Wednesday, March 26, 2008

Maji ya Baridi!“...Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari…” Mwanzo 1:9-10

Kwa wale wapendao maji ya baridi, nadhani taarifa hii itawafaa sana!

Ni kweli inapendeza na ni sahihi kabisa kwa wengi kwamba wakati walapo au mara baada ya kupata mlo kutumia bilauri ya maji. Maji hayana tatizo bali yanapokuwa ya baridi sana hapo ndo penye tatizo.

Maji baridi yaingiapo mwilini hugandisha mafuta ambayo umemaliza kuyala pamoja kwenye chakula. Sambamba na hiyo pia maji baridi hupunguza kasi ya utendaji kazi wa vimeng’enyo mahsusi vya vyakula mwilini. Hii hupunguza kasi ya usagishaji na kufyonzwa kwa virutubisho vilivyomo vyakula hivyo kuingia katika chembechembe za mwili. Mafuta hayo yaliyoganda yachanganyikapo na tindikali mwilini humeng’enywa kwa haraka kuliko chakula kingine kigumu ulichokula.

Mafuta yaliyoganda hutengeza utando pembezoni mwa ukuta wa tumbo (intestines). Baadae mafuta hayo huweza kupelekea mtu kupata saratani ya utumbo.

Hivyo kwako mpendwa unayesoma makala hii ni vizuri kuzingatia matumizi ya vitu vya moto au vya uvuguvugu haswa pindi umalizapo kupata mlo. Vitu kama supu au maji ya uvuguvugu ni bora zaidi. Wachina na wajapani ni utamauni wao kula chakula na chai ya moto, sasa sijui na sisi tuige au la!!

Mafuta mengi mwilini pia huweza kupelekea tatizo la mshtuko wa moyo hivyo chukua tahadhari kungali na mapema.

Ni ahadi ya Mungu uishi siku nyingi hapa duniani na kisha uzima wa milele mbinguni na baba !

The more we know the better chance we could survive!!!
Hosea 4:6

1 comment:

Anonymous said...

Mungu akubariki mtumishi, nadhani nitabadilika sasa, maana leo hii kuna mtu amenieleza sawa na ulivyoandika, biblia inashauri kwa vinywa vya wawili au watatu neno uthibitishwa.Ubarikiwe this blog is helpful to me

stay blessed

Kalenge