Tuesday, March 25, 2008

Mungu anaangalia moyo..

Kuna mtu nilimsikia leo asubuhi pale mwenge kituoni akilalamika kuwa jana alienda kusali kanisa flani lipo karibu na maeno hayo na kukuta wanawake waliokoka wamejichubua sana na mavazi yao yalikuwa yanamtamanisha sana kiasi kwamba akashindwa kufuatilia ibada vizuri.

Eti wapendwa hii imekaaje...maana kuna wanaosema Mungu anaangalia moyo na wengine wanasema tusienende kama mataifa wafanyavyo..

Picha kwa hisani ya Strictly gospel

4 comments:

Anonymous said...

Hiyo kauli ya Yesu anaangalia moyo watu wengi wameitumia kuhararisha mapungufu yao au dhambi katika Kristo.

Ni kauli nisiyoipenda kabisa!

Sijawahi ona tangu nizaliwe mpaka leo hii ni mtu mzima MOYO ukitembea barabarani peke yake bila kiwiliwili. Sasa kama Mungu anaangalia moyo sie wanadamu alama ya kwanza kukutambua ni mwili au muonekano wako wa nje!!

Tusidangayike Mungu hadhihakiwi chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna. Wengine kwa kujipamba sana na kutamani umaarufu wa dunia hii wametupoteza. Wengi wame-compromise na dunia kwa kisingizio cha Mungu anaangalia moyo/roho.

Siamini sana nimuonapo mpendwa viwanja vya adui kisha anambie kwamba yuko upande wa Bwana, hainiingii akilini hiyo. Hebu waimbaji wetu, wachungaji na hata sie washirika na tum - potrait YESU katika maisha yetu kama alivyo kwa matendo na si gharasha! Kama ni kuimba hebu na tuimbe kwa maana ya kumtukuza Mungu na sio siasa, ndombolo wala kwasakwasa pia isiwe kutafuta mapato na mafanikio ya haraka-haraka.Kwa kufuata mafanikio wengi wamepotea!!

Yatosha kwa leo!

Anonymous said...

Bahati amekuwa hivyo siku hizi!!!, wanaosema hivyo watembee uchi basi tuwaone.

Dhambi tu zimewajaa, mwanadamu akitaka kuhalalisha kitu hakosi sababu.

Pili uongozi wa Roho mtakatifu haupo ''Wale wanaoongozwa kwa Roho hao ndio wana wa Mungu'' Kama Roho aliwaambia hizo sentensi wanazojitetea nazo sawa, lakini kama hakusema(na ndivyo ninavyoamini) basi sio wana wa Mungu na wanapoteza muda kwenye wokovu wao

Kalenge

Anonymous said...

kwa kweli kujichubua sio sawaaaaa ni roho ya shetani hiyooooo mungu amekupa weusi furahia na kama wewe mweupe pia furahia ndivyo mungu alivyotuumba weupe kwa weusi.mpingeni shetani muache kujichubua.lo sio sawa kabisaaaaaa

Anonymous said...

Sisi waafrika mbona kazi yetu kuigaiga tu vya wenzetu hususan wazungu? Kwani hatuna nguo zetu na marembo yetu asilia?

Nyie mnaowalalamikia hao wadada usikute ndio wa kwanza kuvaa tai na suti za kizungu mkijiona ndio watakatifu, labda niwaulize je Bwana Yesu na wanafunzi wake walikuwa wanavaaje? Labda tuige uvaaji wao hapo ndio pengine wapendwa hawataleta ubishi kuhusu mavazi! Nani yuko tayari jumapili twende na kanzu na vijikofia vya kiyahudi kanisani?