Monday, March 31, 2008

Mama Rwakatare na Misukule

Week mbili zilizopita tuliambiwa na watu walioudhuria ibada kanisani kwa mchungaji Rwakatare na hata vyombo vilireport kuwa kuna watoto wawili (Ramadhani na Yusufu) waliodai kuwa ni misukule na kuwa walianguka wakati maombi na ibada ya nguvu ikiendelea kanisani hapo.Mwandishi wetu wa sayuni alikuwepo ibadani hapo na alituletea habari hiyo mchana huo huo wa jumapili.Ila mlima sayuni tulisita kidogo kuzitangaza hapa habari hizo hasa kwa kuzingatia nature ya tukio lenyewe.
Siku chache tangu Mch. Rwakatare atangaze kisa cha watoto hao kudondoshwa na nguvu ya maombi kanisani hapo, jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa kinondoni na mganga (Daktari) mmoja wa kitengo cha magonjwa wa akili muhimbili walisema kuwa watoto hao hawakuwa misukule na ni matapeli wanaojulikana.Polisi walidai kuwa watoto hao wenye umri kati ya miaka 7 na 10 walishawahi kukamatwa kwa utapeli huo na kanisa moja la kipentekoste manzese na walipobainika kuwa walikuwa na njama za kujipatia kipato kwa udanganyifu walipelekwa kituo cha polisi.Kamanda wa polisi mkoa wa kipolis kinondoni ndg Jamal Rwambow, alisema kabla ya kujifanya wameanguka katika kanisa hilo la Mchungaji Rwakatare, hivi karibuni, watoto hao walifanya jambo kama hilo Januari 6, mwaka huu katika eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam.
Watoto hao walidaiwa kuanguka kanisani hapo mikocheni B assemblies of God wakati wakisafiri kwa ungo kutokea mwanza kuelekea mtwara.Na kwamba wao makazi yao ni makaburi ya kindondoni jijini Dar wanapofukua makaburi na kula nyama za watu.
Kisa hiki kimezua mjadala mpya kuhusu maombi ya kuombea misukule hapa nchini.
Sisi kama wanasayuni tunasema kuwa
1.Iwe kwa njia yoyote ile injili lazima itahubiriwa kila mahali ili iwe ushuhuda kwa watu wote na hapo huo mwisho ndipo utakapo kuja.Biblia inasema iwe kwa hila au kwa ukweli injili inahubiriwa.
2.Ni ushauri wetu kuwa ni vyema tuwe makini na roho zidanganyazo makanisani ili kuepuka kuutia aibu mwili wa Kristo.
3.Tunamuheshimu Mch. Rwakatare kama mtumishi wa Mungu na tunatambua mchango wake kwenye jamii yetu.Tunaomba wakristo wawe wanajifunza Biblia kwa umakini zaidi ili wasitumbukie kwenye mitego ya shetani.
4.Ni vyema wakristo tujue kuwa sisi sote ni mwili wa Kristo na shetani amefurahi sana kusikia habari hii na hata kusema kuwa "kiko wapi sasa...tulisema ninyi ni wasanii"...sasa naomba ndugu zangu wapendwa katika Bwana tuwe tunapima mambo maana wakati mwingine shetani anaweza kuleta jambo hili kwa mtindo huu kumbe akawa na lengo la kutuchafua wakrsito wa kweli.
5.Ni vyema tusisahau kuwa shetani ni baba wa uongo tena kweli haipo ndani yake.Kama watoto wale walienda kanisani na kudai kuwa wameanguka kwa nguvu ya maombi..kanisa likawaamini...then wakaenda hospitali na kukiri kuwa walidanganya habari ya kuanguka kwao na pia jamii ikawaamini....je tunaweza vipi kuthibitisha habari wanayoidai sasa kuwa walidanganya nayo ni ya ukweli...?
NB: Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa ya akili hospitali ya muhimbili akihojiwa na ITV alidai kuwa watoto hao wanaugua ugonjwa unaitwa saikosis ambao humfanya mtu kutunga habari na kuifanya kuwa ya kweli hata kama ni uongo...Sasa cha kujiuliza hapa ni kuwa bado tuendelee kuamini habari hii ya wagonjwa hawa wa saikosisi?
Mwandishi wetu wa mlima sayuni alituambia kuwa watoto hao waliletwa kanisani hapo wakiwa na mavumbi mwilini na michubuko sehemu sehemu inayodaiwa ilitokana na kuanguka kwao na kujeruhiwa na kuwafanya watu wengi waamini habari hiyo..

