids, and put them to bed. At 9 P.M. He was exhausted and, though his daily chores weren't finished, He went to bed where he was expected to make love, which he managed to get through without complaint. The next morning, he awoke and immediately knelt by the bed and said: -"Lord, I don't know what I was thinking. I was so wrong to envy my Wife's' being able to stay home all day. Please, oh! Oh! Please, let us Trade back." The Lord, in his infinite wisdom, replied: "My son, I feel you have learned your lesson and I will be happy to change things back to the way they were. You'll just have to wait nine months though. You got pregnant last night." ------------ ---------
May the God's unending wisdom guide all Sayuni visitors.

Thursday, March 27, 2008

AHSANTE YESU KWANI ZAMA ZA NUHU HAZITARUDI KAMWE!!!

Jana Dar Es Salaam palikuwa ni hekaheka baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mitaa kadhaa kujawa na maji na baadhi ya barabara kufungwa kwa muda. Wako waliochelewa kufika majumbani kwa takribani masaa manne hadi matano kisa ni mafuriko yaliyosababishwa na mvua hizo. Ashukuriwe Mungu kwamba mpaka sasa hakuna taarifa za vifo wala majeruhi kutokana na mvua hizo japo wakazi wa mabondeni ndo wahanga wakubwa wa mvua hizo!!!!! '

Picha hapa chini zinajieleza zenyewe!!




Picha hizi ni kutoka mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam!

JESUS: IDENTITY THEFT VICTIM



"Behold, many will come in My name..."

Wednesday, March 26, 2008

Maji ya Baridi!



“...Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari…” Mwanzo 1:9-10

Kwa wale wapendao maji ya baridi, nadhani taarifa hii itawafaa sana!

Ni kweli inapendeza na ni sahihi kabisa kwa wengi kwamba wakati walapo au mara baada ya kupata mlo kutumia bilauri ya maji. Maji hayana tatizo bali yanapokuwa ya baridi sana hapo ndo penye tatizo.

Maji baridi yaingiapo mwilini hugandisha mafuta ambayo umemaliza kuyala pamoja kwenye chakula. Sambamba na hiyo pia maji baridi hupunguza kasi ya utendaji kazi wa vimeng’enyo mahsusi vya vyakula mwilini. Hii hupunguza kasi ya usagishaji na kufyonzwa kwa virutubisho vilivyomo vyakula hivyo kuingia katika chembechembe za mwili. Mafuta hayo yaliyoganda yachanganyikapo na tindikali mwilini humeng’enywa kwa haraka kuliko chakula kingine kigumu ulichokula.

Mafuta yaliyoganda hutengeza utando pembezoni mwa ukuta wa tumbo (intestines). Baadae mafuta hayo huweza kupelekea mtu kupata saratani ya utumbo.

Hivyo kwako mpendwa unayesoma makala hii ni vizuri kuzingatia matumizi ya vitu vya moto au vya uvuguvugu haswa pindi umalizapo kupata mlo. Vitu kama supu au maji ya uvuguvugu ni bora zaidi. Wachina na wajapani ni utamauni wao kula chakula na chai ya moto, sasa sijui na sisi tuige au la!!

Mafuta mengi mwilini pia huweza kupelekea tatizo la mshtuko wa moyo hivyo chukua tahadhari kungali na mapema.

Ni ahadi ya Mungu uishi siku nyingi hapa duniani na kisha uzima wa milele mbinguni na baba !

The more we know the better chance we could survive!!!
Hosea 4:6

Tuesday, March 25, 2008

Did Jesus Died on Friday?

It is not necessary to know the exact day Jesus died in order to be saved; you just need to believe that He died for your sins. Knowing the day of His death is important, but not essential. There have been a few people who have doubted the veracity of the Bible because they assume it teaches that Jesus died on Friday, yet they know the prophecy of Christ, “For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth” (Matt 12:40).
Therefore to say that Jesus arose on the third day is not sufficient, because Jesus said he would be buried for three days and nights. Skeptics take out their hand and start counting the days and nights, and it does not add up correctly. So they throw out the Bible and say it is inaccurate. However, the Bible does not say that Jesus died on Friday, only that he arose on Sunday. Jesus rose early on the first day of the week (Mark 16:9).So where did the tradition of Good Friday start? Well, for the first three centuries Christians did not celebrate the death of Christ on Friday. In fact, they did not even celebrate the resurrection on Sunday. They celebrated the day of the resurrection based on the Jewish Passover, thus resurrection day would fall on different days, depending on the day of the Passover. It wasn’t until the Emperor Constantine fixed the day of Easter on Sunday after the first full moon of spring, which corresponded to the Jewish Passover. After setting Easter on Sunday, the church leaders made an honest mistake by assuming the death of Christ was on Friday.
They came to that conclusion based on the fact that Jesus died before the Sabbath (Saturday was the regular "Sabbath" for the Jews which means "Rest" or no work). Mark 15:42 confirms that Jesus died the day prior to the Sabbath: It was Preparation Day (that is, the day before the Sabbath). They assumed this Sabbath was Saturday and thus they concluded the death of Christ was on Friday. That seemed reasonable enough, since at first counting—Friday, Saturday and Sunday—that makes three days. This assumption was considered fact, and so the tradition of Good Friday began with hardly anyone questioning it. Unfortunately, they forgot to take into account that the Passover itself was also a Sabbath.
The LORD’s Passover begins at twilight on the fourteenth day of the first month. On the fifteenth day of that month the LORD's Feast of Unleavened Bread begins; for seven days you must eat bread made without yeast. On the first day hold a sacred assembly and do no regular work. (Lev 23:5-7, emphasis added) As you can see, on Passover no one was allowed to do regular work, which makes “Passover” a “Sabbath”. Since Jesus specifically declared that he would be in the heart of the earth for three days and nights, there is only one day that Jesus could have died to make three days and nights, and it is Thursday, and as we shall see, the Bible actually points to this day.What about Wednesday?Nearly every article that disputes Friday as the day of Christ death, will then argue that Jesus died on Wednesday. The reason they do so is in their view the three days and nights must be at least 72 hours. However, there is no prophecy of scripture that says after 72 hours Jesus would rise again. It was common practice in those days, as well as today, to consider any “part” of the day to be “a day”.
For example you say you spent the day with someone. It does not mean you arrived before the sun rose and left as the sun set. No! That is silly. To spend the day with someone doesn’t imply you spent 12 hours with them. It just means you spent “part” of the day, which you consider to be “a day”. This is how days and nights were treated in the Bible. So long as Jesus spent part of the day or part of the night in the tomb it is considered a day and night.

If Jesus died on Wednesday, he would have been in the tomb for four days and four nights. This would contradict scripture, plus it would pose another real problem for those who believe Jesus died on Wednesday. Here is the big problem?The scriptures tell us that the women prepared spices to anoint Jesus’ body on Sunday.
On the first day of the week, very early in the morning, the women took the spices they had prepared and went to the tomb (Luke 24:1). They could not do it earlier because they had to rest on the regular Saturday Sabbath. If Jesus had died on Wednesday, the Passover would have been on Thursday, however, the next day would be Friday, and there would have been no Sabbath on this day. They could have anointed Jesus body on Friday. So if that was the case, why did they wait until Sunday to do it, when Friday would have been a much better day? Do you see the problem with this view?Some in order to justify this sloppy conclusion argue that it took the women a full day to buy and prepare the spices, and by the time they were done, it was Saturday again and thus the regular Sabbath began. This argument is really stretching one’s rationality.
There is no way it would take more than 24 hours to buy and prepare the spices, for the Jews always buried their dead within one day, so they were accustomed to preparing spices for the deceased within a day. Besides that if they had waited 72 hours before coming to the tomb then decomposition would have begun and according to scriptures this could not have happened. Because you will not abandon me to the grave, nor will you let your Holy One see decay (see Acts 2:27). God promised the resurrection before decomposition. You might remember that Lazarus had already been in the tomb for four days (John 11:17). Decomposition had begun for Martha, his sister, said, “By this time there is a bad odor, for he has been there four days.” (John 11:39)In the end, I see three major problems to the theory of Wednesday being the day of Jesus death:1. If Jesus died on Wednesday, then Jesus would have been in the tomb for four days and four nights.2. If Jesus died on Wednesday, then the women would have gone to the tomb on Friday.3. If Jesus died on Wednesday, then more than 72 hours would have elapsed which would have caused Jesus body to “see decay”.
Thursday is the Day


I believe Thursday was the day of His death; let us clarify when a day ended and when it began. According to the Jews the day was over when the sun had set. We can see in Genesis that a day begins in the evening. And there was evening, and there was morning — the first day (Gen 1:5). It is hard for us to comprehend that evening comes before morning but in order to count three days and nights, you have to begin a day with the evening, or otherwise you will come up with 4 days and 3 nights. It is clear this is how the days were counted in biblical times, for remember, Jesus died somewhere near 3 p.m. and His body needed to be taken down from the cross and put in the tomb before the sun had set. The problem theologians have had on pinpointing the day of His death stems from not taking into account the fact that the Passover was a “special” Sabbath, not the ordinary one which always landed on Saturday. John in his gospel mentions this point, “Now it was the day of Preparation, and the next day was to be a special Sabbath” (John 19:31).John calls this Sabbath a special one. Since it was a “special Sabbath” not the ordinary one, there is no requirement on our part to say that the Passover landed on a Saturday. The “date” of the Passover was always fixed; it was the fourteenth day of their first month (see Leviticus 23:5-6 and Exodus 12:6). Prior to Christ, the Jewish calendar consisted of twelve months at 28 days for each month. So this meant that the Passover would always land on the same day, however, the Jews left that calendar and adopted a 29 to 30 day a month calendar. This was the calendar used during Jesus era; therefore the Passover was a “floating day”, which means it could land on any “day” of the week.


