Monday, March 10, 2008

Mkoa wa mbeya

Mkoa wa mbeya ndio unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya makanisa au madhehebu karibu kila kona ya mji(hii ni kwa takwimu zangu na sio rasmi).Ni mkoa uliobarikiwa kwa mambo mengi.Kuanzia vyakula vya kila aina, hali nzuri ya hewa, uchumi mzuri na kadhalika.Pia Mbeya inaongoza kwa kutoa wanasiasa na wasomi mashuhuri hapa nchini kama akina Prof. David Mwakyusa,Pro. Mark Mwandosya,Dr. Harison Mwakyembe na wengineo wengi.Mbeya imetoa watumishi wakubwa mashuhuri wa Mungu kama Bishop Ranuel Mwenisongole,Pastor Mwanjala,Mwalimu Christopher Mwakasege na wengine wengi sana tunawaojua wanatokea mbeya.Kwa idadi ya watumishi wa Mungu kuna idadi kubwa sana ya watumishi wanaotokea mbeya.
Inasemekana kuwa mbeya ni miongoni mwa mikoa michache ilioyokuwa ya kwanza kabisa hapa nchini kupokea ukristo ( sina uhakika na hili).

Cha kusikitisha ni kwamba, Mbeya ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa hivi sasa kwa mauaji ya kutisha ya kikatili kabisa ambayo hayaelezeki.Mara nyingi tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa watu wamechunwa ngozi, maalbino kuuwawa kinyama na ujambazi wa kutisha.Mara nyingi matukio haya yamekuwa yakiunganishwa na vitendo vya kishirikina.Mbeya ni miongoni mwa miji ambayo huwezi kutembea usiku peke yako na amani hata kidogo kwani huwezi jua wachuna ngozi watatokea wapi muda huo.

Mbeya ni mmoja kati ya mikoa inayoongoza kwa idadi kubwa sana kwa maambukizi ya ukimwi.Ngono imekuwa ni kitu cha kawaida sana mkoani humo kiasi kwamba hata night clubs na casinos kama Mbeya Carnival vimeanzishwa na vimekuwa vikipata wateja wengi kupita kiasi.

Jamani wakazi na wenyeji wa mkoa wa Mbeya, wakati umefika sasa amkeni, mjifunge magunia muingie katika toba ya kuuombea mkoa wenu kwani shetani amawakamatia pabaya.

Biblia inasema katika 2Nyakati 7:14 "..ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu...watajinyenyekeza kwa kutubu makosa yao ..na kuacha njia zao mbaya...nitaiponya nchi yao na kuwasamehe makosa yao..."

1 comment:

Anonymous said...

Neema inapokuwa nyingi ndipo na uovu huongezeka!