Mungu atusaidie katika kutafakari jambo hili.

5 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli mambo kama hayo yanalichafua Kanisa,hata baadhi ya Wakristo ambao hawajakomaa wanaweza kurudi nyuma wakidhani mara zote usanii hufanywa kanisani.Lakini nafikiri Makanisa nayo yameweka mbele zaidi Shuhuda ambazo mara nyingine zinaweza kuharibu Kanisa,wamesahau ushuhuda Mkubwa kuliko yote ambao ni mtu Kuokoka.Sawa biblia inahimiza mtu kutoa ushuhuda,lakini isiwe kwa kulazimishwa.Bora mtu asikie rohoni mwake Roho mtakatifu akimuhimiza kufanya hivyo.Mtu akishuhudia ameokoka Kanisani basi waumini wataona kitu cha kawaida tu.Lakini akisimulia vitu vya ajabu ajabu basi Watashangilia kupita kiasi hata kama ni ushuhuda FEKI.Ndio maana wengi wao wanakimbilia katika Makanisa wakifuata miujiza,badala ya kufuata Neno la Mungu. lenye uzima tele ambalo kwalo miujiza yatendeka....MUNGU TUSAIDIE...

Daniel J.Nzali

Anonymous said...

Kwa kweli mambo kama hayo yanalichafua Kanisa,hata baadhi ya Wakristo ambao hawajakomaa wanaweza kurudi nyuma wakidhani mara zote usanii hufanywa kanisani.Lakini nafikiri Makanisa nayo yameweka mbele zaidi Shuhuda ambazo mara nyingine zinaweza kuharibu Kanisa,wamesahau ushuhuda Mkubwa kuliko yote ambao ni mtu Kuokoka.Sawa biblia inahimiza mtu kutoa ushuhuda,lakini isiwe kwa kulazimishwa.Bora mtu asikie rohoni mwake Roho mtakatifu akimuhimiza kufanya hivyo.Mtu akishuhudia ameokoka Kanisani basi waumini wataona kitu cha kawaida tu.Lakini akisimulia vitu vya ajabu ajabu basi Watashangilia kupita kiasi hata kama ni ushuhuda FEKI.Ndio maana wengi wao wanakimbilia katika Makanisa wakifuata miujiza,badala ya kufuata Neno la Mungu. lenye uzima tele ambalo kwalo miujiza yatendeka....MUNGU TUSAIDIE...

Daniel J.Nzali

Mary Damian said...

Watu wengi wanaamini kwa kuona! ishara na miujiza imejaa akilini mwa watu, wengi wanapenda wahubiriwe kuhusu ishara na miujiza na ukiangalia watumishi wanaohubiri hayo wana wafuasi wengi, Biblia inasema enendeni ulimwenguni mkahubiri injili kwa kila kiumbe, aaminiye na kubatizwa ataokoka asiyeamini atahukumiwa. makanisani mengi hawahubiri kuhusu kuacha dhambi wanaliwazana na kutoa shuhuda nyingi zisizokuwa na hakika na kuzitangaza kila mahali, watumishi wengi wanavua watu kutoka makanisani mwa watu kwa kisingizio cha ishara na miujiza,inabidi tujitahidi kusema ukweli na kuwaambia watu habari njema za ufalme wa Mungu, watu waache dhambi na sio kupeana matumaini.

Anonymous said...

Mtumishi,shetani huwa anafanya hivyo, anakupeleka mahali fulani kwa mbwembwe halafu anakuacha.

Biblia imeonya mara nyingi msimpe nafasi shetani, huwa hafanyi makosa akipewa nafasi, anaharibu, anaua na anachinja.