For example, Christmas is a floating day, it is always on the 25th day of December, and so it can float and land on any day of the week. This was the case of the Passover. It is my belief that the Passover landed on a Friday the year Jesus died. This would provide us the three days and three nights we need to fulfill scripture and explain why the women had to wait until two Sabbaths had passed to anoint the body. So with that said, is there any other biblical evidence we can unearth which could shed light on the death of Christ taking place on Thursday? There is one other passage which proves the Passover landed on Friday of that year: Six days before the Passover, Jesus arrived at Bethany, where Lazarus lived, whom Jesus had raised from the dead (John 12:1). Jesus arrived at the home of Mary on the ordinary Sabbath and it was there that Mary poured perfume on Jesus feet. A few scriptures later, the Bible says, “The next day the great crowd that had come for the Feast heard that Jesus was on his way to Jerusalem. They took palm branches…” (John 12:12-13). Historically and traditionally this is Palm Sunday. Notice carefully the previous day when Mary poured perfume on Jesus feet the gospel writer says that this day was Six days before the Passover.
Did you get it? Count six days from Saturday, and there you have it! Passover landed on a Friday.


The death of Christ was on Thursday afternoon and His resurrection was on Sunday before the sun had risen. Early on the first day of the week, while it was still dark, Mary Magdalene went to the tomb and saw that the stone had been removed from the entrance (John 20:1). This passage clearly shows that Jesus rose on Sunday while it was still dark. This is significant because to get an even 3 days and 3 nights, Jesus had to die before the sunset and resurrect before sunrise.Keep Good FridayI am not advocating to depose Good Friday as a remembrance of the death of Christ, just like I’m not advocating getting rid of the our calendar because it is off by 4 or 6 years from the birth of Christ.
People make mistakes on counting days and years, and I believe the church leaders made a mistake on the day of His death. However I am satisfied at keeping Friday as the holiday, even if I do know the death of Christ was on a Thursday.Our church has a great miracle service on Good Friday, and I’m just glad we have a day to celebrate the atonement of Christ through His death. It is not overly important that we get the day right, so long as we remember His death.

Mungu anaangalia moyo..

Kuna mtu nilimsikia leo asubuhi pale mwenge kituoni akilalamika kuwa jana alienda kusali kanisa flani lipo karibu na maeno hayo na kukuta wanawake waliokoka wamejichubua sana na mavazi yao yalikuwa yanamtamanisha sana kiasi kwamba akashindwa kufuatilia ibada vizuri.

Eti wapendwa hii imekaaje...maana kuna wanaosema Mungu anaangalia moyo na wengine wanasema tusienende kama mataifa wafanyavyo..









Picha kwa hisani ya Strictly gospel

Siionei haya injili..maana ni uweza wa Mungu...




Baadhi ya vijana wadogo wengi wao wakiwa chini ya umri wa miaka 20 ("under 20") wakimuhubiri YESU kwa wapita njia na watu wengi pale kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam.
Hiyo ilikuwa ni jana jamatatu ya pasaka nilipowakuta vijana hao wakipiga injili iliyojaa uweza wa ajabu.Binti huyo alikuwa akihubiri huku kila mtu akiwa ametulia kimya kama amemwagiwa maji ya baridi na kusikiliza neno lililojaa munyu kutoka katika kinywa cha binti huyu mdogo.
Naomba kuuliza wana sayuni...Hivi injili ya Yona bado inanafasi katika siku zetu kama ilivyokuwa miaka ile ya mwanzo ya themanini au ndio hivyo tena...?

Mwalimu Christopher Mwakasege

Nilibahatika kuhudhuria semina ya mwalimu huyu.Kwa kweli ilikuwa imejaza watu wengi kupita kiasi pale katika viwanja vya biafra kinondoni hapa jijini Dar es Salaam.

Wakati wa kutoka jioni magari yalikuwa mengi sana kiasi cha kusababisha msongamano mkubwa wa magari maeneo hayo.











Baadhi ya washiriki wa semina ya mwalimu Mwakasege iliyokwisha last week hapo kinondoni viwanja vya biafra wakinunua kanda za mafundisho ya mwalimu huyo kwa wingi.

Uamsho wa kiroho Mtwara

Nimekuwa Mtwara mara kadhaa lakini ni hivi majuzi nimetoka huko tena.Nilifanikiwa kutembelea makanisa machache ya kiroho huko.

Nimefurahishwa sana na uamsho mkubwa wa kiroho unaoukumba mji huo mdogo ulio kusini mwa Tanzania.

Makanisa mengi yamechupua huko na watu wameingiwa na uamsho wa ajabu kumpenda Mungu.



Pengine hii inaweza kusabishwa na makampuni makubwa ya uwekezaji yanayokimbilia mtwara kwani kuna mradi mkubwa wa kiserikali wa kuendeleza so called "Mtwara corrido" (sijui kama nimepatia kiingereza).


Makampuni kama Artumas yameleta wafanyakazi wengi sana na mzunguko wa pesa kwa kweli ni mkuwa.

Artumas ndio wanaochimba gas inayopatikana huko mnazi bay na inaaminika gas na mafuta yaliyopo maeneo ya mikoa ya kusini inaweza kuchukua hata miaka 500 kuja kuimaliza.
Kweli Mungu ameibariki Tanzania.






Haya shime kwa wale mitume,manabii,wachungaji,wainjilisti na waalimu opportunity ya uwekezaji kiroho ipo tele huko,twendeni jamani maana huko kuna "maji tele"





Maelezo ya picha.


Picha ya kwanza:

Bango la Kanisa la International Evengelism Church (AGAPE).

Picha ya pili:

Hapo ni baadhi wa washirika wa moja ya makanisa yanayochipukia kwa kasi sana Mtwara mjini wakitoka ibadani.

Picha ya tatu:

Kibao cha kanisa la Tanzania Assemblies Of God Mtwara Mjini.(TAG ni moja kati ya makanisa ya kwanza kabisa ya kiroho kufika Mtwara)

Wednesday, March 19, 2008

10 GREAT RULES THAT WILL HELP YOU REMAIN POOR ALL YOUR LIFE

Hello brother and sisters in Christ, if you want to be poor - then implement strongly the following rules,10 GREAT RULES THAT WILL HELP YOU REMAIN POOR ALL YOUR LIFE
1. Never wake up early: Keep stretching and turning in bed until you get too hungry to continue dozing. If there are no bedbugs, why hurry to get up?
2. Never plan how to spend your money: Whenever you get money, start spending it right away and when it is finished, try to count and recall how you spent it.If someone ask you tell them that even God says the birds of the air do not plant or havest yet God feeds them.
3. Don't think of saving until you have real big money: How can you save when you earn so little? Those telling you to save are not sympathetic to your burning needs.Msisumbukie ya kesho.Mle nini mvae nini....
4. Don't engage in activities usually reserved for the "uneducated": How can you, a graduate, engage in petty trade or home-based production? That is for people who never went to school.You are educated banaa..
5. Don't think of starting a business until an angel comes from heaven and gives you capital.How do they expect you to invest before you get millions of shillings? Even though more than half the businesses in your town were started with a few hundred shillings, you as a smart person can only start with millions.Ukiulizwa sema hata Mungu anajua...
6. Complain about everything except your own attitude: Blame the system, the Government and the Banks that refuse to lend you money. They are all bad and do not want you to get rich.
7. Spend more than you earn: To achieve this, buy consumer products in credit and keep borrowing from friends and employer.
8. Compete in dressing: Make sure you wear the latest clothes among all the workers in your office or in your church. Whenever your neighbours buy a new phone, get one that is more expensive. Lazima wakujue wewe ni nani.Nenda na wakati banaa...wenye wivu wajinyonge.
9. Get yourself a nice second- hand car that costs more than three times your gross monthly pay: That will surely keep you in debt long enough to hinder the implementation of any bad plans that could make you accumulate capital.
10. Give your children everything they ask for since you are such a loving parent: They should not struggle for anything because you do not want them to suffer. That way, they will grow up lazy and hence poor enough to ensure they cannot help you in your old age.
If you diligently implement these 10 great rules, you will not fail to invite poverty in great measures to your homestead. That way, all important leaders, from East or West, will spend a lot of hours thinking about you, planning how to uplift your daily expenses above one dollar. Isn't it nice to be the subject of concern of all those leaders and scholars?
Remain blessed...

Tuesday, March 18, 2008

Marriage Software

This is what a guy wrote to our systems analyst (Marriage Software Division):
Dear Systems Analyst, I am desperate for some help! I recently upgraded my program from Girlfriend 7.0 to Wife 1.0 and found that the new program began unexpected Child Processing and also took up a lot of space and valuable resources. This wasn't mentioned in the product brochure. In addition Wife 1.0 installs itself into all other programs and launches during systems initialization and then it monitors all other system activities. Applications such as 'Boys' Night out 2.5' and 'Golf 5.3' no longer run, and crashes the system whenever selected. Attempting to operate selected 'Saturday Rugby 6.3' always fails and 'Saturday Shopping 7.1' runs instead. I cannot seem to keep Wife 1.0 in the background whilst attempting to run any of my favorite applications. Be it online or offline. I am thinking of going back to 'Girlfriend 7.0', but uninstall doesn't work on this program. Can you please help? ....
AND THIS IS WHAT OUR ANALYST SAID:
Dear Customer,
This is a very common problem resulting from a basic misunderstanding of the functions of the Wife 1.0 program. Many customers upgrade from Girlfriend 7.0 to Wife 1.0 thinking that Wife 1.0 is merely a UTILITY AND ENTERTAINMENT PROGRAM. Actually, Wife 1.0 is an OPERATING SYSTEM designed by its Creator to run everything on your current platform. You are unlikely to be able to purge Wife 1.0 and still convert back to Girlfriend 7.0, as Wife 1.0 was not designed to do this and it is impossible to uninstall, delete or purge the program files from the System once it is installed. Some people have tried to install Girlfriend 8.0 or Wife 2.0 but have ended up with even more problems. (See manual under Alimony/Child Support and Solicitors' Fees). Having Wife 1.0 installed, I recommend you keep it Installed and deal with the difficulties as best as you can. When any faults or problems occur, whatever you think has caused them, you must run the......... C:\ APOLOGIZE\ FORGIVE ME.EXE Program and avoid attempting to use the *Esc-Key for it will freeze the entire system. It may be necessary to run C:\ APOLOGIZE\ FORGIVE ME.EXE a number of times, and eventually hope that the operating system will return to normal. Wife 1.0, although a very high maintenance programme, can be very rewarding. To get the most out of it, consider buying additional Software such as 'Flowers 2.0' and 'Chocolates 5.0' or 'HUGS\ KISSES 600.0' or 'TENDERNESS\ UNDERSTANDING 1000.0' or even Eating Out Without the Kids 7.2.1' (if Child processing has already started). DO NOT under any circumstances install 'Secretary 2.1 ' (Short Skirt Version) or 'One Nightstand 3.2' (Any Mood Version), as this is not a supported Application for Wife 1.0 and the system will almost certainly CRASH. BEST WISHES! Yours, Systems Analyst.

