Sunday, March 9, 2008

Bishop George Gichana

Unamkumbuka Mwinjilisti huyu?
Kwa sasa anatambulika kama Bishop George Gichana(GG),anachunga kanisa lake kule Eldoret Kenya.
Kwa hapa nyumbani Tanzania si mgeni sana kwa watu wengi waliokuwa wanahudhuria mikutano maarufu ya the Big November Crusade iliyokuwa inafanyika viwanja vya jangwani mjini Dar es Salaam.
Namkumbuka muhubiri huyu kwa mara ya Kwanza nilimwona pale viwanja vya mnazi mmoja mwaka 1986 wakati the Big November inaanza kabla haijahamia viwanja vya Jangwani.Namkumbuka mtu mmoja anaitwa Salvatory aliponywa kimiujiza kabisa wakati muhubiri huyu anayependa kuitwa GG(tamka jiijii) alipokuwa anaombea watu na kuhubiri injili ya upako na nguvu nyingi.Siku hiyo Salvatory alikuja akiwa amebebwa kwenye machela akiwa mahututi kabisa hawezi chochote akitokea muhimbili na kulikuwa na wagonjwa wengi wameletwa kutoka muhimbili na manesi wengi na magari ya wagonjwa yalikuwa mengi.Mara Salvatory akasimama baada ya maombi na akaanza kutembea mwenyewe kwa kasi ya ajabu akitokea kule nyumba alikokuwa amelezwa na kuja mbele kwa furaha akimshukuru YESU KRISTO wa nazareth kwa kumponya.
Huu ni moja kati ya miujiza ambayo nimewahi kuishuhudia kwa macho ya nyama akitokea live kabisa bila kuwa na maswali maswali yoyote.
Kwa anayejua habari za Salvatory alipo kwa sasa atuambie.
Kwa kweli the Big November miaka ile ilikuwa ya nguvu sana.Nakumbuka miaka iliyofuata watu kama akina Roy Durman na wengine wengi walianza kuja na Dar es Salaam kuliwaka moto kila mwaka.
Hata hivyo hivi sasa the big November imepoteza ule umaarufu wake iliokuwa nao miaka ile na msisimko wa miaka ile.


Mungu atusaidie.

1 comment:

Anonymous said...

GG ananikumbusha mbali mno (1980s) wakati huo ukiwa umeokoka unaonekana ni KITUKO kumbe hatukuwa tunajua kuwa ni NGUVU YA MUNGU...!
GG na kiswahili chake kilifanya nimkumbuke zaidi