Hainiingii akilini kama jambo la misukule au wachawi kukamatwa ni jambo la kuutangazia ulimwengu, hata wasio amini. Hiki ni chakula kigumu kwao na wengi huwa hawaelewi badala yake huishia kuona kuwa kumbe ukristo kuna uchawi!!! hawajui.

Hata Yesu alipoponya kuna watu aliwaambia msiseme. kuna mahali walimwambia anatumia nguvu za giza!! maana hawaelewi.

Kuna shuhuda za kutangaza kwa watu, na zingine tunazimeza kwanza, lengo ni kuwa hawa watu wanaodondoka kwa uweza wa Mungu, ndio wa kwanza kwenda kueleza wachawi wenzao kuwa Yesu, anaweza, ushuhuda!!

Tukitaka sifa za kuleta watu na kuwajaza makanisani matokeo yake ni aibu kama hizi.

WATU HAWAONGOZWI TENA KWA ROHO, WANAONGOZWA KWA UTASHI WAO, WAMEMZIMISHA ROHO MTAKATIFU.KINACHOBAKI NI AIBU.

KUNA vyakula vya kuwapa watu wanaomjua Yesu na vingine havieleweki kwa wasiomjua, tunaposema kutangaza ukuu wa Mungu sawa, lakini mpaka Roho akuambie asiposema kaa kimya.

Roho ni msaidizi, Rafiki, Mwombezi,mkumbushaji, mwonyaji, hana papara, huwa anazungumza kwa Sauti ya upole sana,HAAIBISHI usipimsikiliza anakaa pembeni.

Huu ni ujinga wetu wenyewe, shetani hana lolote, wala nguvu zake haziwezi kutushinda, ila tumeonywa tusimpe nafasi.

Tunajifanya tunajua, Na kipimo ni kuwa WATU WANGAPI WALIOKOKA KWA KUSIKILIZA KUWA WATOTO WAWILI WAMENASWA NA NGUVU ZA MUNGU, KAMA HAKUNA ALIYEOKOKA, HUO HAUKUWA USHUHUDA WA MUNGU.

INJILI KUBWA NI SISI KUWA BARUA, NI INJILI YA NGUVU KULIKO HATA MIUJIZA.
WALOKOLE TUMEKOSA USHUHUDA WA KUWAFANYA WATU WAOKOKE.

Tumewaachia kazi hii wasanii wachache ambao wako tayari kuwaita watu wafanye matamasha ya kuwaenzi wafu. HALAFU WALOKOLE KIBAO WANAENDA,.


BILA MAANADIKO NA MAARIFA YA MUNGU, TUTAANGAMIA, TUTAAIBIKA KILA SIKU.

NAMALIZA KUSEMA KUWA ROHO HUWA ANAMUANDAA MTU FULANI AOKOKE KWA NAMNA FULANI, KAMA AKIKUAMBIA USHUHUDA HUU SEMA LAZIMA KUNA MTU UTAMLENGA AMA SIVYO NI KUPOTEZA MUDA NA KUTAKA SIFA.


NINA WASIWASI WACHUNGAJI WENGI WA SASA YESU AKIRUDI GHAFLA WANAWEZA KUUA TENA!! maana hawafanyi bliblical things.

KUNA WACHUNGAJI NASIKIA WAMEANZA KUWEKA PICHA ZAO KUTANGAZA MAKANISA !!!! KILA MCHUNGAJI AKIWEKA , NCHI NZIMA ITAJAA PICHA ZA WATU.

YESU ATUSAIDIE.mwanadamu akitaka kuhalalisha kitu hata kosa sababu wala pengine andiko.

Anonymous said...

Kwakweli tunachoshwa na mambo kama hayo. Yule mama alifanya makosa kumkaribisha Askofu mmoja wa pale Ubungo (zamani) kutoa mahubiri yake ya misukule kwenye redio yake. Washirika wake wengi wakahamia Ubungo wakati huo. Akatangaza hio ya Ubungo ni imani potofu. Ghafla na yeye akaanza kutoa misukule. Sasa watu wanajiuliza which is which? Ingawa watu wake hawakurudi ila akapata wengine wapya wengi. Siku hizi watumishi wanafanyia watu biashara. Mungu atusamehe sana.