Monday, March 17, 2008

TANZANIA KUNA MAMBO!!!

Aibuka na kujiita Mtume!

Mtu anayejiita Mtume, ameibuka mjini hapa na kuwahamasisha wafanyabiashara na wafanyakazi kuchukua fedha zote kweye akaunti zao na kuzitoa sadaka.

Mtu huyo, Damas Mukasa, amekuwa akisema iwapo wafanyabiashara na wafanyakazi watachukua fedha zao zote na kuzifunga akaunti, watabarikiwa zaidi na kufunguliwa milango na baraka za mbinguni.

Alitoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki wakati akihubiri kwenye Kongamano la Mitume na Manabii mjini hapa. Alisema kitendo cha watu kujilimbikizia mali, ni kuukaribisha umaskini.

Aliwataka matajiri wawe na ujasiri wa kufunga akaunti zao au kutoa sadaka na mali zao zenye thamani kwa Mungu. Alielekeza mali hizo zitolewe kwenye makongamano yanayoandaliwa na Mitume hao ili watoaji waweze kuombewa na kubarikiwa.

Alisema ili mtu awe tajiri na kushiriki vyema mema, ni lazima kumtanguliza Mungu kwa mali zake alizonazo kwa kuzitoa kwa watumishi wa Mungu aliowaita ni mitume na manabii.

Aliwahamasisha wenye viwanja kuviuza na chochote walichonacho kukitoa kwa Mungu.

Alisema wapo ambao wamejaza fedha kwenye akauti zao na kuwa wabahiri katika kumtolea Mungu mali zao, matokeo yake wanajikuta wakiandamwa na mikosi mbalimbali ambayo inawafanya kuwa maskini.

Baada ya hapo, mtu huyo akiwa na wenzake watano, alitenga makundi matatu ya wafanyakazi, wafanya biashara na wanafunzi akiwataka wote walio tayari kufunga akaunti zao benki kutoka mbele ili waombewe.

Wafanyabiashara na wafanyakazi takriban 12, walijitokeza mbele na kuahidi kufunga akaunti zao kwa lengo la kumtolea Mungu mali zao.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliokuwa katika mahubiri yake, walimpinga wakidai ni utapeli wa kutumia jina la Mungu ili kujinufaisha.

``Hakuna mafundisho ya Mungu katika Biblia yanayotaka mtu awe maskini, anataka watu wafanye kazi ili wawe na maisha bora... sasa hawa jamaa tunawashangaa wanaposema mtu atoe fedha zake zote kwa Mungu ili abarikiwe,`` alihoji Bi. Aisha Baraka.

Askofu Msaidizi wa Kanisa la Pentekoste, aliyekataa kutaja jina na mahali anapotoa huduma , alisema utoaji wa fedha na kuwashawishi watu wafunge akaunti benki, siyo mafundisho ya Mungu.

Baadhi ya waandishi wa habari waliojiandaa katika mkutano huo kuwahoji Mitume hao juu ya mafundisho yao, walishindwa kutokana na kuwepo ulinzi mkali waliowekewa mitume hao.

Tukio hili limekuja siku chache baada ya Mchungaji mmoja kuibuka mkoani Mara na kuwataka waumini wake kuuza mali zao pamoja na wanafunzi kuacha kwenda shule ili wajiandae kumpokea Yesu atakayekuja mwezi ujao.

SOURCE: Nipashe

Sunday, March 16, 2008

Wakristo muwathamini wafanyakazi wa ndani -Bartomayo hakuwa kipofu

Nawasalimu wote kwa jina la Bwana Yesu!, Serikali hivi karibuni imetoa tamko au agizo la kupandisha mishahara kwa watumishi wa ndani na sekta zingine binafsi.Agizo hili limekuja huku kukiwa na malalamiko mengi sana ya miaka mingi juu ya jinsi gani ndugu hawa wanavyotendewa na moja ya watu wanaowaonea,kuwatukana,kuwafanyisha kazi ngumu,kuwalipa kidogo au kutowalipa kabisa na wengi wa hawa waoneaji ni wakristo, nimetumia neno la wakristo kwa maana ya wale waliojitangaza na kuonekana katika jamii ni wafuasi wa Yesu,pengine kwa lugha yangu ili niwatofautishe na wakristo jina basi hawa watu niwaite waliozaliwa mara ya pili au walokole au waongofu. Mambo na jinsi wanayochukuliwa wafanyakazi wa ndani walokole wengi limewashinda mimi nikiwa na ushahidi niliouona kwa macho yangu achilia mbali kusimuliwa.’’Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu na vyumba vyake kwa udhalimu.Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira wala hampi mshahara wake’’Yeremia 22:13.

Hivi tunafikiri tukitoa pepo na kuhubiri injili na kufanya mambo yote yawapasayo watauwa huku nyumba zetu tukifanya uonevu mkubwa tutapona hukumu? ‘’Nami nitawakaribieni ili kuhukumu nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi,wazinzi,waapao uongo;Na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa,kwa ajili ya mshahara wake’’ Malaki 3:5.Aibu gani hii kuwekwa kundi moja na wachawi na wazinzi, hebu fukiri mchungaji,askofu mshirika? Hivi tunasubiri serikali itueleze kuwa tupandishe mishahara kwa hesabu za serikali huyu mtu inabidi alipwe 65,000 akikatwa kama anaishi kwako itabaki 20,500, wangapi walikuwa wanatoa hiyo? Au je hata hii inatosha? Kama wewe kazini unalipwa NSSF je huyu? Kwa sababu masikini? Kuna mtumishi mmoja alikuwa anasema kwa kutamba , eti namsaidia kwa sababu ana shida! Fikiria huyu mchungaji!

Hivi Farao anatushinda? ‘’Nami nitakulipa mshahara wako’’ Kutoka 2:9, Au Labani aliyeongeza mshahara angalau mara kumi kwa yakobo katika kipindi chote cha ukaaji wake Mwanzo 31:41,Mwanzo 30:28.? .Je leo wakiambiwa nao waanze kufanya kazi kwa kudai masaa ya ziada!

Akina baba tunaweza kujitetea kuwa akina mama ndio wanahusika na wafanya kazi wa ndani, kama,Utetezi uleule wa Adamu baada ya Eva kula tunda, hivi alivyojitetea alipona?.

Nchi zilizoendelea mfanyakazi wa ndani unaogopa kumuajiri kwa sababu ni gharama! Mchango wa wafanyakazi wa ndani ni mkubwa sana katika ujenzi wa familia,kanisa na taifa, ndio sehemu ambayo hali zetu za uchumi na baraka zitakuwa imara endapo unamjali kama binadamu.Imefikia hatua mtu aliyeokoka kuamini kuwa mfanyakazi wa ndani hawezi kuolewa au kuoa msomi!,kuvaa nguo nzuri hata kula pamoja kama ndugu.Tunadanganya watu kuwa hawa ni sehemu ya familia huku hatutekelezi mambo ya muhimu kwao.Namshukuru alinifungua mapema!

Ikumbukwe kuwa, thamani ya mtu haipo katika kuwa na magari,nyumba elimu na mali nyingi, thamani ya mtu iko katika kuonyesha upendo kwa watu wengine pamoja na kuwajali,Wazungu wana tabia ya kupenda wanyama hata kuwalipia bima za matibabu, sembuse kumpenda mwanadamu mwenzao.Mbele za Mungu tuko sawa kabisa, Yesu alitupenda pasipo sababu yoyote iliyomvutia yeye atupende hata akafa kwa ajili yetu. Wakristo tuwe na tabia ya kuwaangalia watu KAMA MUNGU ANAVYOWAANGALIA.Hawa ni watu ambao wengine walileta hata ukombozi kwa mataifa yao na wakuu wao(Ester).Hili wazo langu halitetei kuwa wanaweza kuwa wengi wao wanamatatizo.lakini kabla ya kutupa lawama lazima tuangalie tumewajibika kwa kiasi gani.Kuwajibika huku ni pamoja na kuwaza kuwa ataishi maisha gani baadae kwani hatazeekea kwako!.Usije ukajitetea kipato kidogo, kwanza kama tunaamini sisi sio maskini matendo yetu yaeleze kwani ndio imani.Pili kama unakipato kidogo utaishi kulingana nacho na upendo utuonyesha kulingana na hali yako.

