Thursday, March 6, 2008

Mahakama ya kadhi...kesi ya Mtikila yatupwa

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali ombi la Mchungaji Christopher Mtikila la kupinga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.
Ombi hilo lilitupiliwa mbali jana kufuatia Mchungaji Mtikila kushindwa kuwasilisha majibu ya pingamizi la awali kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali la kutaka kesi hiyo ifutwe. Uamuzi huo ulitolewa na jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu, wakiongozwa na Jaji Salum Masati. Majaji wengine walikuwa ni Robert Makaramba na Aisha Nyerere.
Mchungaji Mtikila aliiomba Mahakama kumpa muda wa kuwasilisha majibu na kwamba alikuwa hana fedha za kuajiri mawakili kwa sababu alihitaji Sh. milioni 40 za kuendeshea kesi hiyo.
Hiyo ni kusema kuwa kwa sasa hakuna kesi ya kupinga uanzishwaji wa mahakama hiyo ambayo imo kwenye ilani ya uchaguzi wa chama cha mapinduzi ya mwaka 2005 na inatakiwa iwe imetekelezwa ifikapo mwaka 2010.
Wapo wapi maaskofu wetu, wachungaji, wainjilisti manabii,mitume na waalimu kulisemea suala hili.Je nafasi ya kanisa katika hili ipo wapi? Maombi ndio silaha yetu kuu katika kurekebisha mambo ambayo hayaendi ipasavyo.Lakini hatua za kisheria za kulinda katiba ya nchi ni vyema zikafuatwa maana katiba inalihusu na kanisa pia.

1 comment:

Anonymous said...

Shalom! nimefurahi kuiona blog hii! Napenda kuwakaribisha pia katika blog nyingine ya kikristo www.strictlygospel.wordpress.com Mungu awabariki sana