Wednesday, March 5, 2008

Ukimya wa tume ya kudhibiti imani potofu

Mwishoni mwa mwaka jana tulisikia kwenye vyombo vya habari hapa nchini kuwa baraza la maaskofu wa kipentekoste (PCT) liliamua kuunda tume ya kudhibiti imani potofu zinazodaiwa kuibuka kama uyoga hapa nchini.
Kulikuwa na maoni mbali mbali ya wadau kuhusiana na kuundwa kwa tume hiyo huku wengine wakiiunga mkono na wengine kuipinga, ilimradi kila mtu alikuwa na uhuru wa kujieleza kama katiba ya nchi inavyosema.
Wapo waliosema kuwa kuunda tume hiyo ni makosa kwa kuwa ni kinyume na maandiko matakatifu ya Biblia.Wapo wale walioiunga mkono kuwa tume hiyo imeundwa kikibiblia na kuwa itasaidia kudhibiti kuibuka kwa imani potofu hasa huduma za maombezi zinazoibuka kila kukicha.
Kumekuwepo na maneno ya chini kwa chini yanayoendelea yakizitaja baadhi ya imani hapa nchini kuwa zipo kwenye black list ya tume hiyo.
Wengi tunasubiri majibu ya matokeo ya uchunguzi uliofanywa na tume hiyo.
Blogu yenu ya sayuni bado inafuatilia kwa karibu majibu ya uchunguzi huo na mara tukiyapata tutawatangazia.

Askofu Sylvester Gamanywa ndiye mwenyekiti wa PCT kwa hivi sasa.

2 comments:

Imani martini said...

UTADAIWA VINGI GAMANYWA

Anonymous said...

Nilisikia imani ya misukule nayo imetajwa.Utade hebu tupe habari zaidi za yanayojiri tafadhali