Hivi karibuni kumezuka watanzania watumishi wa ndani kufanya vitu vya kikatili kwa watoto wa mabosi wao, sio lengo la waraka huu kuwatetea, ila ni kuangalia tatizo ni nini?? Huyuhuyu mama anayelalamika housegirl ni mkatili, ndie aliyemchukua kijijini kwa ahadi za kumsomesha, ndiye anayemtenga na hamfanyi huyu mtu kuwa sehemu ya familia, ndiye huyuhuyu hampi mshahara, ndiye huyuhuyu anayemkaripia usiku na mchana wala hakuna alama ya upendo.Hivi hawa watumishi wa ndani wangekuwa nyumbani kwa kwa baba na mama je wangefanya ukatili huo, jibu ni hapana, sasa ni kitu gani kinawafanya wawe makatili?? Kuna jambo ambalo kabla ya kuanza kutoa vibanzi na kuwalaumu tujiangalie tunavyowachukula hawa watu katika jamii.Tunawachulia kama ni watu wa chini, waliodharaulika, hawana akili hawana mbele wala nyuma.Kuna siku nilijiuliza ni kwa nini maaskari wengi wa magetini ni wakali sana, kumbe wengi wanajihisi inferior na wanajidharau kwa sababu jamii inamuona hivyo, hivyo ukali wake ni kukueleza hata ‘’mimi niko’’ .Huyu mfnyakazi wa ndani kisaikolojia akiishaona ametengwa roho ya ukatili inaingia(TUSIMPE NAFASI SHETANI).
Lakini kwa walokole ni sehemu nyingine ya kujadili kwa upana sana kiasi ambacho wengi ulokole wao ni wa makanisani sio wanavyoonyesha na kuwatendea watu hawa wa ndani.Pia hata kujadili swala lenyewe ni uthibitisho tosha kuwa tumeweka matabaka katika jamii!!!

Naomba mlokole aniambie kama kweli ni nani aliyekuwa anampa mshahara mzuri mfanyakazi wake wa ndani kiasi kikubwa angalau sio kama hiki(maana mshahara wa serikali ni sh.elfu sitini ukikata makato kama ilivyoelekeza net pay unayotakiwa umlipe ni kama 23,000), kama ulishtuka baada ya serikali kutangaza wapandishiwe mishahara,basi macho ya kiroho huna,tena inabidi mtubu.Walokole tuwe wa kwanza na kuwaza mbali sana nje ya upeo wa serikali, maana tuna macho ya kiroho.

Ni walokole wangapi wanaosema nina mfanyakazi wa ndani, naye ni sehemu ya familia, je kama sehemu ya familia umemfikira huyu mtu baada ya miaka mitano ijayo atakuwa wapi?? Kama huna wema wa kufanya hivyo na kuwaza mazuri kwa mtu anayeishi na kuwatunza watoto wako, anakupikia kila siku, je Mungu wetu ansema nini, najua mawazo ninayowawazia ni mawazo ya amani.

Hili pengine ni gumu kulipokea, kama walokole wameweka matabaka, basi hakuna mbingu, Yesu alikaa na watu wa kila aina na kamwe hakumbagua mtua.Wanafunzi wa Yesu walikuwa wanapita njia aliyokuwa anakaa Bartomayo na bado hakuna aliyewaza kumbeba wala kumpeleka kwa Yesu, mbaya zaidi hata siku ambayo Yesu alipita , wakati anaita wakamnyamazisha, akae kimya.KIPOFU HAPA HAKUWA BARTAMAYO WALIKUWA WAFUASI WA YESU, YESU ALIKUJA KWA WATU WA AINA ILE HIYO NDIYO MISHENI YAKE KUBWA!! Watumishi na walikole wengi wamesema Bartomayo alikuwa kipofu kuna mengi hatuyaoni maisha ya kila siku ili yatupe ubora ule ambao Mungu anautaka, hatuyaoni sisi ndio vipofu!! Bartamayo hana shida anaupofu wa mwili.UPOFU WA KIROHO NI MBAYA ZAIDI.

Serikali inaweza na itawabana wale wote wsiotekeleza hili,mlokole haupaswi kufuatiliwa.’’Mambo yale yaliyo mbali na yale yaendayo chini sana ni mtu yupi awezaye kuyatafuta?’’Mhubiri 7:24.

Hivi ndio nionavyo
Kalenge

Saturday, March 15, 2008

"SUPER-MOUSE" with extraordinary physical abilities

What does this signify? Is this not part of the fulfillment of our Lord's prophecy when he was asked by his disciples about the end of the world?

"Tell us, when shall these things be? and what [shall be] the sign of thy coming, and of the end of the world?" Mat. 24:3



Scientists have been astounded by the creation of a genetically modified "supermouse" with extraordinary physical abilities – comparable to the performance of the very best athletes – raising the prospect that the discovery may one day be used to transform people's capacities.
The mouse can run up to six kilometers (3.7 miles) at a speed of 20 meters per minute for five hours or more without stopping. Scientists said that this was equivalent of a man cycling at speed up an Alpine mountain without a break. Although it eats up to 60 per cent more food than an ordinary mouse, the modified mouse does not put on weight. It also lives longer and enjoys an active sex life well into old age – being capable of breeding at three times the normal maximum age.

American scientists who created the mice – they now have a breeding colony of 500 – said that they were stunned by their abilities, especially given that the animals came about as a result of a standard genetic modification to a single metabolism gene shared with humans.

By Steve Connor, Science Editor - The Independent 02 November 2007

Kibwetere Mtanzania aibuka

Serikali mkoani Mara, imevunja kambi ya mchungaji wa kanisa la Wasabato wenye msimamo mkali, linalohubiri kushuka kwa Yesu mwezi ujao, hatua ambayo imewafanya baadhi ya waumini wake kuanza kuuza vitu vyao.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Bw. Saveli Maketta, aliliambia gazeti hili mjini hapa kuwa kambi ya mchungaji huyo, Ephraem Mtabi, iliyokuwa katika kijiji cha Kyagata, wilayani hapa ilivunjwa Machi 12 kwa ushirikianao wa jeshi la polisi.
Bw. Maketta alisema kuwa mchungaji Mtabi, mkazi wa mjini Bunda, awali alikuwa ni muumini wa kanisa la Wasabato halisi, lakini baadaye alijiengua na kuanzisha kanisa lake ambalo lina msimamo mkali. Baadhi ya wananchi wamemfananisha Mtabi na \'Askofu\' Joseph Kibwetere, kiongozi wa Kanisa la Kurejesha Amri 10 za Mungu, ambaye alisababisha waumini wake kujilipua moto nchini Uganda kwa kuamini kwamba mwaka 2000 ulikuwa mwisho wa dunia.
Bw. Maketta alisema alipata habari za kuwepo kwa mchungaji huyo katika wilaya yake, kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, ambaye pia alizipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema wakiwemo walimu wa shule na wanafunzi, ambao pia walijiunga na kanisa hilo na kuacha masomo.
``Mchungaji huyo amekuwa akihatarisha amani katika jamii, kwa kuhubiri hivyo, kwani watu watakaposubiri bila kumuona huyo Yesu, kwa siku walizoambiwa, wanaweza kukata tamaa ya kuishi, na hivyo wanaweza kujiua au hata kumuua yeye mwenyewe... Sasa sisi kama serikali tumeliona hilo na kuchukua hatua ya kuvunja kambi hiyo mara moja,`` alisema.
Aliongeza: ``Kuna madai ya baadhi ya wanafunzi waliojiunga na kanisa lake kuacha masomo. Tumesikia kwamba baadhi yao hawakufanya mitihani yao ikiwemo ya kidato cha nne.``
Alisema alimuagiza ofisa tarafa kufanya uchunguzi na tathmini haraka, ili hatua zichukuliwe.
Alisema katika mahubiri yake mchungaji huyo alisisitiza kwamba Yesu atashuka mwezi Aprili mwaka huu, katika kijiji cha Kyagata na kwamba amekuwa akiwataka watu mbalimbali wakiwemo waumini wa kanisa hilo kujiandaa, ili waweze kupaa na mwokozi huyo.
Imeelezwa kuwa kutokana na mahubiri hayo, watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi walihama makwao na kwenda katika kambi ya mchungaji huyo ili kushirikiana naye katika kuhubiri ujio wa Yesu Kristo, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wengine waweze kujiunga na kanisa hilo na kukaa mkao wa kumsubiri.
Taarifa zinaonyesha kuwa baadhi ya waumini wenzake walikwishauza baadhi ya vitu vyao, kikiwemo chakula na mifugo, ambapo pia wanafunzi wamekataa kusoma kwa madai kuwa hawawezi kusoma wakati ufalme wa mwenyezi Mungu umekwisha kutimia na hivyo wanasubiri kupaa mbinguni. Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Bw. David Saibullu, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mahubiri ya mchungaji huyo yanahatarisha amani na kwamba bila kudhibitiwa mapema, yanaweza kuleta maafa makubwa kama ilivyokwisha kutokea nchini Uganda, ambako waumimi wenye msimamo mkali walijifungia kanisani na kujilipua kwa moto.
Kamanda Saibullu alisema kuwa jeshi la polisi linawashikilia na kuwahoji watu kadhaa, wakiwemo wanafunzi wanne.
Walioshikiliwa ni Edina Joseph na Nimrod Machumu, wanaosoma katika Shule ya Sekondari Lubana ya wilayani Bunda, Eliza Joseph, Shule ya Msingi Migungani, Bunda na Manyama Benabato, Shule ya Msingi Namibu A.
Wengine ni Katibu wa kanisa hilo, Mussa Waitaro, mkazi wa Kyagata, pamoja na wazazi wawili wa wanafunzi hao, ambao ni Joyce Paul na Nyanjura Machumu, wote wakazi wa wilayani Bunda.
Kamanda Saibullu, alisema kuwa Mchungaji wa kanisa hilo kwa sasa yuko safarini mkoani Tabora, ambako inadaiwa kuwa amekwenda kuhamasisha watu wengine waweze kujiunga na kanisa lake.
SOURCE: Nipashe

Thursday, March 13, 2008

Huduma ya kitume na kinabii


Apostle Dastun Maboya wa Calvarry Assemblies of God




Kuna kipindi huduma hii ilionekana kwa wapentecoste wengi kama kituko.Nakumbuka miaka ya 80 na mwanzo kabisa wa 90's nilikuwa nasikia sana karama ya unabii kwenye makanisa mengi yaliyokuwepo wakati huo.
Kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90 Mtume Dastani Maboya ndio ninayemkumbuka kuwa ni mtu wa kwanza kabisa kujitambulisha kama Mtume.,kipindi hicho alitambulika kama apostle Dustan Maboya.
Kuanzia miaka ya katikati ya 90 na hadi sasa tumesikia watumishi wengi wakijitambulisha kama mitume na manabii.

Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Efatha Ministries
Hata wale ambao tulikuwa tukiwatambua kama wachungaji kwa miaka mingi nao sasa wanatambulika kama mitume/manabii au vyote kwa pamoja.Huduma za kitume na kinabii zimeonekana kuwa na mvuto sana kwa siku za karibuni na kuvutia mamia kwa maelefu ya watu hata wakati mwingine kusababisha wachungaji wa makanisa kongwe ya kipentecoste kulalamika kuwa washirika wanawakimbia na kuhamia huko ambako miujiza na uponyaji ni mambo yanayopewa umuhimu mkubwa sana.

Swali kwa wapendwa...;Kama YESU alitoa wengine kuwa mitume,wengine manabii,wengine wachungaji,wengine wainjilisti na wengine waalimu...Je Huduma hizi zinatumika vile ipasavyo? Ni kweli kuwa zinapewa umuhimu ule ule unatakikana kibiblia?
Ni kweli kuwa huduma za kitume na kinabii zinazipa nafasi ya kutosha huduma kama uchungaji,uinjilisti na ualimu kwa maana yake?
Ni kweli kuwa makanisa kongwe ya kipentecoste yanazipata nafasi huduma na kitume na kinabii kama ofisi na kama yanavyozipa nafasi huduma za kichungaji, kiinjilisti na kinabii?
Mheshimiwa Nabii Joedavie wa Ngurumo ya Upako











Mtume Vernon Fernandez wa Agape Ministry (ATN)

Wafanyikazi wa ndani! (HOUSE GIRLS)!

Nimesikia habari na matukio mbalimbali yahusianayo
na wafanya kazi wetu wa ndani majumbani! Kwa mfano matukio ya hivi karibuni Mfanyi kazi mmoja alimuua kwa kumuweka mtoto kwenye oven kisha kumuoka kama mkate, mwingine alimsokomeza matambara mdomoni na hivi karibuni tukio la ndugu yangu mpendwa (jina kapuni) mtoto wake alinyweshwa mafuta ya taa kwa nia ya kumtoa roho. Ashukuriwe Mungu kwamba alimnusuru maisha yake. Baadae huyu house girl aligundulika kuwa na mapepo ndani yake. Wengine wamediriki hata kusema kwamba ma-housegirl hao ni kama tumewafanya kuwa watumwa kwa kazi wazifanyazo majumbani mwetu, sina uhakika kama ni wote. Swali la msingi ni hili, Je ni kweli kwa zama za leo zenye DayCare nyingi na nyumba za kutunzia watoto japo si za kiwango cha juu twahitaji wafanyi kazi wa jinsi hiyo?

Kwa Housegirl wakati mwenye nyumba yuko kazini, shuleni, biasharani au mihangaiko mingine yeye:
1. Anakula na kunywa vizuri anachotaka awapo nyumbani kuliko wewe

2. Ndo mwenye kuangalia TV yako nzuri na mikanda mizuri ya Video kwa muda mrefu kuliko wewe. Kama ni nyimbo ni yeye azijuaye na hata hufikia kipindi cha yeye kukuhadithia

3. Kama ni viti vyako vya bei mbaya yeye ndo anavikalia kwa muda mrefu

4. Ana muda mwingi wa kupumzika mchana kuliko hata wewe

5. Akiugua wewe ndo unamtibu tena kwa gharama kubwa

6. Wakati wa safari lazima umkatie tiketi na uhakikishe kasafiri salama wakati wewe hujihangaikia mwenyewe

7. Hana shida ya kupanga bajeti ya nyumba (Haumizi kichwa) na wala hatafuti pesa

8. Christmas na sherehe nyingine, lazima nae umtoe kwa kivazi kizuri

9. Umempa dhamana ya kulea na kufundisha watoto wako chochote atakacho kwa muda mrefu kuliko wewe

10. Ndiye mwenye kuijua nyumba yako na kona zake pengine kuliko hata wewe

11. Lazima umpe mshahara wake wa mwisho wa mwezi ambao yumkini ni nusu ya wako (60,000/- Tshs.)
12. Mengine ongeza wewe!!!!

Ni kweli nae huweza kukusaidia kufanya baadhi ya mambo hapo nyumbani lakini kwa faida hizo ambazo kwako mwenye nyumba ni aghalabu kuwa nazo, ni halali kuwa na mfanya kazi wa namna hii kwa siku za leo Au ni kujirudisha nyuma kimaendeleo??

Ndugu msomaji hebu kong'oli mahala palipoandikwa comments na utoe mtazamo wako!

Wednesday, March 12, 2008

Mtoto umleavyo...!

Biblia inasema mfundishe mtoto katika njia impasayo, naye hataicha hata atakapokuwa mkubwa.

Ni jukumu letu wazazi kuwafundisha watoto maadili mema.

Mtu huwa hazaliwi na tabia mbaya ila tabia ( characters) huumbwa.Hakuna mtu anayekuja duniani akiwa mtenda dhambi ila mtu huwa anafanywa vile alivyo.

Monday, March 10, 2008

Our God reigns in deed and in truth

A Muslim man in Egypt killed his wife because she was reading the Bible and then buried her with their infant baby and 8-year old daughter. The girls were buried alive! He then reported to the police that an uncle killed the kids. 15 days later, another family member died. When they went to bury him, they found the 2 little girls under the sand - ALIVE! The country is outraged over the incident, and the man will be executed. The older girl was asked how she had survived. 'A man wearing shiny white clothes, with bleeding wounds in his hands, came every day to feed us. He woke up my mom so she could nurse my sister,' she said. She was interviewed on Egyptian national TV, by availed Muslim woman news anchor. She said on public TV, 'This was none other than Jesus, because nobody else does things like this!' Muslims believe Isa (Jesus) would do this, but the wounds mean He really was crucified, and it's clear also that He is alive! But, it's also clear that the child could not make up a story like this, and there is no way these children could have survived without a true miracle. Muslim leaders are going to have a hard time to figure out what to do with this, and the popularity of the Passion movie doesn't help! With Egypt at the centre of the media and education in the Middle East , you can be sure this story will spread. Jesus Christ is still turning the world upside down! Please let this story be shared. The Lord says, 'I will bless the person who puts his trust in me. 'Jeremiah 17

Toba ya kweli....True repentance......

Jimmy Swaggart

During the 1970s, Swaggart was ordained by and established a ministry under the Assemblies of God. It was at this time that Swaggart decided to use television as his primary preaching medium, and by 1980, he had become the most popular television preacher in the United States. Upwards of 200 television stations broadcast his program; “The Jimmy Swaggart Telecast” was regularly watched by two-million households. Jimmy Swaggart Ministries, at this time headquartered in Baton Rouge, Louisiana, grew to include a local congregation at the Family Worship Center of more than four-thousand members, a printing and mailing production plant, a television production facility, a recording studio, and later a Bible college in 1984. The college had been formerly named Jimmy Swaggart Bible College ("JSBC"). Presently, it is renamed as the World Evangelism Bible College & Seminary. The Seminary opened in the fall of 1988.

In 1986, Swaggart exposed fellow Assemblies of God minister Marvin Gorman, who was having an affair with one of his parishioners. The following year, Swaggart exposed televangelist Jim Bakker's sexual indiscretions and appeared on the Larry King Show, stating that Bakker was a "cancer in the body of Christ." As a retaliatory move, Marvin Gorman hired a private-detective to follow Swaggart. The detective found Swaggart in a Louisiana motel on Airline Highway with a prostitute, Debra Murphree, and took pictures of the tryst. Gorman presented Swaggart with the photos in a blackmail attempt to force Swaggart to come clean, but Swaggart refused. Gorman then presented the pictures to the presbytery leadership of the Assemblies of God, which decided that Swaggart should be suspended from broadcasting his television program for three months.
On February 21, 1988, without giving the details of his transgressions, Swaggart tearfully spoke to his family, congregation, and audience, saying, "I have sinned against you, my Lord, and I would ask that your precious blood would wash and cleanse every stain until it is in the seas of God's forgiveness."(On a New Orleans morning news show four days later, Murphree stated that while Swaggart was a regular customer, they had never engaged in intercourse.)
Against the ruling of the governing body of the Assemblies of God, Swaggart returned to his television pulpit long before his three-month suspension expired. He stated, "If I do not return to the pulpit this weekend, millions of people will go to hell." Believing that Swaggart was not genuinely repentant in not submitting to their authority, the Assemblies of God immediately defrocked Swaggart, removing his credentials and ministerial license.
On October 11, 1991, Swaggart was found in the company of another prostitute, Rosemary Garcia,when the pair was pulled over by the California Highway Patrol in Indio, California, for driving on the wrong side of the street. According to Garcia, Swaggart stopped to proposition her on the side of the road. When the patrolman asked Garcia why she was with Swaggart, she replied, "He asked me for sex. I mean, that's why he stopped me. That's what I do. I'm a prostitute." Rather than confessing to his congregation, Swaggart told his flock this time that "The Lord told me it's flat none of your business." His son Donnie then announced to the stunned audience that his father would be temporarily stepping down as head of Jimmy Swaggart Ministries for "a time of healing and counseling."

Following the scandals, Swaggart's ministry had been reduced by 85% as of 1995. While his ministry's annual revenue shrunk, his annual salary was still over $350,000 at that time.

Mkoa wa mbeya

Mkoa wa mbeya ndio unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya makanisa au madhehebu karibu kila kona ya mji(hii ni kwa takwimu zangu na sio rasmi).Ni mkoa uliobarikiwa kwa mambo mengi.Kuanzia vyakula vya kila aina, hali nzuri ya hewa, uchumi mzuri na kadhalika.Pia Mbeya inaongoza kwa kutoa wanasiasa na wasomi mashuhuri hapa nchini kama akina Prof. David Mwakyusa,Pro. Mark Mwandosya,Dr. Harison Mwakyembe na wengineo wengi.Mbeya imetoa watumishi wakubwa mashuhuri wa Mungu kama Bishop Ranuel Mwenisongole,Pastor Mwanjala,Mwalimu Christopher Mwakasege na wengine wengi sana tunawaojua wanatokea mbeya.Kwa idadi ya watumishi wa Mungu kuna idadi kubwa sana ya watumishi wanaotokea mbeya.
Inasemekana kuwa mbeya ni miongoni mwa mikoa michache ilioyokuwa ya kwanza kabisa hapa nchini kupokea ukristo ( sina uhakika na hili).

