Tuesday, March 25, 2008

Siionei haya injili..maana ni uweza wa Mungu...
Baadhi ya vijana wadogo wengi wao wakiwa chini ya umri wa miaka 20 ("under 20") wakimuhubiri YESU kwa wapita njia na watu wengi pale kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam.
Hiyo ilikuwa ni jana jamatatu ya pasaka nilipowakuta vijana hao wakipiga injili iliyojaa uweza wa ajabu.Binti huyo alikuwa akihubiri huku kila mtu akiwa ametulia kimya kama amemwagiwa maji ya baridi na kusikiliza neno lililojaa munyu kutoka katika kinywa cha binti huyu mdogo.
Naomba kuuliza wana sayuni...Hivi injili ya Yona bado inanafasi katika siku zetu kama ilivyokuwa miaka ile ya mwanzo ya themanini au ndio hivyo tena...?

2 comments:

Anonymous said...

Umenikumbusha mbali sana na kwa kweli vijana wa Tanzania na Africa kwa ujumla tunahitaji kumshukuru Mungu sana kwa kuwa sisi bado tuna moto wa Injili na tunampenda Yesu na kuitangaza Injili kama sehemu ya maisha yangu.
Nina abudu kanisa lenye washirika 400 lakini hata vijana 15 hawafiki na hata hao 15 wamezaliwa hapo kanisani ni thehebu lao si kwamba wamekuja kwa Yesu kutoka nje ya kanisa.
Hali ya kanisa kwa vijana katika nchi za dunia ya kwanza inatia shaka sana hasa kwa miaka 40 ijayo kama yesu atakuwa hajarudi.
Hivyo naomba vijana wa Africa tujitahidi na kuzidi kumtumikia Mungu hasa kushiriki katika kuwaleta wengine kwa Yesu na Mungu atatubariki sana.

Najisikia fahari sana kuona vijana wa Tanzania wapo mbele katika Injili.

Lazarus Mbilinyi
Canada
http://mbilinyi.blogspot.com/

Anonymous said...

Injili ni injili tu, iwe ya Yona au akina Bonnke na vyombo viiiingi!!! Kwa injili hiyo wengi tumemjua na kuwa karibu sana na Mungu!

Niungane na mchangiaji wa kwanza kwamba Afrika na haswa Tanzania tuna neema kwa upande wa vijana. Wakati vijana wengine wakiwaza ma-concert na nitoke vipi week-end hii na nani, wako vijana watakatifu walio jasiri kumtangaza Yesu kwa kila mtu pasi kujali eneo.

Vijana wa Ki-Tanzania endeleeni na moto huo na Bwana ni mwaminifu kazi yenu si bure! Kwani wengi wameokoka kwa aina hii ya uinjilisti.

Ila nitoe ANGALIZO epukeni injili za mipasho haziwaleti watu kwa Yesu, bali lihubirini neno la Mungu kwa ufasaha!