Tuesday, July 8, 2008

Angela Deo Lubala awa miss Temeke

Yule mtoto wa askofu wa kanisa la World Alive Mchungaji Deo Lubala anayechunga kanisa lililopo sinza mori jijini Dar jana amechaguliwa kuwa miss Temeke.Soma habari zaidi na picha za tukio nzima hapa chini.
Angela Luballa (18) ameunyaka Miss Temeke 2008, baada ya kuwashinda wenzake 11 na anatarajiwa kuungana na washiriki wenzake katika kambi ya Miss Tanzania wiki hii.
Angela, alitwaa taji hilo, katika shindano liliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Changombe Temeke Dar es Salaam jana usiku.Mwandaaji wa shindano hilo, Benny Kisaka ndiye aliuyemtangaza mshindi huyo ambaye anayemfuatia ni Rona Swai aliyeshinda pia taji la kipaji ‘Miss Talent’ akifuatiwa na Florence Josephat, huku Lilian Shayo akishika nafasi ya nne na Caroline Joseph ya tano.Wanamuziki baba na mwana, Zahir Ally Zoro na Baba Zoro, walipamba onyesho hilo kwa nyimbo ya kusindikiza warembo huku Big Brother II Richard, akiwa mgeni mwalikwa pamoja na miss Temeke 1997, Miriam Odemba na warembo kadhaa waalikwa wakiwamo wachezaji wa timu ya The Express walihudhuria.Washiriki waliopanda jukwaani juzi ni Zainabu Ally, Frolence Josephat, Evanuv Isaac, Caroline Sechuma, Lilian Shayo, Groly Charles, Radhia Omary, Angella Luballa, Rona Swai, Shabia Ally, Nunu Hussein na Mwasha Ramadhan.Pichani Miss Temeke 2008, Angela Luballa (katikati) katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rona Swai (kulia) mshindi wa tatu, Florence Josephat ( kushoto) .Picha nyingine ni ya Richard akijiandaa kumtangaza Miss Talent na nyingine mamisi wakijimwayamwaya ukumbini

Habari hii tuliwahi kuwaletea hapa mlimani sayuni wakati Angela alipochaguliwa kuwa miss Chang'ombe na ushindi wake kuzua mjadala mzito hapa jijini kwa mtoto huyo wa mchungaji wa kanisa la kipentecoste nchini kushiriki mashindano hayo huku akikungwa mkono kwa asilimia 100 na baba yake na mama yake ambao ni watumishi wa Mungu.Wakati anashinda miss Chang'ombe Mchungaji na Askofu Deo Lubala alipoulizwa kuhusu kuunga mkono mtoto wake huyo anayedai kuwa ameokoka alisema kuwa hakuna ubaya wowote kwa binti yake kushiriki mashindano hayo kwani ni njia ya kumhubiri YESU.

Picha chini Angela Deo Lubala (mwenye namba 8 kiunoni) akiwa na washiriki wengine wa miss Temeke wakifanya mazoezi makali ya kunengua kabla la shindano hilo mapema week iliyopita.






2 comments:

Anonymous said...

Hayo mambo hayatufai huku. Yaliwatokea puani watu wa Shani Ngomeni.

Anonymous said...

Umalaya, Umalaya, Umalaya, Umalaya, Umalaya, Umalaya, Umalaya, Umalaya. HATUUTAKI KANISANI!!!!!!!!!