Cha kusikitisha ni kwamba, Mbeya ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa hivi sasa kwa mauaji ya kutisha ya kikatili kabisa ambayo hayaelezeki.Mara nyingi tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa watu wamechunwa ngozi, maalbino kuuwawa kinyama na ujambazi wa kutisha.Mara nyingi matukio haya yamekuwa yakiunganishwa na vitendo vya kishirikina.Mbeya ni miongoni mwa miji ambayo huwezi kutembea usiku peke yako na amani hata kidogo kwani huwezi jua wachuna ngozi watatokea wapi muda huo.

Mbeya ni mmoja kati ya mikoa inayoongoza kwa idadi kubwa sana kwa maambukizi ya ukimwi.Ngono imekuwa ni kitu cha kawaida sana mkoani humo kiasi kwamba hata night clubs na casinos kama Mbeya Carnival vimeanzishwa na vimekuwa vikipata wateja wengi kupita kiasi.

Jamani wakazi na wenyeji wa mkoa wa Mbeya, wakati umefika sasa amkeni, mjifunge magunia muingie katika toba ya kuuombea mkoa wenu kwani shetani amawakamatia pabaya.

Biblia inasema katika 2Nyakati 7:14 "..ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu...watajinyenyekeza kwa kutubu makosa yao ..na kuacha njia zao mbaya...nitaiponya nchi yao na kuwasamehe makosa yao..."

Sunday, March 9, 2008

Bishop George Gichana

Unamkumbuka Mwinjilisti huyu?
Kwa sasa anatambulika kama Bishop George Gichana(GG),anachunga kanisa lake kule Eldoret Kenya.
Kwa hapa nyumbani Tanzania si mgeni sana kwa watu wengi waliokuwa wanahudhuria mikutano maarufu ya the Big November Crusade iliyokuwa inafanyika viwanja vya jangwani mjini Dar es Salaam.
Namkumbuka muhubiri huyu kwa mara ya Kwanza nilimwona pale viwanja vya mnazi mmoja mwaka 1986 wakati the Big November inaanza kabla haijahamia viwanja vya Jangwani.Namkumbuka mtu mmoja anaitwa Salvatory aliponywa kimiujiza kabisa wakati muhubiri huyu anayependa kuitwa GG(tamka jiijii) alipokuwa anaombea watu na kuhubiri injili ya upako na nguvu nyingi.Siku hiyo Salvatory alikuja akiwa amebebwa kwenye machela akiwa mahututi kabisa hawezi chochote akitokea muhimbili na kulikuwa na wagonjwa wengi wameletwa kutoka muhimbili na manesi wengi na magari ya wagonjwa yalikuwa mengi.Mara Salvatory akasimama baada ya maombi na akaanza kutembea mwenyewe kwa kasi ya ajabu akitokea kule nyumba alikokuwa amelezwa na kuja mbele kwa furaha akimshukuru YESU KRISTO wa nazareth kwa kumponya.
Huu ni moja kati ya miujiza ambayo nimewahi kuishuhudia kwa macho ya nyama akitokea live kabisa bila kuwa na maswali maswali yoyote.
Kwa anayejua habari za Salvatory alipo kwa sasa atuambie.
Kwa kweli the Big November miaka ile ilikuwa ya nguvu sana.Nakumbuka miaka iliyofuata watu kama akina Roy Durman na wengine wengi walianza kuja na Dar es Salaam kuliwaka moto kila mwaka.
Hata hivyo hivi sasa the big November imepoteza ule umaarufu wake iliokuwa nao miaka ile na msisimko wa miaka ile.


Mungu atusaidie.

Saturday, March 8, 2008

Viongozi wa kanisa muda umefika amkeni!

Lengo na dhumuni la nakala hii ni kusupport mawazo ya ndugu Lema ambaye ameandika nakala ya iliyotangulia;

Unajua kwa nini viongozi wetu wa dini wako kimya? Wako kimya kwa sababu hawatoki tena mbinguni.Wanatoka duniani.Wanaitegemea serikali badala ya serikali kuwategemea wao ,''tumepewa mamlaka'' inaishia madhabahuni

Nimefundishwa kanisani na nimeelewa uhusiano uliopo kati ya Kristo na Kanisa, achilia mbali kufundishwa kwenye mafundisho ya ndoa kwa undani zaidi, lakini kila mchungaji padri,maaskofu makadinali wanayajua haya, kuwa kanisa ni mfano halisi wa mwanamke!
Linatakiwa liwe na sifa zote za mwanamke, ambazo ni pamoja na utii,upendo,kujali,kukusanya kulinda n.k

Pamoja na kuwa tunaweza kuringa tuna roho mtakatifu hata na kuwa na nguvu za kuhamisha milima,kufufua wafu,katu bila upendo unaoendana na matendo halisi ya wakati na mahali husika karama zetu na kazi zetu ni bure,bila kuwa na moyo,hari na uwezo wa kutetea haki hatufai utumishi wetu tutaulizwa,wapentekoste wangapi wanalea yatima?,maskini?,wajane? n.k, ni aibu ya kuwa pengine wamataifa wametuzidi kwa mbali sana.

Kwa sababu tunajiona tumefika mbinguni,upako tulionano pengine umetupofusha? Nitakataa kumbe penye upako au nguvu za Mungu kuna haki kuna ukweli,kuna ujasiri kama wa Stefano akifa bila kumkana Yesu, Kama tunasema Mungu habadiliki ni yule jana leo na hata Milele,tunaambiwa pia Eliya alikuwa mtu wa kawaida sawa na sisi aliamuru Mvua isinyeshe na ikawa,naam zaidi tunaishi pia katika kipindi ambacho Roho mtakatifu ni dhahiri kwa watu walioamini, wakati zamani nguvu hizo zilikuwa kwa wachache na ndio tunaowasoma hata leo. Wako wapi akina Daniel,Shadrack, Meshack na Abedinego,nimesikia kuna manabii wengi zama hizi , wako wapi akina Yohana mbatizaji ambaye alieleza uovu wa kiongozi serikalini!??????

Watu wanaishi kwa taabu nchi hii, maisha Magumu, rushwa kila mahali,ubadhirifu wa fedha za umma uko dhahiri, haki kupindishwa, uonevu mahali mahali, wakati kuwa Kuna baadhi ya viongozi wa dini wanadai waliomba wakajibiwa na kuwa ni majibu ya Mungu kuwa na viongozi tulionao sasa! Nikaamini zama za viongozi kupakwa mafuta kumbe hata sasa zipo japo si za moja kwa moja ‘indirectly’ .Nikaamini basi watatokea akina Samweli na Nathani enzi za mfalme Sauli na Daudi ambao watakosoa utendaji kazi mbovu, baadhi ya mambo yasioyosahihi ya serikali,vyama,taasisi hata zisizo za kiserikali.Mmekaa kimya kama vile sio viongozi wa kanisa.Yesu ni Mfalme wa wafalme, yuko juu ya serikali na mamlaka zote, Yesu huyo mnae tena kila siku mnawaita watu waje kuombewa magonjwa mbalimbali yakiwemo ukimwi ambao nimeona kwa macho yangu watu wanapona hata kama serikali haitaki tuseme,

Kanisa likae kimya juu ya ununuzi wa rada, ndege ya raisi,matumizi mabaya ye serikali,kunyima haki watu, maisha ya taabu na dhiki wanayoishi watanzania,EPA,RICHMOND,? Kama tunaambiwa tuheshimu mamlaka ni pamoja na kuiambia ukweli, si mamlaka zote zinaheshimiwa kwani sidhani kama Mungu anaweza kuweka mamlaka kama za akina madikteta tunaowajua kama hatukutaka wenyewe!

Kanisa ni dhaifu kwa sababu tuna viongozi wa makanisa dhaifu katika kutambua na kuelewa wajibu wao katika jamii si kiroho tu bali hata kimwili.Yale yaliyo katika uwezo wetu kuyafanya mnatakiwa mfanye kwani ninyi ni miungu(Zaburi 82:6, Yohana 10:34) .

Waumini wenu au washirika wenu, wamesalitiwa vyama vinavyojiita vya upinzani vimewasaliti maana havina mpango wa kuungana pamoja kilammoja anataka chake,baadhi ya wasomi wakiwemo maprofesa wamewasaliti, wengine mmewaona juzi wakitoa maamuzi ya kisiasa wakati wao wasomi, Siasa imeingia kwenye elimu ambayo ni dira ya taifa,kodi wanazotoa waumini wenu na nyie maaskofu zinaharibiwa. Yesu alikasirika siku moja alipoingia hekaluni na kukuta minada inaendelea badala ya neno la Mungu,hekalu la sasa ni mtu.Tumaini la watanzania liwe viongozi wao wa kanisani.

Hawa wasomi, viongozi wa serikalini mafisadi ni waumini wenu na mnachukua sadaka zao! Mambo wanayopitia kizazi cha sasa ndio kinaelezea aina ya viongozi ambao tutakuwa nao baadae, aina ya wachungaji ambao tutakuwa nao baadae, hali ya maisha ya sasa inelezea jinsi ambavyo ni vigumu kwa viongozi wa kanisa kukataza rushwa hapo baadae,mmeona jinsi ambavyo mkuu wa mkoa wa DSM akipiga vita wasichana kujiuza mwili, wameacha au wamebadilisha maeneo?, jamani manabii,mitume,walimu,wainjilisti,wachungaji mko wapi? Au kwa sababu zaka na sadaka vinaletwa tu? Lakini hao waumini wenu watafika mbinguni??? hizo sadaka na zaka zinapatikana kihalali?(Fikiria wewe ni mchungaji wa Lowassa mpaka anapata aibu ile si ni aibu ya kanisa!! wewe mchungaji ulikuwa haujui kuwa ana tatizo, la hata inawezekana kweli ulikuwa haujui kwa jinsi ya kibinadamu, je Roho hakukuambia?? kama hakukuambia basi hauombi! na kama hauombi basi haufai kuwa mchungaji!!! na kama ulijua ukaka kimya dhambi hiyo pia ni yako.Timotheo aliambiwa ONYA, KARIPIA maana mchungaji wa kweli aliyejazwa Roho , hekima na mamlaka viongozi wa serikali wanatetemeka maana sio wewe unayeishi bali ni kristo) kuna mtu atasema mchungaji yule wa Lowassa hajaokoka , je ni wachungaji wangapi waliookoka wangeweza kuzuia kama yasimtokee Lowassa kamaLowassa angekuwa muumini wa kanisa lake??

