Thursday, March 13, 2008

Huduma ya kitume na kinabii


Apostle Dastun Maboya wa Calvarry Assemblies of God




Kuna kipindi huduma hii ilionekana kwa wapentecoste wengi kama kituko.Nakumbuka miaka ya 80 na mwanzo kabisa wa 90's nilikuwa nasikia sana karama ya unabii kwenye makanisa mengi yaliyokuwepo wakati huo.
Kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90 Mtume Dastani Maboya ndio ninayemkumbuka kuwa ni mtu wa kwanza kabisa kujitambulisha kama Mtume.,kipindi hicho alitambulika kama apostle Dustan Maboya.
Kuanzia miaka ya katikati ya 90 na hadi sasa tumesikia watumishi wengi wakijitambulisha kama mitume na manabii.

Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Efatha Ministries
Hata wale ambao tulikuwa tukiwatambua kama wachungaji kwa miaka mingi nao sasa wanatambulika kama mitume/manabii au vyote kwa pamoja.Huduma za kitume na kinabii zimeonekana kuwa na mvuto sana kwa siku za karibuni na kuvutia mamia kwa maelefu ya watu hata wakati mwingine kusababisha wachungaji wa makanisa kongwe ya kipentecoste kulalamika kuwa washirika wanawakimbia na kuhamia huko ambako miujiza na uponyaji ni mambo yanayopewa umuhimu mkubwa sana.

Swali kwa wapendwa...;Kama YESU alitoa wengine kuwa mitume,wengine manabii,wengine wachungaji,wengine wainjilisti na wengine waalimu...Je Huduma hizi zinatumika vile ipasavyo? Ni kweli kuwa zinapewa umuhimu ule ule unatakikana kibiblia?
Ni kweli kuwa huduma za kitume na kinabii zinazipa nafasi ya kutosha huduma kama uchungaji,uinjilisti na ualimu kwa maana yake?
Ni kweli kuwa makanisa kongwe ya kipentecoste yanazipata nafasi huduma na kitume na kinabii kama ofisi na kama yanavyozipa nafasi huduma za kichungaji, kiinjilisti na kinabii?
Mheshimiwa Nabii Joedavie wa Ngurumo ya Upako











Mtume Vernon Fernandez wa Agape Ministry (ATN)

6 comments:

Anonymous said...

Mtumishi tatizo hapo sio hizo huduma, bali ni utendaji wa hao waliojipa hizo huduma. Kwa mfano naliwahi hudhuria huduma zinazoendeshwa na mmojawapo wa hao uliowataja, maneno wanayotumia kwenye huduma zao hayana staha hata kidogo kwa neno la Mungu, Kristo na hata kwa sirika lao wenyewe. Huwezi simama madhabahuni na kutumia maneno kwa mfano "..washkaji bro Jesus yuko hapa kumpa kila mtu dozi kama atakavyo..." Mwingine nalimsikia akisema "...Oyaa wagonjwa wote simama juu na kimbia madhabahuni hapa kuchangamkia tenda ya uponyaji..." Mwingine nikamuona kwenye TV akiadhimisha ibada ya Valentine na washirika wake tena kwa mavazi yaleyale wayavaayo siku hiyo. Sidhani kwa misingi kama hiyo ndo inavyopasa kazi ya Mungu itendwe.

Kuhusu miujiza, hiyo haitishi na waifuatao ninawapa pole kwani Mtu wa Mungu hatambuliwi kwa miujiza bali upako wa ki-Mungu na matendo yake. Hatusomi eneo liwalo lote kwenye biblia kwamba Yohana mbatizaji alisifika kwa miujiza bali neno na matendo yenye nguvu ya Mungu ndani yake.

Hivyo basi kwangu huduma zote ni sawa cha msingi zitendwe kulingana na neno lisemavyo na sio mtaji wa kujipatia umaarufu na kuongeza kipato binafsi huku washirika wakiwa walalahoi na zaidi wakiukosa ufalme wa Mungu kwa sheria walizotungiwa na hao wenye huduma!

Mbarikiwe!

Anonymous said...

No comments for that....umemaliza yote mpendwa..
ubarikiwe

Anonymous said...

Biblia haikatazi kuhukumu, kama wengi wanavyosema au kufikiri, biblia inakataza unafiki,hukumu za kinafiki.ILa ukijiona wewe ni wa kiroho onya,karipia,shauri,chunguza, zijaribuni hizo Roho, je wayafanyayo yanaendana na neno la Mungu???

Anonymous said...

Kwa kweli nami nashangazwa sas na baadhi ya watumishi,nashukuru kwa aliyetoa maoni tarehe 13/3/2008 kwani katika vitu ambavyo havinibarki ni hivyo vyote alivyovitaja hapo juu,eti umite Bwana Yesu aliyekufa kwa ajili yako msalabani ''UNCLE JESUS'',valentine KANISANI JAMANI!!!Bwana atusaidie.

Kuna wengine pia wanawaombea watu kwa kuwasukuma,kuwakumbatia,kwa kweli hamtukuzi Mungu.

Pia watumushi wasemana kwenye mahubiri,yaani siku hizi wewe angalia TV siku za mahubiri,huyu akisema hiki anayefuata anapinga,jamani watumushi hubirini NENO LA MUNGU,acheni kurushiana maneno madhabahunu,muogopeni Mungu aliyewaita mtumike,hebu kumbukeni mlipookoka mwanzoni mlikuwa hivyo kweli?mbona mnaacha ushuhuda wenu wa kwanza??? Na ninyi watazamaji someni biblia ili mjue vema neno msije kuyumbishwa.

Bwana atusaidie sana

Anonymous said...

Watume wapo, manabii wapo, wainjilisti na wachungaji pia wapo. Shida ya wakristo wapentekoste wakongwe hawataki kuwatambua wahudumu waliotokea hivi karibuni. Hakuna mhudumu aliyekamilika, kila mmoja ana mapungufu yake, kwa hiyo kama wanatoa neno la Mungu, sisi tusiwapige vita ila tuwaombee na kuwashauri. Hata akina mzee Kulola walipoanza injili walikuwa na makosa yao ya kibinadamu ila baada ya kukua (kwa miaka mingi) sasa hivi wanaelekea karibu na ukamilifu wa huduma zao. Hii inachukua muda wapenda tuvumiliane, tusikatane mapanga wenyewe kwa wenyewe. adui yetu ni shetani na siyo hao watume.

Anonymous said...

Mungu kaweka hizi huduma toka siku nyingi sana ila binadamu wanapinga kwa sababu ya maslahi yao binafsi
Huduma za kinabii zina saidia kanisa kuona mbele n,,,,,,,,,,,,,,,,,. Lakini utakaa ndani ya kanisa usiloweza kuponywa na Yesu???????? haiwezekani!!!!!!!
T7uache tu ushabiki wa washirika, Mimi nimewaona wenye shida pale kwa Geordavie Mungu akiwa nyanyua toka Mautini hadi uhai mpya!! Ashukuriwe Mungu aliyewapa wanadamu Uwezo wa kutumika kwa ajili ya utukufu wake.