Tuesday, March 25, 2008

Uamsho wa kiroho Mtwara

Nimekuwa Mtwara mara kadhaa lakini ni hivi majuzi nimetoka huko tena.Nilifanikiwa kutembelea makanisa machache ya kiroho huko.

Nimefurahishwa sana na uamsho mkubwa wa kiroho unaoukumba mji huo mdogo ulio kusini mwa Tanzania.

Makanisa mengi yamechupua huko na watu wameingiwa na uamsho wa ajabu kumpenda Mungu.



Pengine hii inaweza kusabishwa na makampuni makubwa ya uwekezaji yanayokimbilia mtwara kwani kuna mradi mkubwa wa kiserikali wa kuendeleza so called "Mtwara corrido" (sijui kama nimepatia kiingereza).


Makampuni kama Artumas yameleta wafanyakazi wengi sana na mzunguko wa pesa kwa kweli ni mkuwa.

Artumas ndio wanaochimba gas inayopatikana huko mnazi bay na inaaminika gas na mafuta yaliyopo maeneo ya mikoa ya kusini inaweza kuchukua hata miaka 500 kuja kuimaliza.
Kweli Mungu ameibariki Tanzania.






Haya shime kwa wale mitume,manabii,wachungaji,wainjilisti na waalimu opportunity ya uwekezaji kiroho ipo tele huko,twendeni jamani maana huko kuna "maji tele"





Maelezo ya picha.


Picha ya kwanza:

Bango la Kanisa la International Evengelism Church (AGAPE).

Picha ya pili:

Hapo ni baadhi wa washirika wa moja ya makanisa yanayochipukia kwa kasi sana Mtwara mjini wakitoka ibadani.

Picha ya tatu:

Kibao cha kanisa la Tanzania Assemblies Of God Mtwara Mjini.(TAG ni moja kati ya makanisa ya kwanza kabisa ya kiroho kufika Mtwara)

1 comment:

Anonymous said...

Nimefarijika kusikia kwamba injili inazidi kuleta watu wengi kwa Yesu hata maeneo kama Mtwara au kusini mwa Tanzania, naamini tunayo kazi ya kuzidi kuomba ili Mungu atuwezeshe watumishi wengi kwenda maeneo ya vijijini kuliko sasa ambapo huduma nyingi za kiroho zinafunguliwa Mijini na kuota kama uyoga na kusababisha kunyang'anyana washirika wakati kuna vijiji ambavyo bado injili haijafika.
Mungu akubariki sana kwa kutupa habari za sehemu kama hizo ili tuweze kuomba zaidi.

Lazarus Mbilinyi
Canada