Friday, March 7, 2008

Yaliyojiri Kanisani Mwananyamala

Aibu ya mwaka imetokea katika Kanisa la Assemblies of God Kijitonyama, Dar es Salaam baada ya kijana mmoja kuingia ibadani akiwa mtupu.....

Tukio hilo la kustaajabisha lilitokea hivi karibuni ambapo kijana huyo aliyetajwa kwa jina moja la Julius alijitosa kanisani hapo kujiokoa na umati wa watu uliokuwa ukimtuhumu kuwa ni mwizi.Shuhuda wetu aliyekuwa eneo la tukio ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo alidai kuwa, wakiwa ibadani walishangaa kumuona Julius aliyedai kuwa ni muumini wa kanisa hilo akiingia na kumfuata madhabahuni mama Mchungaji, Zetumbi aliyekuwa akiongoza ibada.“Kila mtu alipigwa na butwaa, tukafikiri ni ibilisi kaingia kanisani, baada ya muda tukasikia mayowe ya watu wakihimiza atolewe ndani.“Jamaa naye alizidi kumsogelea mama mchungaji na kuomba asaidiwe, waumini nao wakawa wanatawanyika kukwepa aibu hiyo,” alisema muumini huyo aliyejitambulisha kwa jina la Zakayo.Aidha, Julius mwenyewe alikana kuhusika na wizi badala yake alidai kuwa yeye ni mkristo na alikuwa akielekea kanisani asubuhi hiyo.Akijitetea na tuhuma hizo za wizi Julius alidai kuwa, wakati akielekea ibadani alikutana na vibaka ambao walimpora, kumvua nguo kisha kumpigia mayowe ya mwizi.Julius aliongeza kwamba, hakuwa na njia ya kufanya baada ya tukio hilo zaidi ya kuingia kanisani humo akiwa mtupu kujiokoa asitolewe roho.“Nishaibiwa na kusingiziwa kuwa ni mwizi, watu wameanza kunifukuza na kunipiga, nifanyeje, imebidi nijisalimishe kwa Mungu,” alisikika Julius akijitetea.Licha kijana huyo kujitetea, kundi la watu waliokuwa mlangoni walizidi kusisitiza kuwa alikuwa ni kibaka mzoefu na kutaka atolewe ndani ili wamuue.Akielezea tukio hilo Mama Zetumbi ambaye ni Mchungaji wa kanisa hilo alisema, kijana yule alikimbilia kanisani kujiokoa lakini akasema hana ushahidi kama ni mwizi au la!“Sisi ni watu wa Mungu hatukumhukumu, tulimsadia na kumwachia aende polisi, hatuna la zaidi,” alisema Mama Mchungaji.

No comments: