Thursday, March 13, 2008

Wafanyikazi wa ndani! (HOUSE GIRLS)!

Nimesikia habari na matukio mbalimbali yahusianayo
na wafanya kazi wetu wa ndani majumbani! Kwa mfano matukio ya hivi karibuni Mfanyi kazi mmoja alimuua kwa kumuweka mtoto kwenye oven kisha kumuoka kama mkate, mwingine alimsokomeza matambara mdomoni na hivi karibuni tukio la ndugu yangu mpendwa (jina kapuni) mtoto wake alinyweshwa mafuta ya taa kwa nia ya kumtoa roho. Ashukuriwe Mungu kwamba alimnusuru maisha yake. Baadae huyu house girl aligundulika kuwa na mapepo ndani yake. Wengine wamediriki hata kusema kwamba ma-housegirl hao ni kama tumewafanya kuwa watumwa kwa kazi wazifanyazo majumbani mwetu, sina uhakika kama ni wote. Swali la msingi ni hili, Je ni kweli kwa zama za leo zenye DayCare nyingi na nyumba za kutunzia watoto japo si za kiwango cha juu twahitaji wafanyi kazi wa jinsi hiyo?

Kwa Housegirl wakati mwenye nyumba yuko kazini, shuleni, biasharani au mihangaiko mingine yeye:
1. Anakula na kunywa vizuri anachotaka awapo nyumbani kuliko wewe

2. Ndo mwenye kuangalia TV yako nzuri na mikanda mizuri ya Video kwa muda mrefu kuliko wewe. Kama ni nyimbo ni yeye azijuaye na hata hufikia kipindi cha yeye kukuhadithia

3. Kama ni viti vyako vya bei mbaya yeye ndo anavikalia kwa muda mrefu

4. Ana muda mwingi wa kupumzika mchana kuliko hata wewe

5. Akiugua wewe ndo unamtibu tena kwa gharama kubwa

6. Wakati wa safari lazima umkatie tiketi na uhakikishe kasafiri salama wakati wewe hujihangaikia mwenyewe

7. Hana shida ya kupanga bajeti ya nyumba (Haumizi kichwa) na wala hatafuti pesa

8. Christmas na sherehe nyingine, lazima nae umtoe kwa kivazi kizuri

9. Umempa dhamana ya kulea na kufundisha watoto wako chochote atakacho kwa muda mrefu kuliko wewe

10. Ndiye mwenye kuijua nyumba yako na kona zake pengine kuliko hata wewe

11. Lazima umpe mshahara wake wa mwisho wa mwezi ambao yumkini ni nusu ya wako (60,000/- Tshs.)
12. Mengine ongeza wewe!!!!

Ni kweli nae huweza kukusaidia kufanya baadhi ya mambo hapo nyumbani lakini kwa faida hizo ambazo kwako mwenye nyumba ni aghalabu kuwa nazo, ni halali kuwa na mfanya kazi wa namna hii kwa siku za leo Au ni kujirudisha nyuma kimaendeleo??

Ndugu msomaji hebu kong'oli mahala palipoandikwa comments na utoe mtazamo wako!

2 comments:

Anonymous said...

Mimi nadhani matatizo haya mengi ya mahouse girl huwa yanasababishwa na wale wafanyakazi wenye umri mdogo kuanzia miaka 12 hadi 19 au 20 hivi but ukichukua house girl mtu mzima mfano miaka 22 au 25 au 30 hivi anakuwa na huruma na mtoto na anajua maisha.Tatizo wake zetu huwa wanaogopa kuibiwa.
Mungu atusaidie

Anonymous said...

mada hii ungeuliza maswali mawili kwanza, umuhimu wa housegirl pili nini kinasababisha matatatizo hayo??inaonekana mtumishi unanegative ideas na housegirls, kwa hiyo umeandika unsuch away kuwa jibu wewe unalo na umeshaliweka mimi alitazama hili kwa mtazamo mwingine,je NINI KINASABABISHA HAYO MATATIZO??

JE HUYO HOUSEGIRL ANGEKUWA KWAO KWENYE FAMILIA YAKE ANGEMUUA MDOGO WAKE KAMA LA KWANINI AFANYE HIVYO?? HOW ARE THEY TREATED ??

will the send article on this issu

ubarikiwe kwa sababu tuna fundishana.

Jibu bado Tanzania haijaifikia viwangi vya daycare-Naandika niko Canada ambapo gharama za mtoto day care kwa mwezi ni laki tatu, gharama ya house girl ni laki sita kwa mwezi!! wengi wanapenda house girls foa safety.lakini ndio wanalipwa pesa nyingi sana.have you ever stay at homethe wole day and just doing some home activities?? is not easy rather it is boring?? then do per month, second-mwaka no where to go??