Amkeni maaskofu kondoo wenu wanararuliwa kwani nyie ni viongozi wa mshahara?, Yesu alisema kiongozi mwema yuko tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine.Mna Mungu anayetisha, anayeweza,wa haki muwazi mkweli,hashindwi,haogopi!.Jamani hata sasa tunahitaji kuwaona mashujaa wa Imani za kiroho na kimwili,hata kama hawataandikwa kwenye biblia mbinguni wataandikwa!

Ukiwa na viongozi wa kidini vipofu,wasiosema kitu wala kukaripia serikali kama akina Gamanywa,Kulola n.k ambao kwa nafasi zao walitakiwa wawe wakali na hakika Taifa lingewaogopa na kuwaheshimu si siri na si bure viongozi wa kilokole Tanzania hawaheshimiwi huwezi kufananisha heshima ya Pengo serikalini na Kulola?? Hiyo nguvu isiishie kuombea watu Yohana alimbatiza mpaka Yesu bado akaenda gerezani kwa kusema kuwa mkuu serikali ni mzinzi, je ni ngumu sana kwa mtu kama Gamanywa kukemea uovu nay eye ni mwenyekiti wa makanisa ya kipentecost!! Kalagabaho watu wanafanya biashara zao na wako tayari ku-compromise GOD’s standard by using money!! Sio kwamba simpendi nazungumza kwa nafasi yake na vita ya maisha bora tunayoyalilia.

Urafiki huu na uoga huu tutaletewa sheria ambazo watapitisha waumini wenu ili hali nyie mmekaa kimya.Wabunge wa Afrika kusini waliopitisha sheria ya kutambua ndoa za jinsia moja, hivi hawa hamna wakristo?, si wana viongozi wao wa kanisa.Basi tunaweza kusema ndiyo wanayofundishwa kanisani? La! sasa wanatoa wapi.Kuchekea na kudharau mambo madogo huzaa makubwa,Kanisa lingekuwa na nguvu hata hiyo hoja ya mahakama ya kadhi wangejiuliza mara mbili kama waizue au wakae kimya , kutokana na udhaifu wa Kanisa linajadiliwa mpaka kuundiwa tume inayolipwa na kodi za waumini wa kanisa! Wameona sisi ni dhaifu tuko kimya kazi kuandaa matamasha na kuwaita viongozi wa serikali wazindue albamu na kugawa tuzo! Tumemwachia kazi hii Mtikila!!

Tusiangamie kwa kukosa maarifa yaliyo katika uwezo wetu kuyafanya tunayafanya,tuna mamlaka,tuna Mungu,tuna Roho tuna elimu,tuna mdomo tuna la kusema,hatujachelewa bado,kumbe kweli mmomonyoko wa maadili,maisha ya taabu ya wananchi kanisa limechangia.Hivi ndio Nionavyo mimi INAWEZEKANA AMKENI!!

‘’Lakini nawasihi, ndugu,mchukuliane na neno hili lenye maonyo maana nimewaandikia kwa maneno machache’’ Waebrania 13:22

Nakala hii pia niliitoa gazeti la nyakati toleo la 335 May 2007, edited to suit now.

Kalenge-Canada
Imanimartini2222@gmail.com

Friday, March 7, 2008

UMUHIMU WA KANISA KATIKA SIASA NCHINI TANZANIA

UMUHIMU WA KANISA KATIKA SIASA NCHINI TANZANIA

Ndugu wana-Kanisa la Tanzania, na wana-blog wote wa SAYUNI Amani, Upendo,na Furaha atoavyo Yesu Kristo viongezwe kwenu wote daima.
(*** Hii ni makala ambayo nimeipeleka katika gazeti la Kikristo hapa Tanzania la Nyakati na pia nimeona vyema kuileta hapa katika mlima huu wa Sayuni)

Nimeguswa siku hii ya leo kusema kidogo yale Mungu aliyoyaweka katika moyo wangu kuhusu uhusiano katika ya Kanisa na siasa ya nchi hii. Nimesikia watu wengi wakitoa mawazo yao, na mimi sipo hapa kuwaponda bali natoa na mimi kile Mungu alichoweka ndani ya moyo wangu. Ni maombi yangu pia kuwa nitakachokisema hapa kitakuwa cha kuujenga mwili wa Yesu na si kuuharibu.
Ninajua watu wengi mno wamekuwa WAKISISITIZA kuwa kanisa haliruhusiwi kabisa kuchangamana/kujihusisha/kuhusika katika siasa, lakini mimi ninaamini kabisa kuwa kanisa lina sehemu yake kubwa mno katika siasa.
Ninachoamini moyoni mwangu ni kwamba kanisa lina mchango mkubwa sana katika mwelekeo wa siasa za nchi ikiwemo Tanzania. Naomba tukubaliane kwanza kwamba hali ya kisiasa ya nchi yoyote iwe mbaya au nzuri inawaathiri watu wa nchi ile wote, kanisa likiwa mmojawapo.Hali ya kisiasa ikiwa mbaya katika nchi wote tunafahamu ni nini matokeo yake,na tunajua kuwa athari zake zitalipata na kanisa pia,kama tulivyoona yaliyotokea kwa wenzetu wa Kenya.
Kutokana na hali hiyo niliyoeleza, ina maana kuwa sisi kama Kanisa tusipofanya sehemu yetu katika kushughulikia hali ya kisiasa ya nchi yetu,tutakuwa tunajiwekea makaa ya mawe vichwani mwetu au kukata tawi tulilokalia.
Kwanza kabisa,Ndugu zangu,ninachofahamu mimi ni kuwa Serikali ya nchi hii(na yoyote) inatakiwa kufanya shughuli zake kwa kufuata ushauri wa karibu sana kutoka kwa Kanisa,yaani kwa kuliangalia kanisa namna linavyofanya mambo yake,kanisa likiwa kama mwakilishi wa Mungu hapa duniani.Twaweza kuliona hili tukiangalia kwa undani safari ya wana wa Israeli kule jangwani kuelekea Kanani.Tuangalie pale walipofika katika mto Jordan.(Yoshua3 hadi 4).Tuangalie Yosh3:3;”Wakawaamuru watu wote wakisema,mtakapoliona sanduku la agano la BWANA, Mungu wenu, na makuhani walawi wakilichukua,ndipo mtakapoondoka hapa mlipo na kulifuata Ninaamini kuwa wengi tunafahamu kuwa sanduku la agano ndani yake kulikuwa na ‘ushuhuda’ yaani Neno la Mungu,kwahiyo kwa sasa maana yake na Neno la Mungu.Halafu wale makuhani walawi kwa sasa ndio watumishi wa Mungu (kanisa),na Roho Mtakatifu ameweka ndani yangu yale maji ya mto Yordani kuwa tafsiri ya Hali muhimu inapopitia nchi yeyote,na kwasasa tukizungumza kuhusu hali ya kisiasa.Tukiutafsiri huo mstari hapo juu ina maanisha kuwa, watanzania(wakiwemo viongozi wa serikali) wanaambiwa kuwa “Mtakapolisikia/Kuliona Neno la Mungu, na Kanisa/watumishi wa Mungu wakilibeba (kulihubiri),ndipo ninyi mtakalifuata hilo Neno wanalolisema kuhusu siasa/uongozi” Na ukiusoma mstari wa Nne kipengele “b” kinasema kuwa “Kwa maana hamjapita njia hii bado”. Ninapenda kusisitiza kuwa inatulazimu sasa kanisa tuifute kabisa ile dhana ya kuiona siasa kama dhambi,kwani inatupeleka sisi wenyewe pabaya.Kanisa linawajibika katika siasa katika njia mbalimbali, si lazima watumishi wote tuhamie kwenye siasa,hapana. Ukiendelea kusoma kitabu hicho cha Joshua sura ya 3 na 4 zote,utaona kuwa wale makuhani waliobeba sanduku la agano walipotia miguu yao katika mto Yordani yale maji,tena mengi ya ule mto yalisimama na wale makuhani waliendelea kusimama pale ndani ya kingo za mto hadi wana wa Israel wakavuka WOTE,Ndipo Yoshua katika Yos 4 anawaamuru kuondoka.Hii ni ishara ya KUHITAJIKA KWA MAOMBI KUELEKEZWA KWA VIONGOZI NA WANASIASA.Maana yake,WOTE tuliookoka tunatakiwa kusimama katika mto Yordani(Yaani kuombea hali ya siasa ya nchi hii) mpaka hapo taifa letu litakapovuka kwa kufanikiwa katika eneo hili la siasa.Nawashauri sana ndugu zangu katika Kristo tuifanye kwa bidii njia hii moja ya kanisa kushiriki katika siasa(kuomba).Haifai kabisa sisi wapendwa kuanza kuwalaumu mafisadi na viongozi wabovu wakati tulikuwa hatuwaombei,it’s not fair,na tusipobadilika tunaweza kujuta siku moja(Ewe Mungu epusha hili)
Njia nyingine (ya pili) ya kanisa/watumishi/waliokoka kuhusika na siasa ni sisi wenyewe kuonesha mfano mzuri wa uongozi unafaa kuigwa na serikali,hiyo ni njia muhimu sana ndio maana kwenye Yoshua3:3 Mungu aliagiza taifa la Israel lifuate Neno la Mungu linalohubiriwa na Makuhani,yaani kanisa.Sisi kama kanisa tunatakiwa tuweke mfano bora,iweje tulaumu kuwa kiongozi amekaa madarakani muda mrefu sana kama kanisani tunao viongozi kama hao pia? Nakumbuka mtumishi mmoja aliwahi kuwauliza watu mahali kama ni watu wangapi makanisa yao yana miradi?Wengi sana walinyoosha mikono.Halafu akauliza, wangapi wameridhishwa na jinsi miradi hiyo inavyoendeshwa?Asilimia kubwa walionyesha kutokuridhishwa kabisa.Sasa ndugu zangu, kama sisi kanisa tutashindwa kuendesha mradi wa shs laki tano, itakuwaje tumlaumu kiongozi aliyeshindwa kutunza mabilioni ya serikali?Je hakuiga kanisani huyu?.Tumeilaumu serikali kuwa haiwajali vijana ipasavyo, je kanisa tunajali vijana, hebu tuangalie namna kanisa linavyoutunza UKWATA na vikundi vingine vya vijana mashuleni na hata makanisani,asilimia ngapi ya bajeti inawalenga vijana? Je serikali haijaiga kwetu? Hatujachelewa sana, we still have time ,let’s make the most of it, tubadilike sasa,tuoneshe mfano bora kwa wanasiasa.

