Thursday, March 6, 2008

BREAKING NEWS

BREAKING NEWS....!

NIMEPATA HABARI ZILIZOTHIBITISHWA KWAMBA NDUGU YETU, KAKA YETU, RAFIKI YETU, MTUMISHI MWENZETU NA MWANAHABARI WA SIKU NYINGI KATIKA ULIMWENGU WA HABARI ZA KIKRISTO LENGAI NELSON, MUME WA AI MWANA WA LAIZER (AMBAYE ANATANGAZA PRAISE POWER RADIO FM) AMEFARIKI KWA AJALI YA GARI JUZI JIONI.
INAELEZWA KUWA LENGAI AMBAYE KABLA MAUTI HAYAJAMFIKA ALIKUWA NI MFANYAKAZI WA WAPO RADIO ALIKUWA AKITOKEA HINDUMANDALI HOSPITAL AKIWA NA MKE WAKE.GARI YAO ILIGONGWA NA GARI NYINGINE MAENEO YA POSTA.
HALI ZA MAJERUHI WENGINE ZINAENDELEA VIZURI NA MSIBA UPO NYUMBANI KWAKE KURASINI KARIBU NA STUDIO ZA WAPO RADIO.
INATEGEMEWA MWILI WA MAREHEMU KUSAFIRISHWA KWENDA ARUSHA KWA MAZIKO SIKU YA IJUMAA.
MIMI BINAFSI NITAENDELEA KUMKUMBUKA LENGAI NELSON KWA MUDA MREFU KWANI ALIKUWA NI RAFIKI YANGU NA MARA YA MWISHO TULIONANA NAE PALE TARAKEA RESTAURANT MWENGE MIEZI KAMA 3 HIVI ILIYOPITA.TULIONGEA MAMBO MENGI SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUANDAA PROGRAM MBALIMBALI ZA TV KWA AJILI YA MWILI WA KRISTO.
LENGAI NELSON NIMEFANYA NAE KAZI KWA KARIBU SANA KWA MUDA MREFU TUKIWA CHINI YA TANZANIA YOUTH MINISTRIES (TAYOMI) KABLA NA BAADA YA YEYE KUHAMIA WAPO RADIO.
TUTAKUKUMBUKA DAIMA LENGAI NELSON
TUMWOMBE MUNGU AZIDI KUMPA AFYA NJEMA NA KUPONA HARAKA MKE WAKE AI MWANA WA LAIZER.

TUTAZIDI KUWALETEA HABARI ZAIDI NA PICHA ZAIDI ZA MATUKIO.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIBARIKIWE

1 comment:

Anonymous said...

Asante kwa taarifa, mtade inahuzunisha, Mungu ampe nguvu dada yetu AI,