Thursday, May 8, 2008

UCHAWI UPO HATA BARABARANI - JE UNAOMBA UNAPOKUWA NJIANI?

Hebu soma ushuhuda huu na Bwana akubariki!

Mwaka 1991 Bwana alinijalia kupandishwa cheo kazini (field supervisor) huko Rakai District km 150 toka makao makuu ya kampuni yetu – Entebe, Uganda. Tulikuwa na madereva wengi na kitu ambacho sikujua ni kwamba kati ya hao wapo wawili waliojihusisha sana na mambo ya uchawi! Hawa hawakupenda mtu yeyote aendeshe magari waliyokabidhiwa na wala kupandishwa cheo juu yao. Siku hiyo nilikuwa na ratiba ya kutembelea mojawapo ya vituo vyetu na nikaazimia kutumia moja ya magari yaliyokuwa yakiendeshwa na hao ndugu – (Toyota Hilux D/cabin). Kitu ambacho sikufahamu ni kwamba dereva wa gari nililochukua hakufurahishwa na aliazimia moyoni kunimaliza. Akishirikiana na mwenzie walikwenda kwa mganga wa kienyeji – mchawi na wakafanya walichofanya kwenye gari hilo usiku huo.

Naliondoka Entebe saa tisa jioni nikielekea Kalisizo umbali wa km 145. Na kama kawaida yangu siwashi gari bila kuomba kwanza, hivyo nikaliitia jina la YESU kwa ajili ya ulinzi. Nalipofika Kitubulu kama km 4 barabara ya Entebe – Kampala naligundua kuna kitu cha tofauti. Badala kuendesha nikiwa upande wa kushoto, gari lilikuwa likinivuta kwenda upande wa kulia. Kidogo nigongane uso kwa uso na gari jingine upande wa pili. Tatizo nalidhani ni upepo kwenye matairi hivyo naliamua nipite kituo cha mafuta ili kupima kama uko sawasawa na kisha niendelee na safari yangu. Nikiwa barabarani ile hali ikajirudia tena, naliliitia jina la Yesu na kuomba tena ulinzi wake. Nikiwa karibu na kukifikia kituo cha kujazia mafuta nalisikia mlio mkubwa kwenye bonnet ya gari, lakini sikusimama kwani nalichelea usiku ulikuwa umeendelea. Nalipofika kituoni ndipo nalipogundua kwamba Bwana amenilinda kwani betri ya gari ilikuwa imetoka nafasi yake wakati nikiendesha.

Nalipokuwa nikilala usiku huo niliwaza sana kwanini mambo haya yalikuwa yakitokea kwangu. Sikudhani hata kidogo juu ya nguvu za giza na mashetani. Naliomba kidogo na kisha kujilaza. Usiku huo Mungu hakunieleza chochote kuhusu jambo hilo si kwa ndoto wala kwa neno.

Asubuhi yake nalishtuka kwa swali naliloulizwa na mmojawapo wa wafanyikazi wenzangu. Aliniuliza: Makko, uko salama? Nami nikamjibu Mary niko salama. Nikamuuliza; kwa nini kuniuliza hivyo? Ndipo naye akasema, usiku huo aliota ndoto, na katika ndoto hiyo aliona wale madereva wawili (majina kapuni) wakiwa wameketi kwenye gema pembezoni mwa barabara wakiliangalia gari lako ulilokuwa ukiendesha jana. Katika ndoto hiyo, naliona wameweka majoka mawili makubwa, moja upande wa mbele kukatiza tairi za mbele na jingine nyuma ya gari lako vivyohivyo. Nao walisemazana wenyewe kwa wenyewe: “Ngoja tuone atavyo endesha hilo gari hapo!!”

Akaendelea: Lakini katika ndoto hiyo, nalikuona ukiliua joka la mbele. Na ulilipiga joka lile la nyuma lakini halikufa kabisa. Mary akamaliza kusimulia ndoto yake.

Mara zote huwa sizidharau ndoto kwani Mungu amekuwa akisema nami mara nyingi kwa njia hiyo. Nilirejea chumbani mwangu na kumshukuru Mungu kwa kunifunulia siri hiyo ya nguvu za giza katika ulimwengu wa roho. Kitu ninachojilaumu ni kwamba sikuomba sana juu ya jambo hilo japo niliambiwa kwamba joka moja halikufa bali lilijeruhiwa tu. Siku hiyo nalikuwa nikiendelea na safari kwa kutumia gari ileile nikielekea Kabundabunda, Mjini Kabula. Ghafla mojawapo ya spring za mbele ikakatika vipande viwili. Gari hili lilikuwa imara na kwa tukio hilo nikatambua kwamba sasa ninapambana na nguvu za giza za uchawi kwa mara nyingine tena.

Nikijua kwamba yuko mtu nyuma ya mambo haya na ambaye angependa nife, nilikasirika na kuamua kuchukua Biblia yangu (NIV version). Nikawaambia abiria wawili waliokuwamo garini, Fred na Mary, mmeziona nguvu za Shetani, sasa ni zamu ya nguvu za Mungu kuonekana. Sifahamu naliyatoa wapi maneno hayo. Nalijikuta nikitamka: “ Ndani ya siku nne, vitu hivihivi ambavyo adui zangu wanatamani vinipate vitawapata wao, kwani imeandikwa “… If a man digs a pit, he will fall into it; if a man rolls a stone, it will roll back on him..” Mithali 26:27.
Baada ya kusema hivyo, sikutambua kwamba Mungu aliyachukulia makini maneno hayo.

Nikiwa nimelala usiku huo, Mungu alinionesha mafunuo ya ajabu. Na tazama, joka kubwa likikimbia toka kwenye gari naliyokuwa nikiiendesha na kuingia kwenye gari ya adui zangu. Siku iliyofuatia wakati hao ndugu walipokuwa wakiendesha gari lao, walihusika katika ajali mbaya ambayo iligharimu uhai wao. Hiyo ilikuwa ni siku ya nne baada ya kuwa nimenena maneno yale ya kwenye biblia. Fred na Mary walipoliona gari la wale ndugu lilivyoharibika waliyakumbuka maneno yangu. Nao wakasema kama Farao alivyosema: Hakika Mungu ni Mungu mwenye nguvu!!
Mungu awabariki na kuwaongezea imani wote waliaminio jina la mwanae mpendwa Yesu Kristo!
Imefasiriwa kutoka kingereza!!
Ushuhuda toka kwa: Makko Musagara - Uganda (http://www.christian-faith.com)

1 comment:

Anonymous said...

Mungu ni mkuu na mwema