Njia nyingine sasa ni hii ya UONGOZI,Nasisitiza kabisa UONGOZI, watu wamepinga sana watumishi wa Mungu kuingia katika uongozi wa kisiasa, mngejua mimi namwomba Mungu atupe viongozi waliookoka WOTE,Hakuna raha kama hiyo.Tatizo ni kwamba kanisa limejijengea mawazo kuwa siasa ni dhambi,au hata kama si dhambi, sisi watumishi wa Mungu haturuhusiwi kugusa siasa kabisa,ni rahisi kuhisi pia kuwa watu hawa huwa hawawaombei viongozi pia.Mimi ninaamini kuwa wapo watu wengi MNO katika hii nchi ambao Mungu amewapaka mafuta kuwa viongozi,ndiyo maana tukisoma habari za karama 1Wakorintho 12:28:Na Mungu akaweka wengine KATIKA KANISA,wa kwanza mitume.....manabii wa tatu waalimu kisha miujiza,kisha karama za kuponya wagonjwa,masaidiano na MAONGOZI na aina za lugha” Angalieni ndugu zangu Biblia imesema katika Kanisa kuna karama zote hizo,Tena Biblia za kiingereza (AMP) imewaita Administrators,yaani watawala/wasimamizi(viongozi)
Ni kweli kuwa si kila mtumishi amepewa kuwa kiongozi,na pia si wote wamepakwa mafuta ya uongozi wa serikali,wengine ni viongozi wa makanisa na huduma.Sina shaka kabisa kuwa wote tunafahamu Mfalme Daudi alipakwa mafuta kuiongoza Israel tena kwa miaka 40 kama mfalme,kiongozi wa nchi ile,tena tunajua kuwa Mungu alikuwa naye karibu sana akimwongoza namna ya kuiongoza ile nchi,hata katika vita alimwambia nini cha kufanya na wakashinda,na pia mwanawe Solomoni namna alivyomwomba Mungu naye akampa hekima kwa ajili ya kuwaongoza watu wake.Hebu mkumbukeni nabii Musa namna Mungu alivyomteremshia hekiama ya kuwaamua watu wake kupitia kwa mkwe wake Yethro kwenye Kutoka 18:13-26,Hebu mkumbukeni mfalme Yehoshafati wa 2Mambo ya Nyakati20 alichofanya.Alikuwa mfalme,wakavamiwa na adui,akenda kumwabudu Mungu,kisha akamwomba,Mungu akasema naye na kisha Mungu akawapigania taifa zima, hebu mkumbukeni mfalme Hezekia kwenye 2Walme18&19,walitishiwa kuvamiwa,tena kwa barua na ujumbe wa watu maalumu kutoka kwa Senakerib,yeye Hezekiah akawahi kumwonesha Mungu,na Mungu akawapigania na kuwaokoa.
Ninawasihi wale watumishi ambao wanajua Mungu amewapaka mafuta kuongoza nchi hii,wajifanye tayari kushika nafasi hizo.Ninaomba tena kanisa tubadilishe kabisa mtazamo huo,mnafahamu ndugu zangu,Kwa sababu kanisa limekuwa likiona kuwa halina uhusiano na siasa,limekuwa likiwalea wakristo,vijana katika namna ambayo haiwaandai kuwa viongozi wa nchi hii,matokeo yake wale vijana wakikua wanapewa uongozi,lakini kwa sababu kanisa halijawaandaa kuwa viongozi,wanafanya mambo wanayoyafanya halafu walezi wao (kanisa) wanajiunga kuwalaumu,wote si tunafahamu ni viongozi wengi ambao hawaongozi vizuri sasa ni wakristo,na hata kwenye sherehe zetu huwa tunawaalika?
Naamini wengi wetu tumewahi kusikia tetesi za kuhusishwa kwa viongozi wetu na mambo ambayo hayampendezi Mungu,je tungekuwa na viongozi waliookoka haya yangepitia wapi?Nadhani mnaamini kuwa kitendo cha kuvunjwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi yetu na Israel kimetuletea mabaya sana, je tungekuwa na viongozi waliookoka yangetufika haya?Hebu angalieni ile hekima Mungu aliyompa Mfalme Solomoni akaitumia kuamua kesi ya wanawake wale katika 1Wafalme3:16-28, je tungekuwa na viongozi waliookoka katika nchi yetu, ndugu zangu mikataba feki ingepitia wapi,huku tuna viongozi waliokoka na kanisa linawaombea mchana na usiku???Habari ya kuiingiza nchi kwenye IOC ingepitia wapi TUKISHIKA ZAMU ZETU?Jambo la Mahakama ya kadhi lingeanzia wapi?
Narudia kusema tena kuwa mimi simlaumu mtu,maana na mimi mwenyewe nipo ndani ya kanisa,lakini naweka changamoto hii kwa kanisa na wachungaji,wainjilisti na maaskofu wetu,tubadilike sasa,tushike zamu zetu katika siasa,Tuwaombee viongozi na wanasiasa,tuoneshe mfano bora na tuingie katika uongozi wa serikali(kama Mungu amekuita kwa ajili hiyo).Tukiendelea kukaa pembeni na kutazama,shetani atakuja saa tumelala,atawavuruga viongozi na watafanya mambo ambayo yatakuja kutudhuru sisi wenyewe kanisa.Tusikubali kukaa pembeni halafu tumwachie ibilisi aje na kupanda mbegu zake mbaya kwa wanasiasa.Si mnakumbuka kitu ambacho Mordekai alimwonya Nabii Esta kwenye Esta 4:12-14. Nasisitiza pia kanisa litie mkazo katika malezi ya vijana kuanzia ngazi ya chini,kuwalea kwa namna ambayo itawaandaa kuwa viongozi wazuri huko baadaye.
Kwa mfano tusipokuwa na vijana waliookoka wanaosomea sheria, je shetani hatawatumia wengine kutunga na kupitisha sheria ambazo ni kinyume na mapenzi ya Mungu katika nchi hii? Tusipokuwa na vijana waliookoka wanaosomea udaktari tutaweza kuwapata madaktari kama wale wakunga waliokuwa wakiwasaidia wanawake wa ki-Israel kujifungua wakati wa kuzaliwa Nabii Musa?
Lakini njia nyingine ya kanisa kuhusika katika siasa ni sisi watumishi wa Mungu KUWASHAURI viongozi.Ni wajibu wetu sisi kama watu tuliojazwa Roho Mtakatifu wa Mungu,watu tuliopewa kusema na kusikia kutoka kwa Mungu,kuwashauri viongozi wa serikali kile ambacho Mungu anatuambia sisi watumishi wa Mungu.Hiyo ni sehemu yetu na sisi na haifai kuikwepa kabisa.Natumaini wote tunajua kuwa kuongoza serikali si kazi rahisi hata kidogo,ni kazi nzito,hivyo kwa mfano kikitokea kitu kizito/kigumu hapa Tanzania ni lazima sisi makuhani tukae katika zamu zetu,twende kwa Mungu tukamuulize hapa tufanye nini? Atakachosema tuje kuwaambia viongozi wetu,hii ni muhimu.Hebu kumbukeni wakati ule wa Farao wa Misri na Yusufu,wakati Mungu alipomwonesha Yusufu miaka saba ya njaa iliyokuwa mbele ya taifa la Misri (Mwanzo 41:1-57),kisha akamwambia na kitu cha kufanya,(akamwambia waweke akiba kwa miaka saba),kisha Yusufu akamshauri Farao cha kufanya,na Farao akaamua kumteua kuwa waziri mkuu. Naona kama tungekuwa tumeshika zamu zetu vizuri,Mungu angesema nasi kuhusu ule ukame wa mwaka 2006 mapema kabla haujatokea,halafu angetuambia tujiandae vipi kuukabili,na nina uhakika kabisa UFISADI WA RICHMOND USINGETUPATA WATANZANIA,maana tungekuwa tumeshaandaliwa na Mungu mapema. Nawatia moyo tuifanye hii zamu yetu.
Ni wazi kabisa kuwa hali ya kisiasa ya Tanzania inashikiliwa na waombaji,nami nichukue nafasi hii kuwatia moyo katika Jina la Yesu,tukazaneni kutubu na kuomba kwa ajili ya eneo la siasa ,uchumi, amani na mambo mengine kwa ajili ya nchi yetu, Mungu aliyetuumba atatulipa kwa wakati tusipozimia roho.
Kwa moyo wangu wa dhati namrudishia Mungu atawalaye bila mwisho utukufu wote,wote kabisa.
Mungu awajaze nguvu zake kwa kusudi lake.
Frank Lema
www.lema.or.tz
savedlema@yahoo.com
Arusha.